Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania


Mkuu umechanganua vizur sana hapo hakuna uchawi kama tutaendelea kuamini uchawi tutazid kupotea kila siku
 
Nafikiri kuna jambo la kufikiri zaidi ya hapo maana ajali zimezidi katika kipindi hiki kifupi na madereva hawakubadilishwa na ni hao hao waliokuwa wanaendesha lakini ajali chache...kwanini zimeongezeka mara dufu sasa?
 
Abiria jamani tuwe wakali tunapoona dereva anafanya mzaha na maisha yetu
 
Hebu turudi kwa Ma Sheikh na Ma Askofu watuambia miezi hii ktk hizo siku za nyuma kulitokea nini....kama ilivyoandikwa kwenye vitabu vitakatifu.Hapo hamna Ramli chonganish itakuwa ni facts tu.
 
Mimi nadhani hili siyo la serikali tu, maana siyo serikali inaendesha au kumiliki hivi vifaa. Ni wakati wa mimi, wewe na watanzania wote kwa pamoja kukaa chini na kutafakari kwa makini ili kuleta ufumbuzi wa tatizo hili kutoka kwa mtu moja moja, familia, jamii na taifa kwa ujumla. Vifo hivi havichagui huyu ni wa serikali, wachama Fulani au kabila au dini Fulani. Kwa hiyo lina hitaji soluhisho la jumla kutoka kwa kila moja uwe dereva, abiria au mpita njia n.k niulize kwa nafasi yako wewe unamchango kiasi gani kuepusha ajali. Je ukipanda gari dereva akiendesha sana unasema/unakemea, je wewe dereva nini hasa kinakufanya uendeshe kwa kasi hadi kuhatarisha maisha yako, ukiendesha gari unakumbuka kuwa kunaajali na unaweza kuua, je unamweleza tajiri matatizo ya gari, je unakunywa ukiwa unaendesha, unafurahia kazi yako. Wewe tajiri unasikiliza mahitaji ya dereva, mahitaji wa gari yako. Unapochangua route unaangalia ubora wa gari yako, inafanyiwa matenegenezo kwa wakati na kiwango. Wewe polisi uliyepokea elfu 20000 baafa ya kuona hitilafu nafsi yako inajisikia vipi ukisikia gari hiyo imepata ajali na kuuwa watu wengi wasio na hatia,. Tukifanya hivyo kila mmoja kwa nafsi yake upo uwezekano wa kupata ufumbuzi wa jumla.
 
Hebu turudi kwa Ma Sheikh na Ma Askofu watuambia miezi hii ktk hizo siku za nyuma kulitokea nini....kama ilivyoandikwa kwenye vitabu vitakatifu.Hapo hamna Ramli chonganish itakuwa ni facts tu.

Soma mada inayoendelea kwenye watsap kuhusu hizi ajali

TAHADHARI KWA UMMA WOTE TANZANIA. Ifahamike kuwa kuanzia tarehe 11 hadi 20 ya kila mwezi wa nne kila mwaka huwa ni siku mahususi za kutoa sadaka (kafara) kwa Wajenzi Huru katika lugha ya kigeni ( Freemasons ) kwa kile kinachoamika kuwa ni utekelezaji wa agizo ambalo mwanachama (member) hulikubali mara ya kwanza anapokuwa amejiunga na kundi hili la Wajenzi Huru. Kuna baadhi ya Watanzania wenzetu waliokwisha jiunga tayari na hili kundi na sasa wapo katika hatua ya kutekeleza ahadi zao hizo za Kimasonia za kila terehe 11 hadi 20 ya mwezi wa nne kila mwaka. Ndani ya hizo tarehe huwa kunakuwa na mfululizo wa kuwepo kwa matukio mbalimbali ya umwagaji damu hususani matukio ya ajali za magari ambazo uhusisha mauaji makubwa ya watu kwa kumwaga damu aidha kwa kupoteza maisha kabisa au kupata majeraha mbalimbali yatoayo damu kwa wingi. Kwa kipindi hiki cha utoaji sadaka kwa hili kundi la Wajenzi Huru (Freemasons) ni vema sana kuwataarifu ndugu,rafiki na jamaa zako wa karibu kujiepusha na safari zinazohusiana na magari kwa kusitisha safari zako hadi pale hizo siku za Kimasonia (Masonic Days) zitakapopita. Ifahamike kuwa utoaji sadaka kwa njia za ajali za magari inakuwa ni rahisi sana kwa sababu Wajenzi Huru wote hupata urahisi huo katika upatikaniji wa damu na pia lazima kutakuwa na umati wa watu tofauti na ajali nyingine,umati mkubwa wa watu kukusanyika katika ajali huwapa nguvu Wajenzi Huru hao. Basi ni vyema kuwaepusha uwapendao kwa kuwahabarisha kwa ujumbe huu,okoa maisha yao dhidi ya sadaka ya Wajenzi Huru katika kipindi chao hiki. Tumuombe Mungu kupitia imani za dini zote ili kwenda kinyume na hizi nguvu za kibinadamu zisizo na mamlaka mbele za Mungu,Ameni. TAHADHARI WASAIDIE UWAPENDAO KWA KUWAHABARISHA JUU YA HIZI NGUVU ZA GIZA. SITISHA SAFARI HADI HIZO SIKU ZITAKAPOKWISHA.
 
Jeshi la police limeshauri kuwekwa adhabu ya kifungo cha maisha kwa dereva atakae sababisha ajali na kuua na kudai haiwezekani auwe watu 20 au 30 aishie kulipa fain sh, 30,000
 

Attachments

  • 1429332203105.jpg
    43.2 KB · Views: 163
Mie ningeshauri iwe miaka 15 ili ilete unafuhu ila kifungo cha maisha nashauri wafungwe wanaoiba pesa ya serikali na mafisadi
 
Si sahihi maana hata uliyeleta hii habari bila shaka utakuwa dereva tu kwa kuwa unamiliki gari, siku ukigonga bahati mbaya unalo.....
 
Ajali zilianza tangu gari zilipoanza kutengenezwa la kushangaza mpaka leo karne ya 21 serikali imeshindwa kujua sababu za ajali, inasikitisha sana.
Kumfungia license dereva sio suluhu, dawa ni pindi dereva anapofanya kosa ahojiwe alipata wapi hiyo license na alifanya wapi mtihani na akisuasua tu apigiwe mwenye basi atume dereva mwenye licence halali na huyo apigwe picha ili ajulikane na akatafute ya uhalali.
Dereva atakaeshikwa kalewa afungwe na hefty fine.
Lingine wakandarasi wa barabara mbovu wafungiwe
 
Kama ilivyo pale Angaza kwenye kipimo cha UKIMWI wakati wa kusubiri kupima na kupokea majibu ambapo wadau waliokwenda kipima wana kaa reception huku wakiangalia video za ukimwi, na jinsi vifo vinavyotokea na miili ya marehemu kuzikwa huku ndugu na jamaa wakiwa na huzuni ya hali ya juu.

Vivyo hivyo iwe kwenye video za kwenye mabasi, na yale ambayo hayana yawekewe video na iwe ni sheria na lazima video ziwe za ajali ya mabasi Tanzania kwani naamini tukiunganisha taarifa za habari za television tutakuwa na documentary ya nguvu. Hii itasaidia abiria kumkanya dereva na crew members wote wa basi husika mara watakapotaka kufanya upuuzi.

Video inakuwa on mwanzo wa safari mpaka mwisho, halafu video hizo zichezwe na sehemu ambapo abiria wanasubiria kusafiri - stand ya basi.
 
siungi mkono maneno yako kwani hata angaza wanachofanya sio sahihi unampa mtu ushauri nasaha uku unamtisha na mapicha ya kufa kufa
 
Ndugu wanajamvi habari ya asubuhi, nimekaa kwa muda mreefu sana nafiiri bila kupata majibu
Kwanini ajari haziishi? Kwanini iwe Tanzania pekee? Kwanini asilimia kubwa ya hizi. Ajali zinatokana na malori+mabasi?
Kwanini ajali hazihusishi na magari mapya?
Kutokana na tafakari zangu nikaona serikali haina budi kufuta bima za magari makubwa yote yaani malori pamoja na mabasi
Kufanya hivyo Najua wazi kabisa wamiliki wote wa magari ya namna hiyo lazima watakuwa wakali dhidi ya watumishi wao kukwepa hasara, na hiyo ndo itakuwa dawa ya kukomesha ajali Tanzania.
Kitu kingine serikali kwanini isitenganishe muda tofauti wa magari hayo kusafiri? Ili mabasi yawe yanasafiri mchana tu na malori iwe marufuku kusafiri mchana tuone mabasi yatagongana na nini Tena

Au wewe unamawazo yapi tofauti na yangu?
 
Hiyo inaweza ikawa solution lakini serikali haiwezi kukubali kwasababu itapoyeza pesa nyingi sana lakini kw upande flani watakuwa wameokoa maisha ya watu kwa kiasi flani labda serikali ingealia upya swala ulipwaji wa bima. Mtu ukipata ajali unalipwa nusu ya ile gari au haulipwi kabisa ikiwezekana ktk mazingira flani ivi wewe ukiilpwa na bima na wewe inabidi uilipe serikali
 

Kwa upande mwingine....fidia ya upotevu wa mali,maisha ya abiria na wenye mizigo(kwa malori) italipwaje? Usiangalie mwenye basi/Lori tu,insurance ina cover na wengine pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…