gda sparta
Member
- Apr 10, 2015
- 30
- 9
Maombi hayawezi kuzuia ajali. Muhimu ni kufanya yafuatayo:
1. Kutengeneza barabara za maana. Siyo vichochoro ccm wanatutapeli eti ni barabara. Barabara gani imejaa matuta, nyembamba ka njia ya waenda kwa miguu? Huu utakuwa ni uchizi
2. Vyombo vya usafiri vya maana
Magari yakiwemo mabasi, vipanya, magari binafsi na milori, huwa vinaingizwa nchini katika kiwango cha mwisho ambapo hakitakiwi kutumika katika nchi kilikoanzia kutumika. Mataifa tajiri hutumia njia hii ku dispose of machine chakavu. Tanzania ndiyo huwa tunanunua. Hata kama uwezo wetu uko chini, lakini tumezidi kunua scraper. Zingine hazitengenezeki, kwa nini zisiue watu?
3. Madreva wasio na uwezo
Hili siyo katika kusababisha ajali tu, bali pia kusababisha usumbufu barabarani. Jams nyingi zinasababishwa na madreva waso na ujuzi.
4. Tabia ya kibongo bongo ya kutojali maisha au mali ya wengine
Kutojali ni shida sana. Mtu anaamua kuharibu au kumdhuru mtu kutokana na kutojali. Hii ni mifumo ya kifamilia zaidi iliyoharibika. Watu katika families nyingi za kibongo hawawafundishi watoto au members wengine kujaliana. Ubinafsi wa kipu.uzi. Fikiria mtu anaovateki kwenye kona ambako pamoja na kuwepo alama za barabarani na yeye kuona hali halisi, bado anaovertake.
Kwa hayo yote, hakuna utachomuomba Mungu akakusikiliza. Ataona kama wewe ni mzembe flani na wala hujui unachokiomba. Sioni cha kuomba, tufanye kazi tupate pesa, tujenge barabara za juu na ardhini na tuweze kununua magari mapya. Njia nyingine ni za kubahatishaaaa
Mkuu umechanganua vizur sana hapo hakuna uchawi kama tutaendelea kuamini uchawi tutazid kupotea kila siku