Mkuu katika visababishi hivyo vya ajali vinatofautiswa na % ya prevalence.
Katika list uliyotoa lion's share - zaidi ya 80% ajali zaletwa na mwendokasi uliopitiliza.
Kisichoongelewa hapa ni unachoona exemption ya makundi fulani fulani katika udhibiti mwendo. Inahitajika jitihada ya ziada kuona hii actually ni ni divide and rule ya kujiwekea na kufanikisha kuwapo kwa RUSHWA makubwa makubwa tokea kwa samaki wakubwa kwa maslahi mapana ya wala RUSHWA hawa.
Wajua katika ajali yoyote ndogo au kubwa vehicle inspector lazima ale vilivyo?
Ni kwa malengo yao hayo ya mbali wamefanikiwa sana kutufunga midomo kudhani kuwa twanufaika na hizi unlimited speed barabarani kwa kuwa na private vehicles kumbe in actual fact si kwa manufaa yetu.
Hili la unlimited speed barabarani (mark my words) halipo duniani labda kwa Tanzania hii tu ya viwanda vya cherehani.
Sheria za nchi yetu zipo vizuri tu na zimeelekeza kila kitu na hata kanuni za udereva wa kujihami zipo na vitabu vipo.
Vyuo vipo watu hawataki kwenda kusomea udereva wanabaki na lawama kwa jeshi la polisi.
Mtu umepata leseni kulingana na uwezo wako wa kuendesha lakini unataka ujionyeshe barabarani kuwa unaweza kuendesha kwa mbwembwe nyingi na speed kubwa kwa kujidanganya kuwa huna Limit ya speed.
Limit ipo kwenye kwenye alama za barabara.
Ukiona kibao cha speed 100 huruhusiwi kuendesha zaidi ya kiwango hicho. Na kama haujui ni wajibu wako kutafuta elimu Darasani au kuwatafuta Wataalam wa mambo ya uchukuzi au wakaguzi wa magari uwaulize.
Tatizo Watanzania wengi wanadharau mambo mengi na kujifanya kuwa wanajua.
Profesa anajiona yeye hawezi kukaa darasani na kujifunza udereva wa kujihami anaona ni elimu ndogo sana.
Matokeo yake bosi yupo kwenye gari na ana leseni na hua anaendesha gari ya nyumbani lakini anaendeshwa na dereva hovyo barabarani bila kumkemea kuwa anakiuka kanuni za bora za udereva na maadili take.
Wasimamizi wa sheria tutawalaumu bure mana wao wanajutahidi kuadhibu kama kanuni na sheria zinavyowaelekeza.
Elimu inatolewa kabla ya kosa kutendeka lakini ukisha vunja sheria jukumu la wasimamizi wa sheria ni kukuadhibu kwa mujibu wa sheria inayohusika.
Ingekua ni masuala ya kutoa elimu basi watu wangeomba wapekekwe mahakamani ili wakapewe elimu na hakimu.
Watu wanashindwa kutofanutisha kuonya na kutoa elimu.
Elimu inatolewa kwa wajinga na wale wanaotaka kujiendeleza ambao wao wanaelimu Ila wanaamua kusoma zaidi.
Sasa sio kazi ya Askari barabarani kumfundisha dereva alama za barabarani wakati yuko ndani ya gari anaendesha .
Lakini ni jukumu la wasimamizi hao wa sheria kutoa elimu mashuleni na kwa watembea kwa miguu wasiojua sheria na kanuni za usalama barabarani.
Ndio maana Mara nyingi wanafanya hivyo kwa abiria lakini sio kwa madereva.
Ni vizuri madereva hasa wa magari binafsi wakatafuta vitabu vya kanuni za udereva wa kujihami kwa Walimu wa NIT au Veta.
Ni kwa faida ya Taifa na wao wenyewe.
Sioni sababu ya kutegemea huruma ya Askari wakati mtu amevunja sheria kwa makusudi.
Askari tuwalaumu kwa kubambikiza makosa yasiyopo kama vile kumwandikia mtu faini kwa sababu gari INA vumbi. Hapo kama atafanya hivyo basis tumlaumu lakini kwa mwendo kasi kwa kuvuka Taa nyekundu,kutofuata alama za kukataza kupita gari jingine.
Kutozingatia speed ya wastani kwenye makazi ya watu ambayo sheria iko wazi kuwa isizidi 50km/hr. Hapa kwa kweli tusiwalaumu wasimamizi wa sheria.
Mara nyingi madereva wanawashawishi askari kwa kutoa rushwa baada ya kufanya kosa.
Kama huna kosa huwezi kutoa Rushwa kamwe utakua ni ujinga wa kupitiliza.
Kama sina kosa mtu akiniandikia nitakwena mpaka kwa Rais kama IGP hatanisikiliza.
Yani gari yangu taa zinawaka halafu uniandikie faini kuwa haziwaki. Itakua ni balaa la hatari.
Kwenye speed 50 ukitembea 48 nani atakuandikia?
Tukitimiza wajibu wetu kama madereva nadhani tutabaki kwenye suala la miundo mbinu na Ubovu wa gari lakini kwa dereva aliyesoma udereva hawezi kuendesha gari bovu.
Kitu cha kwanza kabisa kufundishwa kwenye udereva ni namna ya dereva kukafua mifumo muhimu ya gari.