Tumekua na ajali za mara kwa mara ambazo haziishi lakini sidhani kama mpaka sasa vyanzo hivi muhimu vya ajali vinazungumziwa zaidi ya kuambiwa tatizo ni mwendo kasi, na Uzembe wa dereva.
Fatigue, Umasikini, Ubovu wa barabara, Elimu ndogo ya vyombo vya moto, Elimu ya msingi (std 1 to std 7), pia ni vyanzo vikubwa sana vya ajali hapa Tanzania.
Nitaelezea kwa uchache na wengine wataweka nyama.
FATIGUE (UCHOVU):
Madereva wengi wa malori, mabasi na hata gari ndogo huwa hawapumziki vya kutosha kiasi cha kufanya safari ndefu, Madereva wa mabasi na malori husafiri mamia ya km lakini huwa hawalali vya kutosha kiasi cha kuwa na nguvu ya kuanza safari siku inayofuata. Wengi wa madereva hawa wakifika kwenye vituo vyao vya kupumzika huanza kufanya starehe kwa maana ya pombe na umalaya na matokeo yake asubuhi huamka na hangover ya K**MA na POMBE, hangover ya hivi vitu viwili ni usingizi na uchovu kupitiliza siku ya pili yake. Elimu ya kujitambua na kuirasimisha hiyo ajili ndio muarobaini pekee kwenye hili, vijana wanahitaji elimu ya kutosha ya kujitambua na Serikali iifanye hiyo kama ajira rasmi kwa maana ya watu walipwe mishahara, night allowance's na wawe na mikataba inayotambulika kisheria wakatwe PAYE NA HIFADHI YA JAMII.
UMASIKINI:
Jamii nyingi sana za kitanzania ziko kwenye umasikini mkubwa na huu umasikini ni chanzo cha matatizo mengi sana Tanzania.
Jamii nyingi za kimasikini ndio zimetoa hawa madereva wengi wanaoendesha roho za watu huko barabarani, na jamii hizi za kimasikini zimekuwa tegemezi sana kwa hawa ndugu zao ambao ni madereva wetu, Shida/Umasikini huleta stress na mwisho wa siku hupunguza umakini barabarani. Dereva huyu anapenda kuwapa wanae elimu bora kama wengine maana anaona mateso anayoyapata yeye barabarani, Dereva huyu anahitaji kusomesha ndugu zake wapate elimu bora, Dereva huyu anahitaji kuwa na nyumba bora ya kuishi, Dereva huyu anahitaji kuwapa matibabu ndugu na wanae, Dereva huyu anahitaji kuwa lishe bora watoto wake, Dereva huyu anahitaji kulea wazee wake choka mbaya wanaishi kijijini huko, HAYO YOOTE MWISHO WA SIKU HULETA STRESS KWA HUYU DEREVA NA MATOKEO YAKE NI KUPUNGUZA UMAKINI AU KUTOKUWA MAKINI KABISA.
Serikali au wenye mamlaka lazima watambue umasikini ni tatizo kubwa Tanzania na tukiwatoa watanzania kwenye umasikini tutakuwa tumetatua mengi, Dereva na ndugu zake wakiwa na kipato kizuri ataishi maisha ya furaha na kazi yake ataifanya vizuri na kwa umakini maana ndio inamuweka mjini ( mfano Madereva South Africa, Botswana, Namibia,Zambia pale London, USA nk).
UBOVU WA BARABARA:
Tanroad jaribuni kuwa na road patrol za mara kwa mara kila mkoa, kila wilaya ili mjue matatizo yaliyopo kwenye barabara zebu na muamue haraka, uzibaji wenu wa viraka bado ni wakizamani na huchukua muda mrefu, barabara zinakaa na mashimo na mibonyeo kwa muda mrefu sana (hapa ni vyema kila Tanroad mkoa ikawa na fungu la emergency){naikumbuka ajali ya basi la MAJINJA PALE KATI YA IRINGA NA MBEYA NA LILE KONTENA CHANZO NI LILE SHIMO PALE).
Tanroad ni vyema mpeleke watu wenu nje wajifunze namna bora ya usimamizi na ujenzi wa barabara ili mwisho wa siku tuwe na Standard yetu ya ubora wa barabara zetu ili kila mjenzi akija tunampa specifications zetu, Kona zisizo na msingi ni nyingi kwenye barabara zetu kiasi cha kutengeneza hatari zisizotakiwa, Maeneo korofi yote yakijengwa mjaribu kuyafanya yawe mapana na ikiwezekana muweke TAA eneo husika ili usiku iwe rahisi. TANROAD NA SERIKALI acheni siasa kaeni chini mchunguze kwa wenzetu ili tupata standard yetu ya ubora wa barabara zetu na tuachane na hizi barabara zinazobonyea na kuchimbika kila siku, kona sehemu zisizohitajika (kifupi makona sio muhimu mbona Kenya hapo wanatushinda hawana kona zisizoeleweka, kule Zambia pia mbona hakuna makona kona kila mahali)
ELIMU NDOGO YA VYOMBO VYA MOTO.
Watanzania wengi wanamiliki na kuendesha vyombo vya moto lakini hawajui matumizi sahihi ya vyombo hivi kifupi wengi hawavijui hivi vyombo sio lazima uwe fundi au proffesional driver hapana hapa tunaongelea General knowledge ya kujua magari na tabia zake mfano huwezi ukawa na IST unataka kuovertake FORTUNER na mbele yako linakuja LANDCRUISER V8 na bado unajiamini utaliwahi, huwezi ukawa na gari yako inachelewa kubadili Gia na wewe huna habari, Ufanyaji wa service kwa wakati na kujua wakati sahihi hii sio kazi ya Fundi, Oil sahihi kwa matumizi ya Gari, Upepo sahihi kwa matumizi ya Gari lako, kwa wale wanaondesha manual kujua wakati gani utumie gia gani, Waendeshaji wa Magari sio lazima uwe umeajiriwa kuna umuhimu wa kulijua gari zako hata kwa kusoma broachure mbali mbali za magari, kuangalia vipindi mbalimbali vya magari, kuzungumza na wataalamu wa magari upate abcd za magari ili ubongo ujue matumizi sahihi ya magari na barabara.
ELIMU YA MSINGI (STD 1- STD 7).
Hii elimu ni nzuri na muhimu sana kwa watu kuwa na uelewa na kujitambua, Elimu ya msingi humsaidia mtu kujijua yeye ni nani na anatakiwa afanye nini, Elimu ya msini humsaidia mtu kujua kusoma na kuandika na hili litamsaidia mtu kujua na kuelewa alama mbalimbali za barabarani, Elimu ya msingi itamfanya mtu kuwa muelewa hata pale anapokosea na kuruhusu kueleweshwa na sio kuwa mbishi, Elimu hii humfanya mtu ajielewe na kuwa na utu barabarani kiasi cha kureport jambo lolote baya alionalo barabarani, Elimu hii humsaidia mtu kuwa na ubongo active kiasi cha kuwa na maamuzi sahihi barabarani.
Watanzania tuitilie mkazo sana elimu ya Tanzania ili watu wengi waweze kuipata, Serikali ni vyema ikahakikisha elimu ya msingi inakuwa bora ili watu wamalizapo shule ya msingi wawe na content sahihi kichwani itakayowawezesha kweli kupambana na mazingira yao, Elimu bora ya msingi ijikite zaidi kwa watu kupata uelewa na kujitambua na kuwafundisha watu mambo yasiyo na msingi, vitu kama alama za barabara,namna bora ya matumizi ya barabara inaweza kuwa kipindi maalumu kwa wanafunzi wa darasa la sita, tusifikirie sana watu kufanya mtihani au mitihani migumu katika level hii hapana ziwepo tu test za kupima uelewa na continuous assessment , Elimu bora ya msingi itajenga watu bora wenye msingi imara ambao mwisho wa siku watatupunguzia matatizo mengi..