Kwanza sijakuelewa unapohusisha rushwa na sheria ya speed limit na ubaguzi wa sheria.
Nimesema tutawalaumu Trafiki bure wakati kazi yao ni kusimamia sheria zilizopo na sio kutunga sheria.
Gari za abiria na gari za mizigo na gari zote zenye uzito wa zaidi ya Tani 3 na nusu ziwe ama za mizigo ,abiria au la zimeelekezwa na sheria kuwa zisizidi 80KM /HR.
Hii ni sheria iliyowekwa na Bunge ambalo lina watu wenye busara ya kitosha na waliozingatia tafiti mbalimbali na mazingira ya barabara zetu.
Wewe kama umewahi kendesha TANKER au Semi Trailer ungejua ni kwa nini hayo magari makubwa yamewekewa speed limit hasa ikitokea jambo la ghafla na dereva akafunga brake.
Magari madogo kama Land Cruiser na Benzi hata kama lipo speed 180 likikutana na jambo la dharura kama dereva analazimika kufunga brake madhara yake sio kama gari kubwa kama basis au Lori.
Hata hivyo magari yote barabarani na madereva wote wanatakiwa kufuata speed signs za barabarani muda wote isipokuwa magari ya viongozi wakati yakiwa yanasindikizwa na king'ora cha polisi kwa ajili ya kutoa tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara.
Kwa hiyo kama kuna alama ya speed 30 km/hr. Hapo hakuna cha basi wala cha private car. Dereva unatakiwa uongee na alama tu.
Kama kuna kibao cha 60km /hr kwenye mteremko au kona hakuna mjadala madereva wote wanapaswa kufuata.
Sasa huo ubaguzi uko wapi?
Speed limit imewekwa kuzingatia utaalam na tafiti zilizofanywa kwa kuangalia uwezekano wa kulimudu gari kubwa au dogo wakati wa dharura. Sio suala la rushwa.
Hata kupata Leseni ya Urubani wa kuendesha ndege za abiria kuna masharti magumu zaidi ya ndege za abiria na hata usimamizi wake ni tofauti lengo hasa ni kulinda abiria wenye lengo la kufika salama. Sio suala la rushwa.
Serikali iko makini haiwezi kutunga sheria za kuhamasisha utoaji wa rushwa.
Ndio maana kuna shule za udereva ili kila dereva asome na kujua kanuni na maadili ya udereva kabla ya kuingia barabarani. Na ajue kuwa anaendesha gari la aina gani na afuate kanuni ili asiangukie kwenye mikono ya sheria.
Mkuu haipo sheria iliyotungwa na bunge inayotaka mabasi, malori zaidi ya tani 3 na nusu kama ulivyosema inayo limit speed yake kwenye 80km/h. Vile vile hakuna sheria ya bunge inayo toa fursa kwa magari mengine yoyote yaliyobakia kuwa ati yana ruksa ya sheria ya kutembea vyovyote bila limit.
Kilichotokea hapa ni matamko tu ya polisi ambayo pia ni kinyume na sheria zinazobebwa na alama za barabarani zilizowekwa na makandarasi na pia TANROADs wao wakajiwekea mabasi na malori speed limit iwe 80km/h. Hii ikiwa ni hata kama kuna sehemu alama za barabarani zinaonesha 100km/h. Hapo hapo wakaendelea na matamko yao yenye kuvunja sheria kuwa magari private yanaweza kwenda speed yoyote hata 500km/h kinyume cha alama zote za barabarani ati kuwa hawa waheshimu 50km/h peke yake.
Cha kushangaza ni hivi hawa wasiokuwa limited kwenye speed, wanatuhakikishia vipi sisi watumiaji wengine wa barabara wakiwamo watembea kwa miguu, pikipiki, mifugo nk,na hata wale kina yakhe tulio kwenye mabasi?
Ninaamini kwa maelezo haya ya awali nimejibu hoja yako ya benz na land cruiser na hizo ulizosema brake za ghafla. Babarani kuna watumiaji wengine. How do we coexist kama kuna vichaa na wenda wazimu na magari yao binafsi wanatembea 180km/h humo humo wakibarikiwa na polisi? Si kuweka maisha yetu sisi rehani kwa tamaa zenu?
Utaona hapa sheria za bunge zinatambua vibao vya barabarani kwa kila mtumia barabara -- hazina ubaguzi. Kwamba palipo na kibao cha 80km/h ni kwa magari yote mabasi, malori, pikipiki na hata magari binafsi. Hali kadhalika katika 50km/h na 100km/h. Tofauti na hapo kwa ubaguzi polisi wamekuja na yao ambayo ni kinyume cha sheria na ni ya kibaguzi au wewe huoni hivyo?
Kwa nini pana rushwa inayopaliliwa kwenye ubaguzi huu?
Mabasi na malori rushwa wanazochukua ni kubwa zaidi. Hawa wala rushwa wamejipanga kupiga bingo kwenye mabasi na malori. Basi moja tu wanakula rushwa ya kutosha magari labda kuzidi hata madogo 100. Mabasi na malori yamewekewa sheria za matamko zisizo rafiki kwa makusudi mazima ili kupalilia rushwa huku private wakipewa incentive ya hakuna limit ili wasihoji kwa niaba ya hawa wanaokamuliwa ili ukamuaji uendelee pasipo na wapigaji kelele kama sisi mitandaoni.
Kwa kukuibia ni kuwa pana polisi wengi tu humu jamii forums. Kwa bandiko hili wote wameingia mitini. Rushwa yake ilivyo hapa walidhani hatuna sababu ya kusema kwani tumepewa incentive ya kutokuwapo na limit barabarani. Inatugharimu maisha lazima tuseme!
Wanajua vyema kuwa sote tungekuwa sawa mbele za sheria, sheria mbovu tungezipigia kelele ingekuwa kuwa na lazima ya maboresho au marekebisho. Hapo wana bank kwenye divide and rule. Wataalaamu hawa wa rushwa kwa matamko ya kibaguzi waliyoyafanya ni sheria wametufanya tudhani kuwa kwa ku limit speed 80km/h kwa mabasi na malori wakituacha sisi huru na speed yoyote tungeamini kuwa wamekuja na mwarobaini wa ajali. Kwa mahesabu yao walijua tutakaa kimya waendelee kupiga pesa ndefu.
Hili la limitless speed ni janga kubwa la kitaifa hatupaswi kulikubali hili.
Tunaingia vipi barabarani wakati pana watu wanaendesha hata 180km/h? Huu ni wendawazimu unaopigiwa chapuo na polisi Tanzania peke yake. Hakuna nchi duniani yenye kitu limitless speed.
Huu ndiyo ule ukweli kuhusu ajali ambao hauongelewi.