Jamani wadau tuache ushabiki hawa madereva wakasome watatuua sana jamani,hata kama ni ndugu zetu,
wengi ni wavuta bangi,wasiosoma,kazi wanayoifanya ni kubwa na Nzuri sana ila hawapendi kabisa kujiendeleza..
hi inakuaje Mtu kaajiriwa kama Operator wa folk lift,operator wa mitambo,au operator wa maji,lakini utakuta wanajiendeleza ili awe mzuri zaidi,na kuweza kupambana na trouble shooting,sasa trouble shutting za kwenye magari ni kifo,halafu hawa jamaa hawataki kabisa kusoma,hata kujitolea kusoma ni wachache sana sana 2 kati ya 45.ok sio mbaya sana basi uanzishwe utaratibu waajiri wao wawapeleke shule,kozi fupi kwa ajili ya kunoa na kuimarisha fani yao.
Technolojia inabadilika kila mara,hata injini,gear box,nk zinabadilika kulingana na uwezo na muda,mtu kasoma miaka 10 tu iliopita anataka kila siku aendeshe kama alivyozoea,changamaoto barabarani ni nyingi sana,
Mimi nachukulia udereva ni kazi kama kazi nyingine za Mitamboni,mtu anaendesha mtambo jamani,ambapo kila baada ya miaka kadhaa say 2,3 kuna kuwa na tathmini ya kazi yako,sasa hawa nani anawatathmini,AJALI NDO TATHMINI YAO..
GARI NI CHOMBO KINARAHISISHA KAZI YA USAFIRI,HIVYO GARI NI MASHINE,HIVYO MWENDESHA MASHINE WA MITAMBONI ANAEFANYA SHIFT,NA DEREVA WA MABASI NA LORI MIMI SIWATOFAUTISHI.
TUBADILIKE Kusoma sio upate Phd,la hasha upate maarifa ya ziada ambayo yanapatikana kwenye fani yako pia u share changamoto unazokumbana nazo barabarani na wenzio.
Ahsante.
Usalama kwanza,kazi baadae.
Safety first,Work later"