Utotole
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,607
- 4,263
cement
Kwanza mimi ningeshauri serikali iwekeze kwenye ujenzi wa barabara. Tunashuhudia ajali nyingi zinazotokea kwenye barabara kuu (highways) huhusisha magari yanayogongana uso kwa uso, aidha wakati wa ku-'overtake' au kukwepa mashimo na wakati mwingine kupoteza tu mwelekeo kwa gari mojawapo na hivyo kuligonga linalokuja mbele yake moja kwa moja.
Pamoja na kushughulika na viwango vya weledi na tabia/nidhamu ya madereva pamoja na ubora wa magari, naamini ni wakati sasa hizi highways zetu zitengenezwe kwa kiwango cha highway. Hapa namaanisha kwamba serikali iwekeze kwenye kujenga barabara madhubuti katika namna ambayo magari itakuwa nadra sana kugongana uso kwa uso. Serikali ijenge barabara mbili zinazojitegemea across all highway routes, mfano wa 'double roads' ili gari inayotoka Dar kwenda Iringa ipite njia yake na ile inayotoka Iringa kwenda Dar ipite njia yake na barabara hizi ikibidi zitenganishwe na kiunga au kingo na nafasi ya kutosha. Ikiwa hivi nina hakika 'it will take the devil himself' on the wheel of one of the cars to achieve a head-on smash between two cars moving in opposite direction.
Na kwa kuwa kila njia itakuwa na uwezo wa kupitisha magari japo mawili kwa wakati mmoja (each direction), hata magari yale yanayoenda uelekeo mmoja hayatakuwa katika hatari ya kukwaruzana kwa kuwa dereva wa nyuma akitaka kumpita wa mbele yake atatumia 'lane' mojawapo kutegemea yule wa mbele yuko lane gani. Hapa hata kukwaruzana haitakuwa kitu cha kila siku.
Hapa zitabaki ajali zinazosababishwa na mechanical failure, dereva kusinzia au kuwa mzembe, unexpected objects on the road, na mengine ambayo as we know of recent...ajali nyingi zilizogharimu maisha ya wengi zimetokana na magari kugongana uso kwa uso. Hali ya barabara zetu ambapo kwa sehemu kubwa barabara ina lanes mbili tu kwa directions zote hufanya magari yapishane kwa karibu sana, jambo linaloongeza uwezekano wa ajali za uso kwa uso.
Sitakubaliana na utetezi kuwa ni gharama sana kujenga barabara za namna hiyo, kwa maana ya ku'double' barabara zilizopo kwa kuwa maisha ya watu yanayopotea kila siku yana thamani kubwa kuliko hizo pesa ambazo nyingi hata hivyo zinaishia kwenye matumbo ya walafi wachache. Vile vile huo ni mpango wa muda mrefu, tofauti na miradi tuliyozoea ya kupigia kampeni, ambayo tunataka ndani ya miaka mitano ikamilike japo kwa kiwango cha hovyo ili chama na wagombea wetu waombee tena kura. Kama tuna maono na dira ya muda mrefu kukomesha ajali hizi, inatakiwa serikali iwekeze kwenye ujenzi wa barabara ya namna hiyo phase by phase.
Likifanyika hilo na masuala yanayohusiana na ubora wa madereva na magari yakafanyiwa kazi, ninayo imani kabisa kuwa ajali zitapungua kwa kiasi kikubwa sana. Lakini kama tukiendelea na barabara yetu moja tunayoiita highway, tutaimba na kuimbiwa parapanda kila siku.

Last edited by a moderator: