Wandugu wapendwa
Nimesikitishwa sana kuona kila kukicha hapa jukwaaani habari kubwa siku hizi ni ajali za barabarani huku watu wengi wasio na hatia wakipoteza maisha. Hili ni jambo baya sana kwa taifa letu na ni wajibu wetu kwa kila Mtanzania kutoa ushauri kwa serikali nini kifanyike kupunguza ajali
Mimi kama Mtanzania, ninapenda kutoa ushauri wa mambo machache tu ambayo nadhani kama yakifanyiwa kazi ajali zitapungua sana nchini
1. Mabasi na malori yote yafungwe speed govenors ili yasikimbie mwendo mkali at least 80km
2. Serikali ipanue barabara kuu kama zile za Mbeya Dar na Chalinze Arusha kuwa na njia nne, yaani mbili kwenda na mbili kurudi .
3. Barabara kuu zote ziwe zimetenganishwa katikati kwa kutumia ukuta mgumu wa zege (Hutasikia tena magari yakigongana uso kwa uso)
4. Alama za barabarani ziongezwe kwa wingi kila sehemu na ziwe visible kwa madereva(SEHEMU NYINGI ZENYE KONA KALI HAZINA ALAMA)
5. Kuwe na Highway patrol ya police kwenye barabara zote kuu
6. Kuwe na ambulance kila baada ya kilomita mia kwenye barabara kuu ili kuokoa maisha ya watu
7. Kuwe na taa za barabarani zinazofanya kazi kwenye barabara zote kuu nchini , hii itasaidia madereva kuwa wanaona vizuri kwani wakati mwingine ajali husababisha na dereva anaekuja kutokea upande mwingine kutumia full beam kwa sababu hawaoni vizuri.
8. Polisi warudishiwe tochi ili wakamate madereva wakorofi
9. Adhabu ya kifungo itolewe kwa madereva walevi
10. Wananchi tuisaidie polisi kwa kureport madereva wanaoendesha magari kwa kuhatarisha maisha ya wengine, tumieni simu zenu kuwarekodi,
Najua kua uchumi wetu ni mdogo na serikali imejitahidi sana kutujengea bara bara nzuri ambazo hatujawahi ziona tokea uhuru, lakini tujue uzuri wa barabara ndio chanzo cha hizi ajali. Madereva wanajisahau sana kwani walizoea mashimo na vumbi tupu, sasa wamewekewa lami wanataka kwenda spidi kuliko hata magari yenyewe