Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

cement

Kwanza mimi ningeshauri serikali iwekeze kwenye ujenzi wa barabara. Tunashuhudia ajali nyingi zinazotokea kwenye barabara kuu (highways) huhusisha magari yanayogongana uso kwa uso, aidha wakati wa ku-'overtake' au kukwepa mashimo na wakati mwingine kupoteza tu mwelekeo kwa gari mojawapo na hivyo kuligonga linalokuja mbele yake moja kwa moja.

Pamoja na kushughulika na viwango vya weledi na tabia/nidhamu ya madereva pamoja na ubora wa magari, naamini ni wakati sasa hizi highways zetu zitengenezwe kwa kiwango cha highway. Hapa namaanisha kwamba serikali iwekeze kwenye kujenga barabara madhubuti katika namna ambayo magari itakuwa nadra sana kugongana uso kwa uso. Serikali ijenge barabara mbili zinazojitegemea across all highway routes, mfano wa 'double roads' ili gari inayotoka Dar kwenda Iringa ipite njia yake na ile inayotoka Iringa kwenda Dar ipite njia yake na barabara hizi ikibidi zitenganishwe na kiunga au kingo na nafasi ya kutosha. Ikiwa hivi nina hakika 'it will take the devil himself' on the wheel of one of the cars to achieve a head-on smash between two cars moving in opposite direction.

Na kwa kuwa kila njia itakuwa na uwezo wa kupitisha magari japo mawili kwa wakati mmoja (each direction), hata magari yale yanayoenda uelekeo mmoja hayatakuwa katika hatari ya kukwaruzana kwa kuwa dereva wa nyuma akitaka kumpita wa mbele yake atatumia 'lane' mojawapo kutegemea yule wa mbele yuko lane gani. Hapa hata kukwaruzana haitakuwa kitu cha kila siku.

Hapa zitabaki ajali zinazosababishwa na mechanical failure, dereva kusinzia au kuwa mzembe, unexpected objects on the road, na mengine ambayo as we know of recent...ajali nyingi zilizogharimu maisha ya wengi zimetokana na magari kugongana uso kwa uso. Hali ya barabara zetu ambapo kwa sehemu kubwa barabara ina lanes mbili tu kwa directions zote hufanya magari yapishane kwa karibu sana, jambo linaloongeza uwezekano wa ajali za uso kwa uso.

Sitakubaliana na utetezi kuwa ni gharama sana kujenga barabara za namna hiyo, kwa maana ya ku'double' barabara zilizopo kwa kuwa maisha ya watu yanayopotea kila siku yana thamani kubwa kuliko hizo pesa ambazo nyingi hata hivyo zinaishia kwenye matumbo ya walafi wachache. Vile vile huo ni mpango wa muda mrefu, tofauti na miradi tuliyozoea ya kupigia kampeni, ambayo tunataka ndani ya miaka mitano ikamilike japo kwa kiwango cha hovyo ili chama na wagombea wetu waombee tena kura. Kama tuna maono na dira ya muda mrefu kukomesha ajali hizi, inatakiwa serikali iwekeze kwenye ujenzi wa barabara ya namna hiyo phase by phase.

Likifanyika hilo na masuala yanayohusiana na ubora wa madereva na magari yakafanyiwa kazi, ninayo imani kabisa kuwa ajali zitapungua kwa kiasi kikubwa sana. Lakini kama tukiendelea na barabara yetu moja tunayoiita highway, tutaimba na kuimbiwa parapanda kila siku.
 
Last edited by a moderator:
Madereva ni wale wale mda wote hapo cha maana ni uchaguzi usifanyike au waganga wa jasi wote wakamatwe ndo ajali zitaisha.
 
Hili linaweza kutokana na imani za kishirikina. Kamatakamata za kuhisi waganga wa jadi na wapiga ramli. Hebu viongozi kaeni nao huenda ndiyo malipizo yao. Otherwise nchi IPO kwenye matatizo makubwa. Tuwaombe radhi viongozi wa dini waiombee. Kitendo cha kuwaua albino watu wasio na hatia ndiyo malipizo ya Mungu. Matendo ya dhuluma na ufisadi. Tutafakari hayo.
 
Mkuu ifanyike survey,una hoja ambayo wengi hawajaiona.Ajali zimeongezeka baada ya Mabasi ya KICHINA kuongezeka.Yawezekana ni mepesi sana kuweza kuyadhibiti kwenye dharura
 
sina usHahidi juu ya hoja yako ila naweza kusema chanzo cha ajali kwa sasa ni kama ifuatavyo:-

1. Kuna madereva wengi hasa wa gari ndogo wamepewa Lesseni bila ya kwenda Driving school. Hivyo chanzo cha kwanza ni Rushwa
2. Barabara zetu ni za mfumo wa kizamani wa barabara moja. Hivi sasa Magari yameongezeka Barabara ni zilezile za kizamani. inatakiwa serikali ya CCM waweke angalau barabara 2 na si moja kama hivi sasa.

3. Barabara ya morogoro Road au Kilwa Road inaitwa High way lakini kuna muingiliano na shughuli zingine kama watembeaji wa miguu, pikipiki, baiskeli, wanyama kukatiza barabara n.k

4. Kuna magali mengi ya Left hand mfano yale ya kimarekani International ambayo dereva pekee anaendesha bila kuwa na msaidizi upande wa kulia. dereva anajiamini kwa vile gari lake ni chuma tupu anaovertake mahali popote

5. Malori mabovu mengi yapo barabarani

6. Madereva wengi hawajui matumizi ya handbreak wakati wa dhararu itumike vipi?, break ya aina gani kukanyaga na ni mahali gani, overtake afanyaje?, tahadhari gani ya kuchukua kwenye mlima, kona, matumizi ya taa n.k

7. Kuna magari mengine Wide abnormal vehicle yanapita kwenye vibarabara vyetu vyembamba ni hatari wakati wa kupishana.
8. Magari mengi ni used hasa Malori yanakufa mahali popote. tumeshuhudia mengi yanashindwa kupanda mlima na yanarudi nyuma, yanaharibika milimani. UKIENDA ZAMBIA UTASHANGAA MALORI YA TANZANIA YAMEKUFA BARABARANI WAKATI YA ZAMBIA HAYAFI KWANI WAO UAGIZA MALORI MAPYA.

9. mfano Scania 113 break zake ni MAJANGA NI HATARI LINAPOSHUKA MLIMA KAMA UPO JIRANI NALO TAFADHALI LIACHE MBALI. NA HAYO YAMEJAA SANA HAPA BONGO. ANGALIA MALORI YA MIZIGO YA RWANDA, ZAMBIA, DRC YANAYOINGIA NCHINI SIO SCANIA 113 AU DAF NI MERCEDES BENZ ACTORS NI IMARA KWA SAFARI NDEFU NA KWENYE MILIMA
 
Rushwa, rushwa , rushwa kwa polisi wa usalama balabalani,
 
Utotole

Umeongea kitu cha maana sana na kila siku hili me nalisema but kwa utawala uliopo sidhani kama wanaweza kufanya haya but me naona inawezekana kabisa chukulia mfano maandalizi ya katiba mpya tangu mwanzo gharama zote zile zoezi lisingefanyika nguvu ikaelekezwa kwenye upanuzi wa Barabara fedha ile ingetosha kujenga Barabara kutoka Dar mpaka Mbeya kigezo cha kutokuwa na fedha hata me sikikubali.
 
Last edited by a moderator:
Nawakilisha ni mawazo yangu
Me kama mwananchi wa kawaida kabisa napenda nitoe mapendekezo nini cha kufanya dhidi ya hizi ajali barabarani zinazozidi kuua mamia na kuwatia uvilema maelfu ya watanzania

1.Serikali inapaswa kusitisha utoaji wa leseni hasa vyombo vya moto vinavyobeba abilia na malori makubwa

2.Kupitia na kuhakiki madereva wote wa malori na mabusi

3.Kuamuru madereva wote warudi kusoma na kupata vyeti na hati mpya za defensive driving

4.Kufuta license za mabasi yote hasa yenye namba kuanzia A pamoja na B kubeba abiria na hata malori ya mizigo pia

5.Serikali kupitia Tanroad kuziba mashino yote yakiyopo hasa hizi main road kuepusha ajari zisizo za lazima

6.Serikali kupitia Jeshi la Polisi kuanza kuwateua hasa trained trafic polisi kusimamia na kutekeleza usalama bara barabi wengine ni hovyo kabisa hawafai (Siku hizi tochi nyingi ajali kibaoooo)

7.Kuandaa sheria mahususi hasa kwa wale wanaoleta ajari kwa makusudi

8.Kiandaliwe chombo maalamu/Taasisi itakayohusika na kusimamia utekelezaji wa hizo sheria

9.Ukarabati wa Reli za kati hasa za mizigo ili kuwe na maandalizi ya kuyapiga marufuku malori yote nchini yawepo lkn kwa vibali maalum sio kama njugu tu

Wenu mwana JF

Mawazo yako ni mazuri sana na tungependa siku moja hii hali ikome kabisa,mm ni dereva wa Lory la masafa marefu nje ya Tz,na kilichopo kwa madereva ni msongo wa mawazo,ujira na posho ndogo visivyokidhi mahitaji ndivyo sababisho kuu la kuendesha akiwa na mawazo lukuki,Serikali imepuuzia kuifanya taaluma hii kua rasmi na kusimamiwa kwa maslahi ya madereva,hivyo dereva anataka awahi ili apige trip nyingine harakaharaka,na hii ni kutokana na kipato kidogo.Pili Tanroads hawapo makini kukagua barabara,wao wanafanya kazi kwa kuvizia tu,Trafic nao ni JANGA kuu.
 
haitasaidia kitu njia rahisi ni kudhibiti mwendo wa mabasi kwa kuyapangia muda maalum wa kufika katika vituo husika

Ndugu,mabasi yamepangiwa muda tangu muda mrefu tu,na wanacheck point kwa ninazozifamu ni Mikumi,Iringa Kabla ya Ndiuka na Makambako,
 
Na ukitizama mabasi ya Tz yanasafiri umbali mfupi tu lkn ajali hazikomi,Zambia mabasi yanasafiri usiku na safari ni ndefu sana kulingana na jiografia yake,lakini tangu 2009 nimeanza kupita zambia hasa barabara ndefu ya kutoka Nakonde-Lusaka au Kasumbalesa,mabasi yaliyopata ajali hata matano hayafiki na si za kuua km ilivyo kwetu
 
Miundo mbinu mibovu
Magar hayana viwango
Msongo wa mawazo uchovu hii Leo mtu anatoka Dar Port lile folen la masaa mawili mpka afike Mbezi shydaa Kibaha check point
Traffic kila mahali ka kunguru weupe
Ajali zitaisha labda waanze na Pale Ruvu kibarabarw kama hakiendi mji Mkuu Drivers wanaendesha kwa kukariri tu
Mizani keroooooooooooooooo
Route zety fupi tu lakini majanga kuna Route ya lilongwe to maputo lakin huwezi kuta majanga au gar break down ila sie tumejaza break dowb kibao et hata hapa hapa Dar HII LEO FIAT LINASAFIRISHA MAKONTENA
fyuuuuuuuu ImageUploadedByJamiiForums1428991863.721612.jpg
 
cement

Kwanza mimi ningeshauri serikali iwekeze kwenye ujenzi wa barabara. Tunashuhudia ajali nyingi zinazotokea kwenye barabara kuu (highways) huhusisha magari yanayogongana uso kwa uso, aidha wakati wa ku-'overtake' au kukwepa mashimo na wakati mwingine kupoteza tu mwelekeo kwa gari mojawapo na hivyo kuligonga linalokuja mbele yake moja kwa moja.

Pamoja na kushughulika na viwango vya weledi na tabia/nidhamu ya madereva pamoja na ubora wa magari, naamini ni wakati sasa hizi highways zetu zitengenezwe kwa kiwango cha highway. Hapa namaanisha kwamba serikali iwekeze kwenye kujenga barabara madhubuti katika namna ambayo magari itakuwa nadra sana kugongana uso kwa uso. Serikali ijenge barabara mbili zinazojitegemea across all highway routes, mfano wa 'double roads' ili gari inayotoka Dar kwenda Iringa ipite njia yake na ile inayotoka Iringa kwenda Dar ipite njia yake na barabara hizi ikibidi zitenganishwe na kiunga au kingo na nafasi ya kutosha. Ikiwa hivi nina hakika 'it will take the devil himself' on the wheel of one of the cars to achieve a head-on smash between two cars moving in opposite direction.

Na kwa kuwa kila njia itakuwa na uwezo wa kupitisha magari japo mawili kwa wakati mmoja (each direction), hata magari yale yanayoenda uelekeo mmoja hayatakuwa katika hatari ya kukwaruzana kwa kuwa dereva wa nyuma akitaka kumpita wa mbele yake atatumia 'lane' mojawapo kutegemea yule wa mbele yuko lane gani. Hapa hata kukwaruzana haitakuwa kitu cha kila siku.

Hapa zitabaki ajali zinazosababishwa na mechanical failure, dereva kusinzia au kuwa mzembe, unexpected objects on the road, na mengine ambayo as we know of recent...ajali nyingi zilizogharimu maisha ya wengi zimetokana na magari kugongana uso kwa uso. Hali ya barabara zetu ambapo kwa sehemu kubwa barabara ina lanes mbili tu kwa directions zote hufanya magari yapishane kwa karibu sana, jambo linaloongeza uwezekano wa ajali za uso kwa uso.

Sitakubaliana na utetezi kuwa ni gharama sana kujenga barabara za namna hiyo, kwa maana ya ku'double' barabara zilizopo kwa kuwa maisha ya watu yanayopotea kila siku yana thamani kubwa kuliko hizo pesa ambazo nyingi hata hivyo zinaishia kwenye matumbo ya walafi wachache. Vile vile huo ni mpango wa muda mrefu, tofauti na miradi tuliyozoea ya kupigia kampeni, ambayo tunataka ndani ya miaka mitano ikamilike japo kwa kiwango cha hovyo ili chama na wagombea wetu waombee tena kura. Kama tuna maono na dira ya muda mrefu kukomesha ajali hizi, inatakiwa serikali iwekeze kwenye ujenzi wa barabara ya namna hiyo phase by phase.

Likifanyika hilo na masuala yanayohusiana na ubora wa madereva na magari yakafanyiwa kazi, ninayo imani kabisa kuwa ajali zitapungua kwa kiasi kikubwa sana. Lakini kama tukiendelea na barabara yetu moja tunayoiita highway, tutaimba na kuimbiwa parapanda kila siku.

Miundo mbinu mibovu
Magar hayana viwango
Msongo wa mawazo uchovu hii Leo mtu anatoka Dar Port lile folen la masaa mawili mpka afike Mbezi shydaa Kibaha check point
Traffic kila mahali ka kunguru weupe
Ajali zitaisha labda waanze na Pale Ruvu kibarabarw kama hakiendi mji Mkuu Drivers wanaendesha kwa kukariri tu
Mizani keroooooooooooooooo
Route zety fupi tu lakini majanga kuna Route ya lilongwe to maputo lakin huwezi kuta majanga au gar break down ila sie tumejaza break dowb kibao et hata hapa hapa Dar HII LEO FIAT LINASAFIRISHA MAKONTENA
fyuuuuuuuuView attachment 243152
 
Suala la kuimarisha usafiri wa reli ni la muhimu sana. Naumia kuona mizigo mizito ikiwa kwenye makontena yanayosafirishwa kwa barabara. Tanzania tuna system nzuri ya reli yenye urefu mkubwa kuliko nchi yeyote ya EAC. Karibia miji na majiji yote makubwa kama arusha, mwanza, mbeya na tanga yanafikika kwa reli. Kikubwa ni kufanya ukarabati na kuhakikisha mizigo yote inasafirishwa kwa treni na baada ya muda Tutaweza kuboresha usafiri huu kwa abiria pia. Njia hii itapunguza watumiaji wa barabara hatua itakayopelekea kupungua kwa vifo. Sitaki kuamini kama suala hili linashindikana kwa serikali inayojinadi kuboresha maisha ya watanzania labda kama ile tuhuma ya vigogo kumiliki vyombo vya usafiri iwe ya kweli
 
cement

Kwa kuwa humiliki gari ungekuwa na moja ya basi au roli lenye kuanzia A usingethubutu kusema wazuie yasibebee abiria na mizigo. halafu yakishazuiliwa yakafanye kazi gani?

kutengenezea mageti

yamezaa mayatima na wajane wengi sana
 
Last edited by a moderator:
''Kutokana na ajali za barabarani ambazo watalawa kama vile wameshindwa kusimamia au kuchukua hatua za dharura kunusuru maisha ya watu ambayo yanapotea kila siku; Ningekuwa kiongozi ningesema haya yafuatayo:

''Sitaki kusikia ajali zinatokea, hivyo basi kamanda wa usalaama barabani wa eneo usika (eneo la ajali), mkuu wa wilaya wa eneo n.k , barua zao ziko tayari kufukuzwa kazi kama hayo yatatokea katika eneo lao ikiambatana na kutunga sheria ya kufungwa kwa miaka 3 jela kushindwa kuweka mikakati ya kuzuia ajali''

MATOKEO:Wakuu hao wataweka mitakati ya kudhibiti ajari, hutasikia ajari za hovyo ovyo.

2.Kama wauzaji wa madawa ya kuleya wamewekewa sheria kali,kwa nini madereva na wamiliki wa kampuni ya usafirishaji yasiwekewe sheria kali.

Mfano🙁a)ikithibitika ni uzembe wa dereva;Dereva akisababisha ajari atalipa fidia ya sh TZS 10 billion Na kifungo cha maisha jela
(b) Wamiliki wa mabasi hayo pia watalipa fidia ya TZS 10 billion na kufungiwa kufanya shughuli za usafirishaji kwa miaka isiopungua 5

3.Serikali kufuta vyuo vya mitaani ambavyo havina sifa za kufundisha udereva.

Je kama haya yakisimamiwa kutakuwa na ajari barabari

WADAU TUJADILI
 
Fanya utafiti wa kutosha kujua vyanzo vikuu vya ajali then mikakati ndio ubuniwe jinsi ya kupunguza ajali
 
Sijali matumizi yako mabovu ya R ila naomba kujua uhusiano ya wote uliowataja na ajali za barabarani!
Na nataka kujua kifungu cha sheria ulichorefer ili faini ya dereva aliyehusika kwenye ajali iwe bilioni 10 na ningependa kujua namna ya utekelezaji wa malipo husika ikiwa mtuhumiwa atakuwa amefariki kwenye ajali!
 
Back
Top Bottom