Ajali ya basi la Ester, Rav4 yaua watatu Kilimanjaro

Inasikitisha mno tena mno .
Kuna nchi ili upate leseni ya udereva ni hadi uwe umehakikiwa kweli kweli sana hatari haikuwa kwake yeye dereva mzembe bali anaweza kusababishia wengine kufa au ulemavu wa kudumu ambao wako innocent.
Na ndio ukweli we unaweza kufata sheria akaja mwingine akakuletea shida
Nadhani tz ni Moja kati ya nchi watu hawafati sheria duniani na sio TU barabarani Bali kwenye mambo mengi zikiwemo ofisi
 
Dah! Pole Kwa familia zilizopoteza wapendwa wao..

RIP
 
Pole wafiwa
Ila tusidanganye watu hakuna luxury buses Tanzania
 
Hizi basi za kampuni ya Ester zikiwa barabarani wanajiona kama wao wanamiliki hii nchi. Hawajali watumiani wengine wa barabara na ndiyo chanzo cha wao kupata ajali mara kwa mara.

Hizi basi inabidi kuchukua tahadhari sana unapokutana nazo njiani. Hawachelewi kukuletea ajali makusudi tu.

Wapate pumziko la amani marehemu wote wa hii ajali
 

Zinakimbia balaa huko barabarani.
Mwendokasi kama wote.
Ukizikuta usiku zinavyo overtake hovyo Yaani ni hatari balaaa.
 
Kwa kumjua Mmiliki wa Basi la Ester, alivyo Kitabia na anapenda nini huku mwaka huu ukiwa ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu hapa najua sana Kafara limekubali na mwaka huu atashinda tena Ubunge huko Jimboni Kwake na kuendelea kutamba hadi katika Noti mpya za duniani.
 
Tatizo lipo pande mbili, kutofuata sheria lakini pia miundo mbinu sio rafiki. Baada ya kukamilika miradi iliyopo sasa ya SGR, BWAWA, MADARAJA, nk. Ingependeza sasa Mradi mkubwa uwe wa kuweka Barabara Nne za Njia kuu zote nchini. Itasaidia kupunguza ajali kwa asilimia kubwa sana.
 
Ajali nyingi bongo ni kukosa umakini Kwa madereva, barabara zenyewe za ku overtake hovyo ziko wapi Sasa?. Njia ikitanda semi moja la maana tu ishakuwa kama kiuchochoro Fulani hivi, tuwe makini sana barabarani na kama una gari ndogo omba sana usifanye uzembe highway ukakutana na semi ya mizigo ama basi Iko full masinondo utakunya Hadi mavi ya mwisho.
 
Ila kuna madereva wengine nao ujinga umewajaa hasa wa malori na mabasi.

Anaona kabisa usha-overtake upo upande wake na umbali aliopo hakuna shida,ajabu naye ananyoosha goti kwa vile tu wewe una gari dogo!

NB:Ajali za wakati wa ku-overtake huwa ni kifo maana mwendo lazima uwe wenyewe!
 
Huko shule hauwezi funzwa vingine tofauti na serikali inavyotaka.
Si umeona huyo wa rav4,alikua anamfuata Kidia bila kuchukua tahadhari yake binafsi,shuleni tumefundishwa somo la tuwe na udereva wa kujihami,akauziwa kicheche,hakufuata sheria za driving,kwamba uovertake tu pale unapojihakikishia usalama wako kwanza.

Shule haijawahi kudanganya,ni kama kioo vile
 
Hapo ilipotokea ajali huwa kuna Misongamano ambayo hupelekea hizo overtake , tungekua na barabara pana inayoweza kukidhi uwingi wa vyombo , ingekupunguza ajali kwa kiasi kikubwa .
 
Soma vizuri na sikiliza kwa makini maelezo ya mashuhuda, chuki zako usituhusishe sisi. Hiyo Rav4 iligongwa nyuma kwenye tairi ya akiba na basi la Kidia One hivyo ikasukumwa na kwenda kujigonga kwenye basi la Ester.
 
Ajali hii imeua mwalimu mstaafu ,mwanamke mwalimu Ayo, alikuwa ametoka kupata mafao yake yaliyopelekea pia kununua gari mpya.
Kwenye gari alikuwa na mwanaye wa kiume ( dereva) , akiwepo pia rafiki wa mtoto wa mwalimu ambaye ni dereva.
Gari ni mpya kabisa na imesajiriwa jana.
 
Qafr za mbio 2030
 
"Fatigue" huwa inaathiri sana maamuzi ya dereva unknowingly.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…