Ajali ya basi la Ester, Rav4 yaua watatu Kilimanjaro

Ajali ya basi la Ester, Rav4 yaua watatu Kilimanjaro

Tatizo lipo pande mbili, kutofuata sheria lakini pia miundo mbinu sio rafiki. Baada ya kukamilika miradi iliyopo sasa ya SGR, BWAWA, MADARAJA, nk. Ingependeza sasa Mradi mkubwa uwe wa kuweka Barabara Nne za Njia kuu zote nchini. Itasaidia kupunguza ajali kwa asilimia kubwa sana.
Kwa uongozi upi😳
 
Ajali hii imeua mwalimu mstaafu ,mwanamke mwalimu Ayo, alikuwa ametoka kupata mafao yake yaliyopelekea pia kununua gari mpya.
Kwenye gari alikuwa na mwanaye wa kiume ( dereva) , akiwepo pia rafiki wa mtoto wa mwalimu ambaye ni dereva.
Gari ni mpya kabisa na imesajiriwa jana.View attachment 3221517
Halafu bima mbona kama ndogo maskin
Wataambulia mabati tu
 
Kila kifo hakikosi sababu lakini barabara ya njiapanda ya himo Hadi Moshi mjini Ina msongamano Sana WA magari pia ni nyembamba mnoo. Kifupi ku overtake ni ku bet maisha yako.
Moshi na arusha ni mikoa ya kitalii kwanini serikali. Haipanui ile barabara? Hata pale sha tours ajali ni kila siku za magari na watu. Tena ajali za shoo kwa shoo.
Madereva nao inabidi wayaelewe hayo maeneo wajue nini cha kufanya.

Ile barabara inaunganisha mikoa ya Kilimanjaro, arusha, manyara, dodoma hadi kanda ya ziwa. Pia inapitisha magari yanayotoka nje ya nchi pia ikiwemo kenya, Uganda na kwingine... Kwanini haipanuliwi imekaa tu kama barabara ya mtaa?

Kwa wembamba wa barabara ile kuna siku naingia town kwa boda asee side mirror ya boda ilipigwa mzinga na gari ndogo ni Mungu tu hatukuyumba tukapelekwa katikati. Nilimlipa boda nauli ya kwenda na kurudi Ila nilimwambia aniache tu ntarudi mwenyewe na nauli nkasemehe.
 
Elimu,watu wengi wamejua kuendesha gari au chombo chochote bila kupata elimu ya u driver hii inawafanya waone Kila kitu sawa TU
Lakini kingine ni ujinga nyuma ya usukani hii inaumiza wengi
Pombe kidogo madhara makubwa.
 
80% ya ajali zote ni wrong driving[makosa ya binadam],15% ni ajali zinazosababishwa na hali ya hewa mbaya eg mvua,ukungu barabarani,n.k, na 5% ndio zinasababishwa na miundo mbinu,hiyo ni kwa mujivu ya shule fupi ya driving niliyopitia
Huu ndio ukweli. Madereva wengi wazembe na wapumbavu ndio chanzo kikuu cha ajali Tz. Hii kusema miundombinu ni kichaka cha kuficha uzembe na uoumbavu wa maderev wengi.
 
Na ndio ukweli we unaweza kufata sheria akaja mwingine akakuletea shida
Nadhani tz ni Moja kati ya nchi watu hawafati sheria duniani na sio TU barabarani Bali kwenye mambo mengi zikiwemo ofisi
Madereva hawajali kabisa sheria za barabarani. Majitu yanapita taa nyekundu,yanaendesha wrong way,yanaegesha gari pipote bila kujali wengine yaani kama mbuzi wanaendesha magari.
 
Si umeona huyo wa rav4,alikua anamfuata Kidia bila kuchukua tahadhari yake binafsi,shuleni tumefundishwa somo la tuwe na udereva wa kujihami,akauziwa kicheche,hakufuata sheria za driving,kwamba uovertake tu pale unapojihakikishia usalama wako kwanza.

Shule haijawahi kudanganya,ni kama kioo vile
Ukiendesha njia kuu utaona hawa wapumbavu wengi sana. Mmoja akiovateki nao wanafuata nyuma kama nyumbu kumbe mwenzao kakadiria gap lake dogo matokeo yake ndio haya.
 
Hizi ajali zinasikitisha sana harafu hapo kujua nani alikua na makosa ni mpaka watafutwe watalaamu wa kupima ajali sio hawa wanakuja na majibu ya uzembe wa madereva sijui mwendo kasi bila kutoa sababu za kitaalamu..inasikitisha sana kwa kweli
 
Madereva hawajali kabisa sheria za barabarani. Majitu yanapita taa nyekundu,yanaendesha wrong way,yanaegesha gari pipote bila kujali wengine yaani kama mbuzi wanaendesha magari.
Kwenye barabara za tz hususani dar labda mataa pekee ndio watu wanaogopa traffic ila kwingine dah!!
Madhara yake ndio hayo tunayoyaona vifo visivyotarajiwa kabisa
 
Huyo dogo aliyefariki amemaliza chuo mwaka jana Degree ya Account na mdogo wangu wa kike hapo TIA..Alikua anaishi kwa Azizi Ali na jana aliwaaga marafiki zake anaenda Nyumbani kusalimia wazee na gari private.Saa 9 na nusu usiku alipost status akiwa anapata chakula (Chips kuku na juice) akaandika short break.Alfajiri saa 12 na nusu kapata ajali.Aisee inasikitisha sana kijana mdogo miaka 25 tu 🄲 mwendo ameumaliza.
 
Kila kifo hakikosi sababu lakini barabara ya njiapanda ya himo Hadi Moshi mjini Ina msongamano Sana WA magari pia ni nyembamba mnoo. Kifupi ku overtake ni ku bet maisha yako.
Moshi na arusha ni mikoa ya kitalii kwanini serikali. Haipanui ile barabara? Hata pale sha tours ajali ni kila siku za magari na watu. Tena ajali za shoo kwa shoo.
Madereva nao inabidi wayaelewe hayo maeneo wajue nini cha kufanya.

Ile barabara inaunganisha mikoa ya Kilimanjaro, arusha, manyara, dodoma hadi kanda ya ziwa. Pia inapitisha magari yanayotoka nje ya nchi pia ikiwemo kenya, Uganda na kwingine... Kwanini haipanuliwi imekaa tu kama barabara ya mtaa?

Kwa wembamba wa barabara ile kuna siku naingia town kwa boda asee side mirror ya boda ilipigwa mzinga na gari ndogo ni Mungu tu hatukuyumba tukapelekwa katikati. Nilimlipa boda nauli ya kwenda na kurudi Ila nilimwambia aniache tu ntarudi mwenyewe na nauli nkasemehe.
Hili jambo huko juu nimelizungumzia wana wakapinga
 
Mama mwalimu kapokea pension kamchukuwa kijana wake twende dar tukachukuwe gari
Kufika wakamlipa dereva awapeleke Arusha na chuma mpya, familia imempoteza kijana na mama yake mzazi na dereva waliyemkodi. Inasikitisha sana
 
Sijakuelewa! Waliokufa mmoja ana miaka 61, eliud ana miaka 65, dereva ana miaka 25.
Kijana ni yupi !!
 
Ukiendesha njia kuu utaona hawa wapumbavu wengi sana. Mmoja akiovateki nao wanafuata nyuma kama nyumbu kumbe mwenzao kakadiria gap lake dogo matokeo yake ndio haya.
Hakika mkuu,binadam tunaoenda sana kulazimisha halafu baadae tunamsingizia Mungu
 
Huu ndio ukweli. Madereva wengi wazembe na wapumbavu ndio chanzo kikuu cha ajali Tz. Hii kusema miundombinu ni kichaka cha kuficha uzembe na uoumbavu wa maderev wengi.
Hakika mkuu
 
Back
Top Bottom