Hapa Watanzania ndipo tuliporogwa, sijui tutakuja kupona lini. Tutakimbilia kutibiwa nje mpaka lini?
Jamani tuimarishe hospitali zetu za taifa, za mkoa na wilaya, hizi pesa tunazotupa kupeleka watu SA, India na Europe, zinaweza kuokoa maelfu ya watu kama tutazitumia vizuri hapo TZ.
Technology ya tiba sasa imekuwa wazi, bora pesa zako, tutatajirisha watu nje mpaka lini?
Hilo la kumtoa dereva nje bila uchunguzi wa ziada nafikiri pia ni matatizo ya sisi Watanzania au Waafrika ya kutokuthamini wasaidizi wetu. Tuna wa treat vibaya wasaidizi wa ndani huku tunawaachia kulea wanetu. Hatuwapi haki zote madereva huku uhai wetu uko mikononi mwao. Huyo dereva naye inatakiwa awe mfanyakazi wa bunge na ungekuwa wajibu wa bunge kuangalia maslahi yake. Lakini kama ilivyo TZ, kigogo anapelekwa sehemu ya maana kutibiwa, vijana maskini wenzetu wanaacha wanazubaa zubaa, nani atawatetea?
Nimeshaona mara nyingi tu TZ, kigogo anajichana huku dereva anahangaika na njaa kwenye gari, kisha wanaondoka safari ya mwendo. Looh! kutembea na dereva mwenye mjaa mbona ni kujitakia balaa? Kuna mambo mengi sana hayako sawa huko nyumbani!
.....ametelekezwa na Mwakyembe!!!!???Right, huyo Mallya ni kwamba Mbunge alienda akachukua mtu amuendeshe wakati hana leseni. Irresponsible. Huyu dereva wa aliyetelekezwa na Mwakyembe na atoe full testimony kama alikuwa under duress ya bosi.
Itabidi tumfanyie "investigation" na kuangalia uwezekano wa possible lawsuit
Madereva wote wa wabunge wawe katika ajira ya serikali
kati ya vitu vinavyoshangaza sana ni kuwa hadi hivi sasa wabunge wanapewa fedha za kuwalipa madereva wao lakini madereva hawa hawajaajiriwa na serikali. Jambo hili kwa kweli ni upungufu mkubwa sana wa maono. Ukifikiria gharama ya uchaguzi mdogo mmoja tu kama ule wa Tarime na gharama ya kuajiri madereva kwa wabunge wote utaona kuwa ni rahisi zaidi kuajiri madereva kwa miaka mitano kuliko kurudia chaguzi angalau moja kila mwaka kufuatia kifo au ajali inayomfanya mtu ashindwe kuendelea na ubunge wake.
Kwa ajili ya mjadala wetu hapa tufikirie kuwa uchaguzi mdogo unagharimu karibu shilingi 2,000,000,000 (hii ni gharama tu ya maandalizi, kampeni na uchaguzi wenyewe), ukizichukua hizo na kugawa kwa wabunge 325 kila mbunge anapata shilingi milioni 6,153,846 kama kila mbunge anamuajiri dereva mmoja kwa mwezi anaweza kumlipa ni laki 512, 820 kiasi ambacho ni kikubwa ukilinganisha na kima cha chini.
Sasa kama tunaweza kuwa na kiasi hicho kwa nini tusiingize fedha hizo kwenye bajeti y a kawaida ya Bunge ambapo madereva wa wabunge watakuwa chini yake na hivyo kuwa waajiriwa wa Bunge? Kwa kufanya hivyo tutaongeza ajira, tutakuwa na utaratibu mzuri na madereva hawa watakuwa wanafanya kazi katika maadili yanayosimamiwa vizuri kuliko jinsi ilivyo sasa. Zaidi ya yote kutakuwa na rekodi nzuri ya madereva na kwa kadiri muda unavyoenda tutakuwa na madereva wazoefu katika shughuli za wabunge kuliko ilivyo sasa. Uchaguzi mpya unapokuja, na wabunge wapya wanapoingia hakutakuwa na haja ya mbunge kuanza kutafuta madereva kwani tayari wapo.
Hii itakuwa ni sawasawa na ilivyo kwenye taasisi au mashirika mengine ya serikali ambapo kuna madereva ambao hawajali ni nani bosi wao bali wako tayari wakati wote kufanya kazi yao chini ya yeyote atakayekuwa bosi wao kwani wao si waajiriwa wa mtu bali wa taasisi. Unapokuwa na madereva rasmi na wenye mkataba wa serikali utaona kuwa linapotokea janga au jambo ambalo likawasababishia ulemavu au au hata kifo basi madereva hao na familia zao watakuwa kwenye utaratibu wa kupata matibabu au mafao ya aina fulani kuliko ilivyo sasa ambapo dereva wa mbunge akifia kazini sijui zaidi ya rambirambi ana haki gani nyingine.
Hili hata hivyo ni jambo ambalo ni wabunge wenyewe wanaweza kuamua kulitungia sheria badala ya kusubiri kuipigia magoti serikali. Mambo yote niliyoyapendekeza hapa na mengine ambayo yapo mbeleni utaona kuwa yanawezekana kufanywa na kuletwa Bungeni na wabunge wenyewe. Jambo moja ambalo hatuna budi kulikataa ni kuambiwa kuwa serikali haina fedha. Mbunge atakayekubali kusikia kuwa ati serikali haina fedha kwa wakati huu kuhusu mabadiliko haya mbunge huyo itabidi tumtimue Bungeni. Tuna kiasi cha kutosha cha fedha na wakati umefika kuanza kuweka vipaumbele vyetu sawasawa.
.......kama ile ya Dr. Masau eehhh!!....hivi ile investigation yake iliishia wapi?
Dalali ataka barabara ya Dodoma ichunguzwe
Mwenyekiti wa Simba Hassan Dalali ameiomba Wizara ya Miundombinu kuifanyia ukaguzi barabara kuu ya Dodoma - Morogoro inayopitia katika Kijiji cha Chamale, Kata ya Magubike, wilayani Kilosa, kwa ajili ya kuweza kubaini vyanzo halisi vya ajali za mara kwa mara.
Dalali alitoa ushauri huo alipowatembelea majeruhi ambao ni mashabiki wa timu yake waliopata ajali usiku wa Aprili 26 katika kijiji hicho walipokuwa wakitoka kuishuhudia Simba ilipocheza na Polisi Dodoma.
"Ipo haja kwa serikali kuingilia kati ili kujua kwa nini eneo hilo linatokea ajali za mara kwa mara ili kunusuru maisha ya watu …huenda eneo hilo lina matatizo au vijana ndiyo wanaomwaga mafuta ya dizeli, " alisema Dalali.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa Simba, iwapo serikali kupitia wizara inayohusika kulikagua eneo hilo la barabara huenda ikatoa majibu sahihi ya kubaini iwapo lami iliyotumika ina kasoro ama kuna tatizo lingine litakalopaswa kuchukuliwa hatua za haraka.
Mashabiki kadhaa wa timu hiyo walinusurika kifo baada ya basi dogo walilokuwa wakisafiria kutoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam, kuacha njia na kupinduka eneo la Chamale, Kijiji cha Magubike, wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Ajali hiyo ilitokea saa 5: 45 usiku katika eneo hilo baada ya siku mbili kupita wakati ilipotokea ajali mbaya ya basi mali ya Kampuni ya RS Investiment iliyosababisha kifo cha Mbunge wa zamani wa Jimbo la Biharamulo Magharibi (TLP), marehemu Phares Kabuye na watu wengine wawili na kujeruhi abiria 54.
Mchana wa siku hiyo, viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro akiwamo Mwenyekiti na Katibu wake walipata ajali katika eneo hilo na usiku wake ndipo mashabiki hao wa Simba walipatwa na mkasa huo. Mashabiki 12 walijeruhiwa katika ajali hiyo na kukimbizwa Hospitali ya Misheni ya Berega iliyopo wilayani humo.
LATEST: Mpiganaji Dk Harrison Mwakyembe atapelekwa Dar kwa charter plane mchana huu kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kidaktari. Kwa sasa anaendelea vizuri Wadi No 5 katika hospitali ya mkoa Iringa. Dereva wake ni mzima kabisa, na yuko chini ya ulinzi wa polisi kwa sasa, hapo hapo hospitali. Anahojiwa kutokana na kudanganya hapo awali kuwa gari yake iligongwa kwa nyuma. Mtu aliyeenda eneo la ajali na baadaye hospitali anasema gari ya Dr Mwakyembe aina ya Landcruiser ilikuwa ina-overtake malori mawili na ghafla dereva alishtukia shimo kubwa mbele yake akapoteza control na gari ikapinduka ikiwa pia imegonga mti mkubwa na kuuong'oa.
Ninaimani hakuna hila za kina Malya na Chaha Wangwe, lakini ni vyema pia kuwa waangalifu na watumishi wetu hata wa majumbani kwani kwenye mapambano kama haya mtu yeyote anaweza kutumiwa.
Sijui wanasiasa wetu wanajifunza nini kutokana na jinsi umma ulivyoguswa na ajali ya ndugu yetu.Ni vyema tukasoma nyakati kuwa kuktenda mema umma unakujali na kukufariji.Maana ninaimani kama ingekuwa ajali za baadhi ya jamaa zetu fulani nadhani watu wangekuwa wanasindikiza na arubadili ili watu hao waondoke katika jamii yetu.
Aljuniour,Mbona ni kama kuna harufu ya ka-ufisadi ktk hii ajali??? 😕 Polisi wanasema ajali imesababishwa na gari ya mh.mbunge lilipo-overtake lori na kuingia ktk shimo (angalia picha chini). Lakini dereva wakati anahojiwa na Abdallah Majura wa BBC alisema; LORI LILIKUWA LINAWAFUATA NYUMA YAO KWA KASI SN, WAKATI AKAWA ANAJARIBU KULIKWEPA BADO LINAWAFUATA THEN LIKAWA GONGA KWA NYUMA NDIO LIKAPINDUKA.
Ile speech ya polisi pia ina mashaka kdg; hivi hili shimo ndio lisababishe tairi ichomoke na kupinduka after over take?
Hapa Watanzania ndipo tuliporogwa, sijui tutakuja kupona lini. Tutakimbilia kutibiwa nje mpaka lini?
Jamani tuimarishe hospitali zetu za taifa, za mkoa na wilaya, hizi pesa tunazotupa kupeleka watu SA, India na Europe, zinaweza kuokoa maelfu ya watu kama tutazitumia vizuri hapo TZ.
Technology ya tiba sasa imekuwa wazi, bora pesa zako, tutatajirisha watu nje mpaka lini?
Hilo la kumtoa dereva nje bila uchunguzi wa ziada nafikiri pia ni matatizo ya sisi Watanzania au Waafrika ya kutokuthamini wasaidizi wetu. Tuna wa treat vibaya wasaidizi wa ndani huku tunawaachia kulea wanetu. Hatuwapi haki zote madereva huku uhai wetu uko mikononi mwao. Huyo dereva naye inatakiwa awe mfanyakazi wa bunge na ungekuwa wajibu wa bunge kuangalia maslahi yake. Lakini kama ilivyo TZ, kigogo anapelekwa sehemu ya maana kutibiwa, vijana maskini wenzetu wanaacha wanazubaa zubaa, nani atawatetea?
Nimeshaona mara nyingi tu TZ, kigogo anajichana huku dereva anahangaika na njaa kwenye gari, kisha wanaondoka safari ya mwendo. Looh! kutembea na dereva mwenye mjaa mbona ni kujitakia balaa? Kuna mambo mengi sana hayako sawa huko nyumbani!
Kela72,Mkuu kwenda kutubiwa nje sio sisi tu, tuwe na kumbukumbu jamani tusinogewe na nyimbo hizi haya mambo hata watu tunaofikiri wametuzidi uwezo hofanya hivyohivyo... Mfalme Hussein Wa Jordan, Omar Bongo umesikia yuko wapi? na wengineo wengi tu..labda useme ni tabia ya kinyonge na haifai lakini sio sisi tu tnaoendekeza haya.
La Dereva kutolewa nje bila kufanyiwa uchunguzi ni ktu cha ajabu sana naungana nawewe lakini bora hata huyo ni Dereva, wakubwa wana ubinafsi wa ajabu kabisa kabisa nakumbuka mheshimiwa mmoja alipata ajali nikiwa Morogoro akiwa na mwanae wa kumzaa cha ajabu yule mtoto hakuangaliwa kabisa wala hakupewa hata panadol!
Mtanzania,
Hapo hamna tofauti kabisa na mitaani (streets) na inatakiwa iwe kwenye 50km/hr. Inabidi TANROADS waanze kupanua haya maeno pembeni mwa barabara ili walau kuwe na urefu wa mita 15-20 kama kweli wanaziita highway.
.