Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Samahani wakuu zangu kuingia kati hapa..
Nimesoma baadhi ya hoja huko nyuma zinasema Mwakyembe alipoteza fahamu baada ya ajali, sasa mlitaka afanye kitu gani ktk hali hiyo..Na kwa nini isiwe kazi ya wale waliokuja kuokoa kuhakikisha watu wote wanapewa huduma sawa ila kosa liwe la Mwakyembe aliyelazwa..
Hizi sinema za kizungu jamani mbona zinatumaliza!
 
Hapa Watanzania ndipo tuliporogwa, sijui tutakuja kupona lini. Tutakimbilia kutibiwa nje mpaka lini?

Jamani tuimarishe hospitali zetu za taifa, za mkoa na wilaya, hizi pesa tunazotupa kupeleka watu SA, India na Europe, zinaweza kuokoa maelfu ya watu kama tutazitumia vizuri hapo TZ.

Technology ya tiba sasa imekuwa wazi, bora pesa zako, tutatajirisha watu nje mpaka lini?

Hilo la kumtoa dereva nje bila uchunguzi wa ziada nafikiri pia ni matatizo ya sisi Watanzania au Waafrika ya kutokuthamini wasaidizi wetu. Tuna wa treat vibaya wasaidizi wa ndani huku tunawaachia kulea wanetu. Hatuwapi haki zote madereva huku uhai wetu uko mikononi mwao. Huyo dereva naye inatakiwa awe mfanyakazi wa bunge na ungekuwa wajibu wa bunge kuangalia maslahi yake. Lakini kama ilivyo TZ, kigogo anapelekwa sehemu ya maana kutibiwa, vijana maskini wenzetu wanaacha wanazubaa zubaa, nani atawatetea?

Nimeshaona mara nyingi tu TZ, kigogo anajichana huku dereva anahangaika na njaa kwenye gari, kisha wanaondoka safari ya mwendo. Looh! kutembea na dereva mwenye mjaa mbona ni kujitakia balaa? Kuna mambo mengi sana hayako sawa huko nyumbani!

Hiki ndiyo kilio changu siku zote.Ni lazima tuukuze uwezo wetu wa ndani kama kweli nia na madhumuni yetu ni kupiga hatua katika maendeleo.Kwa nini viongozi wetu watibiwe nje ya nchi??Kiongozi mkubwa kama Rais anatibiwa nje ya nchi halafu kiongozi huyo huyo haoni aibu kuniambia mimi nirudi nikajenge nchi!!!Yeye anatumia mamilioni ya dola kutibiwa nje, kwa nini asitumie mamilioni hayo kujenga walau Muhimbili tu ili wao wenye nundu watibiwe hapo??Mimi situmii fedha ya nchi kuishi hapa bado naonekana si mzalendo kwa sababu sirudi kwetu kujenga nchi. Lakini viongozi kutibiwa nje ya nchi kwa fedha za umma unaonekana ni uzalendo wa hali ya juu." Uhangala wufula wa mbwa"Umasikini ni sawa na uchi wa mbwa unanuka.
 
Right, huyo Mallya ni kwamba Mbunge alienda akachukua mtu amuendeshe wakati hana leseni. Irresponsible. Huyu dereva wa aliyetelekezwa na Mwakyembe na atoe full testimony kama alikuwa under duress ya bosi.
.....ametelekezwa na Mwakyembe!!!!???
 
Tuzidi kumwombea Dr Mwakyembe kwa Mungu apone na arejeshewe afya yake. Wana JF na raia wote wa Tanzania wenye nia njema na nchi yetu tuwe tayari kusaidia kwa hali na mali endapo msaada utahitajika. Kwa sasa tuweke kando speculation na conspiracy theories.
 
...mnh, kwa maana hii hawa madereva wa waheshimiwa wajijue "heri punda afe mzigo wa bwana ufike!"
 
Katika makala yangu ya "Mapendekezo ya Ulinzi wa Bunge na Wabunge" iliyotoka Feb 25, 2009 kwenye TAnzania Daima nilisema hivi:



Madereva wote wa wabunge wawe katika ajira ya serikali
kati ya vitu vinavyoshangaza sana ni kuwa hadi hivi sasa wabunge wanapewa fedha za kuwalipa madereva wao lakini madereva hawa hawajaajiriwa na serikali. Jambo hili kwa kweli ni upungufu mkubwa sana wa maono. Ukifikiria gharama ya uchaguzi mdogo mmoja tu kama ule wa Tarime na gharama ya kuajiri madereva kwa wabunge wote utaona kuwa ni rahisi zaidi kuajiri madereva kwa miaka mitano kuliko kurudia chaguzi angalau moja kila mwaka kufuatia kifo au ajali inayomfanya mtu ashindwe kuendelea na ubunge wake.

Kwa ajili ya mjadala wetu hapa tufikirie kuwa uchaguzi mdogo unagharimu karibu shilingi 2,000,000,000 (hii ni gharama tu ya maandalizi, kampeni na uchaguzi wenyewe), ukizichukua hizo na kugawa kwa wabunge 325 kila mbunge anapata shilingi milioni 6,153,846 kama kila mbunge anamuajiri dereva mmoja kwa mwezi anaweza kumlipa ni laki 512, 820 kiasi ambacho ni kikubwa ukilinganisha na kima cha chini.

Sasa kama tunaweza kuwa na kiasi hicho kwa nini tusiingize fedha hizo kwenye bajeti y a kawaida ya Bunge ambapo madereva wa wabunge watakuwa chini yake na hivyo kuwa waajiriwa wa Bunge? Kwa kufanya hivyo tutaongeza ajira, tutakuwa na utaratibu mzuri na madereva hawa watakuwa wanafanya kazi katika maadili yanayosimamiwa vizuri kuliko jinsi ilivyo sasa. Zaidi ya yote kutakuwa na rekodi nzuri ya madereva na kwa kadiri muda unavyoenda tutakuwa na madereva wazoefu katika shughuli za wabunge kuliko ilivyo sasa. Uchaguzi mpya unapokuja, na wabunge wapya wanapoingia hakutakuwa na haja ya mbunge kuanza kutafuta madereva kwani tayari wapo.

Hii itakuwa ni sawasawa na ilivyo kwenye taasisi au mashirika mengine ya serikali ambapo kuna madereva ambao hawajali ni nani bosi wao bali wako tayari wakati wote kufanya kazi yao chini ya yeyote atakayekuwa bosi wao kwani wao si waajiriwa wa mtu bali wa taasisi. Unapokuwa na madereva rasmi na wenye mkataba wa serikali utaona kuwa linapotokea janga au jambo ambalo likawasababishia ulemavu au au hata kifo basi madereva hao na familia zao watakuwa kwenye utaratibu wa kupata matibabu au mafao ya aina fulani kuliko ilivyo sasa ambapo dereva wa mbunge akifia kazini sijui zaidi ya rambirambi ana haki gani nyingine.

Hili hata hivyo ni jambo ambalo ni wabunge wenyewe wanaweza kuamua kulitungia sheria badala ya kusubiri kuipigia magoti serikali. Mambo yote niliyoyapendekeza hapa na mengine ambayo yapo mbeleni utaona kuwa yanawezekana kufanywa na kuletwa Bungeni na wabunge wenyewe. Jambo moja ambalo hatuna budi kulikataa ni kuambiwa kuwa “serikali haina fedha”. Mbunge atakayekubali kusikia kuwa ati serikali “haina fedha kwa wakati huu” kuhusu mabadiliko haya mbunge huyo itabidi tumtimue Bungeni. Tuna kiasi cha kutosha cha fedha na wakati umefika kuanza kuweka vipaumbele vyetu sawasawa.

Hii ina maana gani? Kwamba, hatukumbuki, hatujifunzi, na hatujali. Tunaishi kwa nasibu na kutegemea mapenzi ya Mungu.
 
.......kama ile ya Dr. Masau eehhh!!....hivi ile investigation yake iliishia wapi?

Iliishia ****** kama kawaidam yake...kimbelembele cha kuandika eti sijui barua kwa law firm gani ile...kimbelembele kile kile cha kuandika barua tukakiona kwa Isha Sessay...eti huyu shori naye aliandikiwa barua....kwikwikwiiiii
 
Kama kuna kitu cha kushangaza au kusikitisha ni jinsi gani ajali hii inavyoonyesha mawazo ya Watanzania yalivyo.

Nilitarajia kurasa hizi 27 zingezungumzia ulazima wa kuboresha barabara, kuimarisha hospitali zetu, kuhakikisha kuwa mafunzo ya usalama wa barabara na udereva yanafanyiwa umakini, lakini gumzo kubwa ni mambo ya kafara na hujuma kisa ni Mwakyembe!

Je wiki kadhaa zilizopita wakati washabiki wa Simba na karibu wachezaji wa Simba wapate ajali mbaya pale Morogoro, tungesema ni Yanga waliochimba mahandaki barabarani au kulegeza nati za gurudumu?

NI Ndugu zetu wangapi; Baba, Mama, Mjomba, Shangazi, Kaka, Dada, Shemeji, Wifi, Babu na Bibi, Rafiki hata Majirani ambao wamepoteza maisha kutokana na ajali za barabarani ambazo chimbuko kubwa ni 1. Ubovu wa Barabara, 2. Ujuvi wa madereva, 3. Magari mabovu, 4, Ufinyu wa huduma za Uokoaji, Tiba na Dharura na zaidi kuwa ni za viwango vya chini?

Tangu Salome Mbatia mpaka leo hii ya Mwakyembe, ni Watanzania wangapi ambao wamepoteza maisha kutokana na ajali za barabarani?

Je kama Taifa tumechukua hatua gani kulifanyia utatuzi tatizo hili sugu?

Siku mashabiki wa Simba walipopata ajali kule Morogoro, Mwenyekiti wa Simba Hassani Dalali alitoa wito kuitaka Serikali na Tanroads kufanya utafiti wa kina wa kinachosababisha ajali za barabarani Nanukuu kutoka Habari Leo
HabariLeo | Dalali ataka barabara ya Dodoma ichunguzwe

Dalali ataka barabara ya Dodoma ichunguzwe

Mwenyekiti wa Simba Hassan Dalali ameiomba Wizara ya Miundombinu kuifanyia ukaguzi barabara kuu ya Dodoma - Morogoro inayopitia katika Kijiji cha Chamale, Kata ya Magubike, wilayani Kilosa, kwa ajili ya kuweza kubaini vyanzo halisi vya ajali za mara kwa mara.

Dalali alitoa ushauri huo alipowatembelea majeruhi ambao ni mashabiki wa timu yake waliopata ajali usiku wa Aprili 26 katika kijiji hicho walipokuwa wakitoka kuishuhudia Simba ilipocheza na Polisi Dodoma.

"Ipo haja kwa serikali kuingilia kati ili kujua kwa nini eneo hilo linatokea ajali za mara kwa mara ili kunusuru maisha ya watu …huenda eneo hilo lina matatizo au vijana ndiyo wanaomwaga mafuta ya dizeli, " alisema Dalali.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa Simba, iwapo serikali kupitia wizara inayohusika kulikagua eneo hilo la barabara huenda ikatoa majibu sahihi ya kubaini iwapo lami iliyotumika ina kasoro ama kuna tatizo lingine litakalopaswa kuchukuliwa hatua za haraka.

Mashabiki kadhaa wa timu hiyo walinusurika kifo baada ya basi dogo walilokuwa wakisafiria kutoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam, kuacha njia na kupinduka eneo la Chamale, Kijiji cha Magubike, wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Ajali hiyo ilitokea saa 5: 45 usiku katika eneo hilo baada ya siku mbili kupita wakati ilipotokea ajali mbaya ya basi mali ya Kampuni ya RS Investiment iliyosababisha kifo cha Mbunge wa zamani wa Jimbo la Biharamulo Magharibi (TLP), marehemu Phares Kabuye na watu wengine wawili na kujeruhi abiria 54.

Mchana wa siku hiyo, viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro akiwamo Mwenyekiti na Katibu wake walipata ajali katika eneo hilo na usiku wake ndipo mashabiki hao wa Simba walipatwa na mkasa huo. Mashabiki 12 walijeruhiwa katika ajali hiyo na kukimbizwa Hospitali ya Misheni ya Berega iliyopo wilayani humo.

Badala ya kuchukua fursa hii ya ajali iliyomkumba mtu maarufu kama Mwakyembe kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya ajali za Barabarani, tunabakia kubishana na hekaya za nani mchawi!

Inachosha!
 
Rev.Kishoka,
Mkuu wangu nadhani watu wanafahamu yote haya na wameisha sema sana lakini inapofikia vita ya Mafisadi na wanaopata ajali hizi ni Wapiganaji inabidi watu wajiulize kwani hakuna mchawi ila ni Assassin kind of..
Hivyo pamoja na barabara zetu kuwa mbaya tena ziliikuwa mbaya zaidi wakati wa Mwinyi na Nyerere lakini siku zote tumeona sababu za uzembe wa madereva, barabara au wanyama kusababisha ajali hizo sio fumbo hizi ambazo hazina hata uchunguzi.

Mama Mbatia ametutoka hakuna uchunguzi wala hadithi nyuma ya ajali ile, yule dereva hajapatikana hadi kesho na wala hatufahamu kilitokea kitu gani. Kina Mwaikambo, Chacha haya yote hayana hata sura ya kutazama kilichotokea tukapata jibu la ajali moja baada ya nyingine.. Mimi nadhani speculations kama hizi ndizo hutupa ufumbuzi wa kiini cha ajali hizi na hakuna lisilowezekana..

Hata huku majuu ajali kama hizi hutokea kila siku na watu wanakufa vile vile lakini aghalab kusikia sababu za kijinga kama nyumbani na uchunguzi kufungwa..ati tairi lilichomoka!..mara shimo kisha shimo lenyewe basi hata halina kina cha kuzungumziwa..Ina maana kweli sisi tunashindwa kuweka vielelezo vya ajali hizi zaidi ya uzushi!.. and why tunatafuta sababu badala ya ajali yenyewe kujieleza.
 
Pole sana Ndugu Mwakyembe, Mungu akupe ahueni haraka urudi kupambana na mafisadi
 
LATEST: Mpiganaji Dk Harrison Mwakyembe atapelekwa Dar kwa charter plane mchana huu kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kidaktari. Kwa sasa anaendelea vizuri Wadi No 5 katika hospitali ya mkoa Iringa. Dereva wake ni mzima kabisa, na yuko chini ya ulinzi wa polisi kwa sasa, hapo hapo hospitali. Anahojiwa kutokana na kudanganya hapo awali kuwa gari yake iligongwa kwa nyuma. Mtu aliyeenda eneo la ajali na baadaye hospitali anasema gari ya Dr Mwakyembe aina ya Landcruiser ilikuwa ina-overtake malori mawili na ghafla dereva alishtukia shimo kubwa mbele yake akapoteza control na gari ikapinduka ikiwa pia imegonga mti mkubwa na kuuong'oa.

Ninaimani hakuna hila za kina Malya na Chaha Wangwe, lakini ni vyema pia kuwa waangalifu na watumishi wetu hata wa majumbani kwani kwenye mapambano kama haya mtu yeyote anaweza kutumiwa.
Sijui wanasiasa wetu wanajifunza nini kutokana na jinsi umma ulivyoguswa na ajali ya ndugu yetu.Ni vyema tukasoma nyakati kuwa kuktenda mema umma unakujali na kukufariji.Maana ninaimani kama ingekuwa ajali za baadhi ya jamaa zetu fulani nadhani watu wangekuwa wanasindikiza na arubadili ili watu hao waondoke katika jamii yetu.
 
Ninaimani hakuna hila za kina Malya na Chaha Wangwe, lakini ni vyema pia kuwa waangalifu na watumishi wetu hata wa majumbani kwani kwenye mapambano kama haya mtu yeyote anaweza kutumiwa.
Sijui wanasiasa wetu wanajifunza nini kutokana na jinsi umma ulivyoguswa na ajali ya ndugu yetu.Ni vyema tukasoma nyakati kuwa kuktenda mema umma unakujali na kukufariji.Maana ninaimani kama ingekuwa ajali za baadhi ya jamaa zetu fulani nadhani watu wangekuwa wanasindikiza na arubadili ili watu hao waondoke katika jamii yetu.

Mbona ni kama kuna harufu ya ka-ufisadi ktk hii ajali??? 😕 Polisi wanasema ajali imesababishwa na gari ya mh.mbunge lilipo-overtake lori na kuingia ktk shimo (angalia picha chini). Lakini dereva wakati anahojiwa na Abdallah Majura wa BBC alisema; LORI LILIKUWA LINAWAFUATA NYUMA YAO KWA KASI SN, WAKATI AKAWA ANAJARIBU KULIKWEPA BADO LINAWAFUATA THEN LIKAWA GONGA KWA NYUMA NDIO LIKAPINDUKA.

Ile speech ya polisi pia ina mashaka kdg; hivi hili shimo ndio lisababishe tairi ichomoke na kupinduka after over take?

i390_Shimo.JPG
 
Mbona ni kama kuna harufu ya ka-ufisadi ktk hii ajali??? 😕 Polisi wanasema ajali imesababishwa na gari ya mh.mbunge lilipo-overtake lori na kuingia ktk shimo (angalia picha chini). Lakini dereva wakati anahojiwa na Abdallah Majura wa BBC alisema; LORI LILIKUWA LINAWAFUATA NYUMA YAO KWA KASI SN, WAKATI AKAWA ANAJARIBU KULIKWEPA BADO LINAWAFUATA THEN LIKAWA GONGA KWA NYUMA NDIO LIKAPINDUKA.

Ile speech ya polisi pia ina mashaka kdg; hivi hili shimo ndio lisababishe tairi ichomoke na kupinduka after over take?

i390_Shimo.JPG
Aljuniour,

Hata ukiliangalia hilo gari kweli limegongwa kwa nyuma? Gari ligongwe na lori kwa nyuma kweli hiyo sehemu yote ya nyuma itatoka nzima hivyo?

Mimi nahisi dereva alikuwa kwenye speed kali wakati ana overtake na alipojaribu kurudi upande wake akakumbana na hilo shimo. Huko nyuma niliwahi kuandika kwamba Mashangingi sio magari mazuri kwenye ku balance, centre of gravity yake iko juu kwahiyo ni rahisi kuhama haraka na hivyo kuliyumbisha gari.

Kama gari limenyoka mbele hilo shimo ni dogo sana kuweza kuliangusha shangingi. Tunaposema mashangingi yanafukia mashimo, ni pamoja na mashimo makubwa zaidi ya hiilo.

Hapo dereva atakuwa alikuwa anajiokoa tu, pia ni kumwonea huyo derva kumwuliza maswali saa moja baada ya ajali, wakati bado amechanganyikiwa. Inaelekea huyo dereva hapo hakuwa na hata mtu mmoja wa kumsaidia, polisi ambao ndio wangetakiwa kuhakikisha yu salama kiafya na anakuwa chini ya ulinzi, nafikiri hawakuwa concerned kama na usalama zaidi.

Kilio cha usalama barabarani tumelia kweli kweli, kijana mwenzetu Masha tungetemea kukaa kwake kote nje na kuwa mwanasheria kungemsaidia kutusaidia kutengeneza sheria za kupambana na makosa mbalimbali ya barabarani. Tanzania tunaendesha magari kwa speed kubwa sana, mara nyingi hata mara mbili ya speed inayoruhusiwa. Hiyo barabara nafikiri maximum ni 80km/h, kwa mwendo kama huo hata likitokea ghafla una nafasi ya kuli balance gari katikati. Lakini maderva wengi huwa wanaenda 120km/h mpaka 160km/h mwendo ambao hata kwa motor ways za Europe bado watu wengine huwa hatudiriki hata kuukaribia hata barabara ikiwa tupu kwa mfano usiku.
 
Hapa Watanzania ndipo tuliporogwa, sijui tutakuja kupona lini. Tutakimbilia kutibiwa nje mpaka lini?

Jamani tuimarishe hospitali zetu za taifa, za mkoa na wilaya, hizi pesa tunazotupa kupeleka watu SA, India na Europe, zinaweza kuokoa maelfu ya watu kama tutazitumia vizuri hapo TZ.

Technology ya tiba sasa imekuwa wazi, bora pesa zako, tutatajirisha watu nje mpaka lini?

Hilo la kumtoa dereva nje bila uchunguzi wa ziada nafikiri pia ni matatizo ya sisi Watanzania au Waafrika ya kutokuthamini wasaidizi wetu. Tuna wa treat vibaya wasaidizi wa ndani huku tunawaachia kulea wanetu. Hatuwapi haki zote madereva huku uhai wetu uko mikononi mwao. Huyo dereva naye inatakiwa awe mfanyakazi wa bunge na ungekuwa wajibu wa bunge kuangalia maslahi yake. Lakini kama ilivyo TZ, kigogo anapelekwa sehemu ya maana kutibiwa, vijana maskini wenzetu wanaacha wanazubaa zubaa, nani atawatetea?

Nimeshaona mara nyingi tu TZ, kigogo anajichana huku dereva anahangaika na njaa kwenye gari, kisha wanaondoka safari ya mwendo. Looh! kutembea na dereva mwenye mjaa mbona ni kujitakia balaa? Kuna mambo mengi sana hayako sawa huko nyumbani!

Mkuu kwenda kutubiwa nje sio sisi tu, tuwe na kumbukumbu jamani tusinogewe na nyimbo hizi haya mambo hata watu tunaofikiri wametuzidi uwezo hofanya hivyohivyo... Mfalme Hussein Wa Jordan, Omar Bongo umesikia yuko wapi? na wengineo wengi tu..labda useme ni tabia ya kinyonge na haifai lakini sio sisi tu tnaoendekeza haya.
La Dereva kutolewa nje bila kufanyiwa uchunguzi ni ktu cha ajabu sana naungana nawewe lakini bora hata huyo ni Dereva, wakubwa wana ubinafsi wa ajabu kabisa kabisa nakumbuka mheshimiwa mmoja alipata ajali nikiwa Morogoro akiwa na mwanae wa kumzaa cha ajabu yule mtoto hakuangaliwa kabisa wala hakupewa hata panadol!
 
Mkuu kwenda kutubiwa nje sio sisi tu, tuwe na kumbukumbu jamani tusinogewe na nyimbo hizi haya mambo hata watu tunaofikiri wametuzidi uwezo hofanya hivyohivyo... Mfalme Hussein Wa Jordan, Omar Bongo umesikia yuko wapi? na wengineo wengi tu..labda useme ni tabia ya kinyonge na haifai lakini sio sisi tu tnaoendekeza haya.
La Dereva kutolewa nje bila kufanyiwa uchunguzi ni ktu cha ajabu sana naungana nawewe lakini bora hata huyo ni Dereva, wakubwa wana ubinafsi wa ajabu kabisa kabisa nakumbuka mheshimiwa mmoja alipata ajali nikiwa Morogoro akiwa na mwanae wa kumzaa cha ajabu yule mtoto hakuangaliwa kabisa wala hakupewa hata panadol!
Kela72,

Labda huna habari, uliza ubalozi wetu kama wa UK, India na SA, kuna watu wanapelekwa huko hata kufanya vipimo vya pressure tu.

Nitaelewa kama kuna magonjwa ambayo tumeshindwa kuwa na daktari bingwa, kama viongozi hao watakimbizwa popote kutibiwa kama ilivyokuwa case ya Nyerere. Lakini kwasasa sio hivyo mkuu, kuna viongozi ambao mpaka wamewahi kuwa mawaziri wakuu, wanaenda nje kufanyiwa check-ups, baada ya hapo dawa pounds 10,000 kwa miezi mitatu, tena kila safari wananunua duka hilo hilo moja la madawa. Hata uwe unatibiwa nini, nakuambia bill ya hayo madawa haiwezi kufikia 10,000 kwa miezi mitatu hapa UK, ni wizi mtupu.

Tanzania sasa inapeleka maelfu ya wagonjwa nje kwa magonjwa ya kawaida kabisa, ambayo laiti tungetengeneza hospitali zetu, tukawasomesha vijana wetu inavyotakiwa wala kusingelikuwa na haja kwa hao watu kwenda kutibiwa nje.

Mimi naona ni heri hata tuwajengee 5 stars hapo Muhimbili, wakitaka kutibiwa na wazungu basi tuwaletee wazungu hao hapo Muhimbili. Lakini resources zote hizo zitatumika pia kutibu na Watanzania wengine.

Kuna haja ya kufanya research kujua Tanzania kama taifa tunatumia pesa ngapi kuwapeleka nje hawa wagonjwa kuanzia wale wa serikali, majeshi na hata watu binafsi.

Hii huenda ni sawa na zamani tulipokuwa tunahangaika kupeleka watoto shule Uganda na Kenya ili wakajifunze kuongea Kiingereza. Mbona sasa tumefuta hilo tatizo hasa kwa upande wa shule binafsi?
 
Kwa kweli Tanzania tubadilike kuhusu watumiishi wetu. mara nyingi kiongozi akipata ajali anashugulikiwa kikamilifu husikii driver katibiwa au anaendelea vipi. Ma driver wanabidi waheshimiwe sana kwasababu wanabeba maisha ya viongozi na kujua siri zao nyingi.
 
Mtanzania,

Nani kakuambia kuwa hiyo barabara unaweza kwenda speed ya 80km/hr? Hebu tuibadilishe hiyo tutapata 22m/sec. Sasa hebu angalia urefu ulipo kutoka kwenye hivyo vichaka ni kama mita 10 hivi kutoka katikati ya barabara au tuseme 15m. Sasa tukisema speed ya wanyama wanaokimbia kuingia barabarani ni 10-15m/sec, ina maana kuwa wanahitaji just 1 sec kuwa katikati ya barabara na wewe waenda hiyo speed ya 22m/sec, utasikia tu BOOOOMMM!!!!

Mtanzania, kuna kitu kinaitwa Right of way ya barabara. Hili ni eneo linatakiwa kuwa jeupe hasa na kwenye highway (kwa nyie wa juu) ambako magari huenda speed zaidi ya 120km/hr, unakuta linaweza kuwa pana hata mita zaidi ya 100 na bado wanaweka na uzio kuzuia watu na wanyama na hapo ndipo wanakwambia nenda unavyotaka mwanangu (Wageruman hawana speed limit kwenye baadhi ya highway zao -Autostrad). Pia zaidi ya hilo, lane za barabara zinakuwa ni pana sana na magari yote yanakwenda upande mmoja na pia kuna sehemu ya wewe kusimamisha mchuma wako ukipata ajali. Kama sikosei lane moja inaweza kuwa hata 3,75m. jambo linalowapa waendeshaji confort kubwa sana waendapo barabarani kwani gari jingine liko mbali sana na hata ukijisahau kidogo wakati unabadili CD, bado unakuwa na muda wa kulinyoosha gari.

Hapo hamna tofauti kabisa na mitaani (streets) na inatakiwa iwe kwenye 50km/hr. Inabidi TANROADS waanze kupanua haya maeno pembeni mwa barabara ili walau kuwe na urefu wa mita 15-20 kama kweli wanaziita highway.

Kuhusu kuligonga gari wa nyuma. Kama uko kwenye highspeed, haihitaji nguvu kubwa kuliangusha. Huwa inakuwa kama unakwanguliwa tu kidogo. Kumbuka ni rahisi kukata kona kwenye gari linalotembea kuliko lililosimama. Na hivyohivyo ni rahisi kulikata mtama gari kama linakwenda speed kali.

Mwisho ni hayo mashimo. Kwa nini wasiwe na mpango wa kuyapitia na kuyaziba? Yanaingia maji chini ya barabara (sehemu ilipo lami) na hivyo kuharibu zaidi eneo zima. Kama wangelipitia zamani wakati shimo linaanza, basi leo hii eneo lolte hilo lingekuwa zima kabisa. Hawa jamaa wanafikiria tu kujenga na bila kuwa na mpango wa kufanyia matengenezo ya haraka? Wakitaka hivyo basi waanze kujenga barabara za Zege la cement maana hapo wanaweza kusahau kuja fanyia matengenezo (so longer watafanya compaction ya udongo vizuri).
 
Mtanzania,

Hapo hamna tofauti kabisa na mitaani (streets) na inatakiwa iwe kwenye 50km/hr. Inabidi TANROADS waanze kupanua haya maeno pembeni mwa barabara ili walau kuwe na urefu wa mita 15-20 kama kweli wanaziita highway.

.

i390_Shimo.JPG

Hayo maeneo ya pembeni ya barabara yanaitwa Mabega, Kwa barabara hii ya Makambako-Iringa kabla ya ukarabati katika miaka ya tisini sehemu kubwa ya barabara ilikuwa na mabega hayo ambayo yalikuwa na upana wa mita chini ya tatu.​
 
Back
Top Bottom