Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Exactly my point. Alitakiwa ajue, maana alizinduka baada ya kusafishwa michubuko.
umeambiwa aliumia kwenye taya, taya ni kiungo muhimu kinachofanya mdomo wa mtu uweze kumove anapozungumza..ni kiungo ambacho meno ya chini yameshikanishwa juu yake. na hivyo kufanya kuzungumza kokote kuwa kugumu.
Ndo maana nikasema kwa nini hakuuliza, ukanambia inawezekana aliuliza.
Hapana sikukuambia hivyo, ulifikiria nimekuambia, nilikuuliza swali wewe umejuaje kama hakuuliza? Hii ni tofauti na kauli isemayo "aliuliza". Tofauti ya swali na kauli ni kuwa moja inasema kitu ikidai ukweli na nyingine inauliza kitu ikitafuta ukweli.
Hapana sija wonder ninakusaidia wewe kuwonder kabla ya kutoa tuhuma nzito.Sasa hivi una wonder kama alijua.
Posted by Dilunga: basi angeonyesha leadership, angesema kutoka kitandani, jamani mnanipeleka Muhimbili, mwenzangu yuko wapi, kapona? Tusimtelekeze mwananchi wangu.
ni kuwa ameumia taya, taya ni kiungo ambacho..
Posted by Mwanakijiji: Umejuaje hajauliza, au unataka kila nenoanalolitoa liandikwe kitabuni na kutangazwa..?
Hili linaitwa swali.
Umejuaje kuna mtu katelekezwa? Kama madaktari wameridhika aliyenusurika katika ajali hayuko hatarini wamamruhusu kurudi nyumbani kwanini kuitwe huko kutelekezwa? Hata hapa (marekani) ni mara ngapi watu wanapata ajali na baada ya uchunguzi na uangalizi wanaruhusiwa kurudi nyumbani? Huko si kutelekezwa.Sasa, alijua au hakujua mwenzake katelekezwa?
Kutelekezwa ni kuwa huyo dereva alikuwa katika hali mbaya na alitakiwa kupelekekwa MOI, na licha ya kujulikana hali yake hiyo Mwakyembe akiwa na taarifa ya mahitaji ya huyo dereva akaamua kuondoka bila kumpa taarifa au nafasi ya kuondoka naye na hakufanya juhudi zozote (kama zimo ndani ya uwezo wake) kumsaidia dereva naye kwenda huko MOI. Hicho kinaitwa kutelekezwa, yaani kumuacha mtu aliyeahidiwa au anayehitaji au kutegemea msaada wako wakati una uwezo wa kufanya hivyo.
Iwapo alijua basi alitakiwa asihi waje nae wote Moi.
Afanye hivyo kama nani? Madaktari ndiyo wana mrefer mtu kwenda hospitali ya juu zaidi, sasa kwa vile ni Mbunge ndiyo awe na uwezo wa kuamua nani apelekwe hospitali gani kwa uwezo gani alionao? Mambo ya tiba wanaachiwa madaktari, lile neno 'Dr' haina maana ni daktari wa binadamu.
Aulize nini? Sasa kwa mfano anauliza "what happened to my driver" halafu daktari (mtaalamu aliyesomea magonjwa na tiba) akamjibu na kusema "tumemchunguza na vipimo vyote vinaonesha yuko salama na tumemruhusu kwenda nyumbani", sasa baada ya jibu hilo Mwakyembe anatakiwa kusema nini? "hapana mmekosea, mpelekeni Muhimbili na yeye"?Kama hakujua, basi kwa nini hakujali kuuliza?
Maana anaongea, keshasafishwa michubuko. Ni hivi:
mmh.. nah!
umeambiwa kaumia na taya na labda maumivu mengine ndiyo maana bado yuko hospitali.Mwakyembe kachubuka.
Bunge limempeleka Moi kuchekiwa zaidi ikibidi ng'ambo.
Ni maamuzi ya madaktari, Bunge siyo jopo la madaktari. Na ikibidi ng'ambo siyo jambo geni, kwani hata watu wa kawaida wanapelekwa ng'ambo pale inapobidi.
Dereva aliyeumia kichwa hatachekiwa Moi, kaende lwake.
Hapana huu ni upotoshaji. Hivi "kaenda lwake" au wataalamu wa fani ya udaktari wameona haitaji zaidi, au unafikiri anahitaji zaidi kwa vile umejua ni jinsi gani ameumia na hakupewa tiba anayostahili? au unahisi tu kwa vile kaumia kichwa basi ina maana hali yake ni mbaya sana. Umeuliza nature ya maumivu hayo ya kichwa?
Kundi JF linasema Mbunge pole, shujaa.
I don't know about that..
Wengine tunasema kila Juma na Roza nchini, kila "hohehahe," anastahili usawa wa haki ya matibabu kama wote.
ndipo tatizo lilipo, hadi hivi sasa sijaona dai lolote kuwa kuna mtu anayehitaji matibabu ambaye kanyimwa matibabu hiyo, mtu huyo awe Juma au Rosa! Unless unatetesi kuwa dereva alinyimwa matibabu ambayo alitakiwa kupata baada ya ajali! Unayo?