Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Exactly my point. Alitakiwa ajue, maana alizinduka baada ya kusafishwa michubuko.

umeambiwa aliumia kwenye taya, taya ni kiungo muhimu kinachofanya mdomo wa mtu uweze kumove anapozungumza..ni kiungo ambacho meno ya chini yameshikanishwa juu yake. na hivyo kufanya kuzungumza kokote kuwa kugumu.
Ndo maana nikasema kwa nini hakuuliza, ukanambia inawezekana aliuliza.

Hapana sikukuambia hivyo, ulifikiria nimekuambia, nilikuuliza swali wewe umejuaje kama hakuuliza? Hii ni tofauti na kauli isemayo "aliuliza". Tofauti ya swali na kauli ni kuwa moja inasema kitu ikidai ukweli na nyingine inauliza kitu ikitafuta ukweli.
Sasa hivi una wonder kama alijua.
Hapana sija wonder ninakusaidia wewe kuwonder kabla ya kutoa tuhuma nzito.

Posted by Dilunga: basi angeonyesha leadership, angesema kutoka kitandani, jamani mnanipeleka Muhimbili, mwenzangu yuko wapi, kapona? Tusimtelekeze mwananchi wangu.


ni kuwa ameumia taya, taya ni kiungo ambacho..

Posted by Mwanakijiji: Umejuaje hajauliza, au unataka kila nenoanalolitoa liandikwe kitabuni na kutangazwa..?

Hili linaitwa swali.

Sasa, alijua au hakujua mwenzake katelekezwa?
Umejuaje kuna mtu katelekezwa? Kama madaktari wameridhika aliyenusurika katika ajali hayuko hatarini wamamruhusu kurudi nyumbani kwanini kuitwe huko kutelekezwa? Hata hapa (marekani) ni mara ngapi watu wanapata ajali na baada ya uchunguzi na uangalizi wanaruhusiwa kurudi nyumbani? Huko si kutelekezwa.

Kutelekezwa ni kuwa huyo dereva alikuwa katika hali mbaya na alitakiwa kupelekekwa MOI, na licha ya kujulikana hali yake hiyo Mwakyembe akiwa na taarifa ya mahitaji ya huyo dereva akaamua kuondoka bila kumpa taarifa au nafasi ya kuondoka naye na hakufanya juhudi zozote (kama zimo ndani ya uwezo wake) kumsaidia dereva naye kwenda huko MOI. Hicho kinaitwa kutelekezwa, yaani kumuacha mtu aliyeahidiwa au anayehitaji au kutegemea msaada wako wakati una uwezo wa kufanya hivyo.
Iwapo alijua basi alitakiwa asihi waje nae wote Moi.

Afanye hivyo kama nani? Madaktari ndiyo wana mrefer mtu kwenda hospitali ya juu zaidi, sasa kwa vile ni Mbunge ndiyo awe na uwezo wa kuamua nani apelekwe hospitali gani kwa uwezo gani alionao? Mambo ya tiba wanaachiwa madaktari, lile neno 'Dr' haina maana ni daktari wa binadamu.
Kama hakujua, basi kwa nini hakujali kuuliza?
Aulize nini? Sasa kwa mfano anauliza "what happened to my driver" halafu daktari (mtaalamu aliyesomea magonjwa na tiba) akamjibu na kusema "tumemchunguza na vipimo vyote vinaonesha yuko salama na tumemruhusu kwenda nyumbani", sasa baada ya jibu hilo Mwakyembe anatakiwa kusema nini? "hapana mmekosea, mpelekeni Muhimbili na yeye"?
Maana anaongea, keshasafishwa michubuko. Ni hivi:

mmh.. nah!
Mwakyembe kachubuka.
umeambiwa kaumia na taya na labda maumivu mengine ndiyo maana bado yuko hospitali.
Bunge limempeleka Moi kuchekiwa zaidi ikibidi ng'ambo.

Ni maamuzi ya madaktari, Bunge siyo jopo la madaktari. Na ikibidi ng'ambo siyo jambo geni, kwani hata watu wa kawaida wanapelekwa ng'ambo pale inapobidi.
Dereva aliyeumia kichwa hatachekiwa Moi, kaende lwake.

Hapana huu ni upotoshaji. Hivi "kaenda lwake" au wataalamu wa fani ya udaktari wameona haitaji zaidi, au unafikiri anahitaji zaidi kwa vile umejua ni jinsi gani ameumia na hakupewa tiba anayostahili? au unahisi tu kwa vile kaumia kichwa basi ina maana hali yake ni mbaya sana. Umeuliza nature ya maumivu hayo ya kichwa?
Kundi JF linasema Mbunge pole, shujaa.

I don't know about that..

Wengine tunasema kila Juma na Roza nchini, kila "hohehahe," anastahili usawa wa haki ya matibabu kama wote.

ndipo tatizo lilipo, hadi hivi sasa sijaona dai lolote kuwa kuna mtu anayehitaji matibabu ambaye kanyimwa matibabu hiyo, mtu huyo awe Juma au Rosa! Unless unatetesi kuwa dereva alinyimwa matibabu ambayo alitakiwa kupata baada ya ajali! Unayo?
 
Mungu wangu!....Jamani hii tena vipi!. Ama kweli hujafa hujaumbika.. duh!
Haya tupeni habari zaidi, kanusurika?
 
Dr dilunga nimemfanyia samare toka bbcswahili

Francis nyabusami daktari aliesafiri na Mwakyembe toka toka iringa mpaka dar kasema.....yuko kwenye conshasi kaumia kwenye shingo na mkono.....kalala kwa sababu ya maumivu,uchovu na dawa...

ofisi ya bunge thomas kashirira ofisi ya bunge....anapeleka moi kwa matibabu zaidi....kaumia sana kwenye bega karibia ya shingo lakn hajavunjika..kapata maumivu makubwa kwenye kichwa na kwenye kifua.....

---- labda tujiulize maelezo ya kamanda wa na dereva wa mwakyembe Joseph msuya kwanini yanapishana.....

kamanda wa polisi akielezea chanzo cha ajali kasema....gari lilikuwa lina overtake lori likakutana na shimo na tairi likachomoka na kupinduka......

dereva wa mwakyembe joseph msuya kupitia gazeti la alasiri leo kasema chanzo cha ajali......ni kuwa lori likuwa linaifata gari kwa nyuma na kila alipojaribu kulikwepa alishindwa maana gari likuwa linamfata kila akijaribu kulikwepa kisaha lori hilo kuligonga gari la mwakyembe kwa nyuma na kupinduka mara 4.....
 

dilunga ulifaulu darasa la 7? una kichwa kigumu kweri kweri.......kwa kukusaidia sikiliza bbc swahili unaambiwa hakuwa na uwezo wa kuongea....

Nifaulu darasa la saba, thubutuu...! Si heri hata ningejaribu hilo la saba; Nilikwama mtihani wa darasa la nne.

Lakini wewe uliyefaulu hata ningeshikiwa panga tubadilishane vichwa ningedai changu, sio cha Yo Yo.

Angalau mimi kichwa changu cha darasa la nne kinajifikirisha chenyewe. Kinakataa nadharia potofu za njama, kwamba Mwakyembe kagongwa na lori lililotumwa na Rostam. Kichwa changu cha darasa la nne kinanambia ni afadhali nimsikilize Dk. Kashilila aliyetibu michubuko ya Mwakyembe na kusema anazungumza kuliko nisikilize kina Charles Hillary wa London na watupu wa BBC walioaanda mikutano ya kusameheana kati ya watoto wa Amin na Nyerere kana kwamba vita vya nchi vilikuwa ni uadui wa familia mbili. Kichwa changu cha darasa la nne kinanambia ukiendesha mbio, bila umakini, ni hatari, awepo Rostam Aziz, asiwepo.

Na kwamba mkipata ajali wawili, wewe ukiwa mtu mashuhuri si vema, si uungwana, si uongozi mwema, ukaangalia mwenzako anatelekezwa aende zake wewe unaenda kuchunguzwa zaidi michubuko. Hapana, sikufika, sio sikufaulu, sikunusa mtihani wa darasa la saba.

Mwisho, nisingependa kufaulu darasa lako la saba halafu nikawa naandika lugha za maneno kama "kweri kweri."
 
Nifaulu darasa la saba, thubutuu...! Si heri hata ningejaribu hilo la saba; Nilikwama mtihani wa darasa la nne.

Lakini wewe uliyefaulu hata ningeshikiwa panga tubadilishane vichwa ningedai changu, sio cha Yo Yo.

Angalau mimi kichwa changu cha darasa la nne kinajifikirisha chenyewe. Kinakataa nadharia potofu za njama, kwamba Mwakyembe kagongwa na lori lililotumwa na Rostam.

Na hili wazo umelitoa wapi?
Kichwa changu cha darasa la nne kinanambia ni afadhali nimsikilize Dk. Kashilila aliyetibu michubuko ya Mwakyembe na kusema anazungumza

Ukisikia mtu anaitwa "dr" haina maana wote ni matabibu. Sasa sijui ni wapi umepata hilo wazo kuwa Dr. Kashillilah ndiyo alikuwa anamtibu Mwakyembe!?

kuliko nisikilize kina Charles Hillary wa London na watupu wa BBC walioaanda mikutano ya kusameheana kati ya watoto wa Amin na Nyerere kana kwamba vita vya nchi vilikuwa ni uadui wa familia mbili.

hii haihusiani kabisa na mjadala; simply irrelevant!

Kichwa changu cha darasa la nne kinanambia ukiendesha mbio, bila umakini, ni hatari, awepo Rostam Aziz, asiwepo.

Sasa sijui gari linaweza kwenda bila kwenda mbio!?

Na kwamba mkipata ajali wawili, wewe ukiwa mtu mashuhuri si vema, si uungwana, si uongozi mwema, ukaangalia mwenzako anatelekezwa aende zake wewe unaenda kuchunguzwa zaidi michubuko.

Ametelekezwa na nani huyo mwenzako? Maana upande mmoja unasema Mwakyembe ndiyo kamtelekeza wakati mwingine unasema si vizuri aangalie mwenzake akitelekezwa.. sasa ni nani hasa unayejua amemtelekeza huyo mwenzake?
Hapana, sikufika, sio sikufaulu, sikunusa mtihani wa darasa la saba.

siyo udhuru wa kutokufikiri vizuri!

Mwisho, nisingependa kufaulu darasa lako la saba halafu nikawa naandika lugha za maneno kama "kweri kweri."

wakati mwingine inabidi uangalie hata habari fulani kuona usahihi wake. Haiitaji elimu ya darasa la sita au la nne.
 
Kuna ajali mbaya sana imetokea Ihemi maeneo ya Iringa karibu na kijiji cha Ifunda ambayo inamhusisha Dr. Mwakyembe

Taarifa zaidi zinafuatia:

Picha ni hizi

i388_2.JPG

Dr Mwakyembe akifikishwa hospitali ya mkoa wa Iringa leo baada ya ajali

i389_Gari.JPG

Gari la Dr Mwakyembe likiwa limeharibika vibaya baada ya ajali

i390_Shimo.JPG

Shimo lililosababisha ajari ya Dr Mwakyembe

- Mkuu Watu, heshima mbele sana ahsante sana kwa hizi habari, wakuu unless kuna wanaojua zaidi ya yaliyosemwa na media kuhusu hii habari, basi watuwekee hapa tujue, maana ni mapema mno kuanza ku-speculate unless kuna concrete dataz, kama zipo ziwekwe hapa basi!

FMEs!
 
Vyanzo vya Sumbawanga vinatema kwamba roli lililogonga gari la mwakyembe lilikuwa linaendeshwa na RA akishirikiana na EL, ndani ya roli inasemekana kulikuwa na ndondocha kadhaa wakiwamo akina Balali, Mbatia, Wangwe, Dito, Chifupa, Moringe wa Sokoine, Mchonga, James Dandu, na Kolimba.

Conspiracies ndio hizo!
Duhh!!,very interesting......lets just blame it on the alcohol!
 
Angalau mimi kichwa changu cha darasa la nne kinajifikirisha chenyewe. Kinakataa nadharia potofu za njama, kwamba Mwakyembe kagongwa na lori lililotumwa na Rostam.
aisee wewe kama Dr kweli utakuwa wale walee.....nani kasema gari la mwakyembe limegongwa na lori la rostam?......mie sijasema wala sijakubali hoja hizo kama zimeandikwa humu...usiniwekee maneno mkuu....

Kichwa changu cha darasa la nne kinanambia ni afadhali nimsikilize Dk. Kashilila aliyetibu michubuko ya Mwakyembe
mkuu aisee unamaliza bandwidth tu bila sababu.....umemsikia dr kashilila kasema mwakyembe ana michubuko tu? au unataka kumuwekea maneno yasio an ukweli daktari wa watu.....

Kichwa changu cha darasa la nne kinanambia ukiendesha mbio, bila umakini, ni hatari, awepo Rostam Aziz, asiwepo.

Na kwamba mkipata ajali wawili, wewe ukiwa mtu mashuhuri si vema, si uungwana, si uongozi mwema, ukaangalia mwenzako anatelekezwa aende zake wewe unaenda kuchunguzwa zaidi michubuko. Hapana, sikufika, sio sikufaulu, sikunusa mtihani wa darasa la saba.
tehe tehe siwezi kujibizana na wewe unaniongezea njaa...nimekula kyepe yai na kyoda usiku huu......
 
Si tuliambiwa dereva ndio kaumia zaidi, ataendaje chini ya ulinzi halafu mbunge aende kwa medical specialists Dar? Dereva, usikubali huu unyama kabisa. Naomba useme yote unayoyajua kuhusu kumuendesha huyo bosi.

Wakati wa ajali ya waziri Mbatia iliyotokea mitaa hiyo hiyo ambacho hakikusemwa japo ilikuwa ni open secret Wizarani ni kwamba Mkuu alikuwa na hulka ya kuwatia pressure madereva wakimbize ili wafike haraka.

Kama ndio haya haya, dereva toa full testimony ya kila kitu, wasitake kabisa kukuletea huu unyama kiongozi mwakilishi wako kukimbia Muhimbili kukuacha mwanachi unaoza hapo na tunaambiwa wewe ndio umeumia zaidi.

Kulingana na habari zilizotolewa, dreva wa Mwakyembe alipata majeraha kidogo, na Mheshimiwa mbunge, Dr. Mwakyembe aliumia kichwani.

Kwenye medical field, trauma yoyote inayohusisha kichwa siyo ya kudharau. Mgonjwa anatakiwa kuwa under observation kwa muda, na ikibidi kufanyiwa CT scan ya kichwa ili ku-rule out head concussion na formation ya epidural hematoma (mgando wa damu kichwani) ambazo zinaweza kuwa fatal.

Mfano mzuri ni wa actress Natasha Richardson ambaye alipata head injuries akajiona kuwa yupo salama na matokeo yake tunayajua... she is down, six feet under!
 
Dk. Kashilila alisema kuwa Ofisi ya Bunge ipo tayari kutoa msaada kwa mbunge huyo kutibiwa hata ikiwa ni nje ya nchi, lakini akasisitiza itategemea ushauri wa wataalamu wanaomtibu.``

Hapa Watanzania ndipo tuliporogwa, sijui tutakuja kupona lini. Tutakimbilia kutibiwa nje mpaka lini?

Jamani tuimarishe hospitali zetu za taifa, za mkoa na wilaya, hizi pesa tunazotupa kupeleka watu SA, India na Europe, zinaweza kuokoa maelfu ya watu kama tutazitumia vizuri hapo TZ.

Technology ya tiba sasa imekuwa wazi, bora pesa zako, tutatajirisha watu nje mpaka lini?

Hilo la kumtoa dereva nje bila uchunguzi wa ziada nafikiri pia ni matatizo ya sisi Watanzania au Waafrika ya kutokuthamini wasaidizi wetu. Tuna wa treat vibaya wasaidizi wa ndani huku tunawaachia kulea wanetu. Hatuwapi haki zote madereva huku uhai wetu uko mikononi mwao. Huyo dereva naye inatakiwa awe mfanyakazi wa bunge na ungekuwa wajibu wa bunge kuangalia maslahi yake. Lakini kama ilivyo TZ, kigogo anapelekwa sehemu ya maana kutibiwa, vijana maskini wenzetu wanaacha wanazubaa zubaa, nani atawatetea?

Nimeshaona mara nyingi tu TZ, kigogo anajichana huku dereva anahangaika na njaa kwenye gari, kisha wanaondoka safari ya mwendo. Looh! kutembea na dereva mwenye mjaa mbona ni kujitakia balaa? Kuna mambo mengi sana hayako sawa huko nyumbani!
 
...Kwenye medical field, trauma yoyote inayohusisha kichwa siyo ya kudharau. Mgonjwa anatakiwa kuwa under observation kwa muda, na ikibidi kufanyiwa CT scan ya kichwa ili ku-rule out head concussion na formation ya epidural hematoma (mgando wa damu kichwani) ambazo zinaweza kuwa fatal.

Mfano mzuri ni wa actress Natasha Richardson ambaye alipata head injuries akajiona kuwa yupo salama na matokeo yake tunayajua... she is down, six feet under!

Ahsante dokta Pangu Pakavu. Unasema aliyeumia kichwa anatakiwa achikiwe zaidi. Yupi hapa achunguzwe?:

``alisema Kamanda Nyombi...kuwa wakati mbunge huyo amepelekwa Dar es Salaam, dereva wake aliyeumia kichwani na kukimbizwa pamoja naye katika hospitali ya mkoa wa Iringa, alitibiwa na kuruhusiwa.

Hata hivyo, mganga mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, Oscar Gabone alisema Dk Mwakyembe aliumia taya na hali yake sio mbaya sana kwani mfupa wa taya haukuvunjika.``

alisema Mboka Mwambusi, ambaye alifika eneo hilo muda mfupi baada ya ajali hiyo na kumchukua mbunge huyo kwenye gari lake hadi Iringa..."Alipata michubuko kidogo..."
 
...Nimeshaona mara nyingi tu TZ, kigogo anajichana huku dereva anahangaika na njaa kwenye gari, kisha wanaondoka safari ya mwendo. Looh! kutembea na dereva mwenye mjaa mbona ni kujitakia balaa? Kuna mambo mengi sana hayako sawa huko nyumbani!

...si hivyo tu, kigogo yupo kwenye 'matanuzi' dereva anaumwa na mbu kwenye gari, halafu alfajr dereva huyo huyo anatakiwa akanyage mafuta kms kadhaa toka mkoa mmoja kwenda mwingine!

...uchovu, njaa... yote yana influence 'poor judgements' hata kama dereva ni mzuri vipi.
 
Hapa Watanzania ndipo tuliporogwa, sijui tutakuja kupona lini. Tutakimbilia kutibiwa nje mpaka lini?

Jamani tuimarishe hospitali zetu za taifa, za mkoa na wilaya, hizi pesa tunazotupa kupeleka watu SA, India na Europe, zinaweza kuokoa maelfu ya watu kama tutazitumia vizuri hapo TZ.

Technology ya tiba sasa imekuwa wazi, bora pesa zako, tutatajirisha watu nje mpaka lini?

Hili ndugu yangu linasemwa na kurudiwa rudiwa weeee.. hadi tutachoka.

Hilo la kumtoa dereva nje bila uchunguzi wa ziada

Nadhani ni madaktari ndio wanatakiwa kuwa na kauli juu ya hali ya mgonjwa na mahitaji anayohitaji.

nafikiri pia ni matatizo ya sisi Watanzania au Waafrika ya kutokuthamini wasaidizi wetu. Tuna wa treat vibaya wasaidizi wa ndani huku tunawaachia kulea wanetu. Hatuwapi haki zote madereva huku uhai wetu uko mikononi mwao. Huyo dereva naye inatakiwa awe mfanyakazi wa bunge na ungekuwa wajibu wa bunge kuangalia maslahi yake. Lakini kama ilivyo TZ, kigogo anapelekwa sehemu ya maana kutibiwa, vijana maskini wenzetu wanaacha wanazubaa zubaa, nani atawatetea?

Hii ni point nzuri ambayo inarudiwa mara nyingi vile vile. Sidhani kama unamaanisha Mwakyembe alitakiwa atoke kwenye machela au huko chumbani kwenda kujua dereva anapata matibabu ya namna gani. Ila ukweli ndiyo huo, madereva wa wabunge lazima waingizwe kwenye utumishi wa umma!

Nimeshaona mara nyingi tu TZ, kigogo anajichana huku dereva anahangaika na njaa kwenye gari, kisha wanaondoka safari ya mwendo. Looh! kutembea na dereva mwenye mjaa mbona ni kujitakia balaa? Kuna mambo mengi sana hayako sawa huko nyumbani!

Yote haya ni kweli, lakini na hao madereva na wenyewe kwanini wasiwe na umoja wa aina fulani wenye kudai haki zao? Haya mambo wanayaona na wenyewe yanatokea kila mara kwanini wasiamue kupigania haki zao? Nadhani madereva wa wabunge wagome kuwaendesha hadi wawe na mikataba yenye kulinda maslahi yao na ya familia zao.
 
Kulingana na habari zilizotolewa, dreva wa Mwakyembe alipata majeraha kidogo, na Mheshimiwa mbunge, Dr. Mwakyembe aliumia kichwani.

Kwenye medical field, trauma yoyote inayohusisha kichwa siyo ya kudharau. Mgonjwa anatakiwa kuwa under observation kwa muda, na ikibidi kufanyiwa CT scan ya kichwa ili ku-rule out head concussion na formation ya epidural hematoma (mgando wa damu kichwani) ambazo zinaweza kuwa fatal.

Mfano mzuri ni wa actress Natasha Richardson ambaye alipata head injuries akajiona kuwa yupo salama na matokeo yake tunayajua... she is down, six feet under!

...Pangu pakavu, CT scanner ipo Muhimbili? (nikitia mchuzi)...ile mashine ya mionzi iliyoibiwa Ocean Rd Hosp ilipatikana?...
 
Ahsante dokta Pangu Pakavu. Unasema aliyeumia kichwa anatakiwa achikiwe zaidi. Yupi hapa achunguzwe?:

Hivi mna uhakika gani kuwa hakuchekewa "zaidi" na "zaidi" ina maana gani hasa ambayo haikufikiwa?
``alisema Kamanda Nyombi...kuwa wakati mbunge huyo amepelekwa Dar es Salaam, dereva wake aliyeumia kichwani na kukimbizwa pamoja naye katika hospitali ya mkoa wa Iringa, alitibiwa na kuruhusiwa.


kuumia kichwani peke yake haielezi ni kuumia kwa aina gani! Mtu ambaye amejikata kwenye paji la uso ameumia kichwani, aliyechubuka shavuni ameiumia kichwani, sasa kuumia kichwani kunawapa habari gani kuwa ameumia kwenye ubongo au zaidi? Ni madaktari ndiyo wanaamua the extent ya mtu kuumia haimuliwi kwa kusoma gazetini "kaumia kichwani" basi inaamani ameumia ndani ya kichwa!

Halafu aliyesema "kaumia kichwani" siyo daktari!! Unless polisi akisema kitu basi anakuwa amediagnose ugonjwa.


Hata hivyo, mganga mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, Oscar Gabone alisema Dk Mwakyembe aliumia taya na hali yake sio mbaya sana kwani mfupa wa taya haukuvunjika.`
`

Sasa hapa mtu mwenye fani ya tiba amesema aliumia taya! na amesema "hali yake siyo mbaya sana". Huyo ni mtaalamu anaposema hivi basi tunachukulia kwa uzito wake.

[/quote]alisema Mboka Mwambusi, ambaye alifika eneo hilo muda mfupi baada ya ajali hiyo na kumchukua mbunge huyo kwenye gari lake hadi Iringa..."Alipata michubuko kidogo..."
[/QUOTE]

Sasa huyo Mboka Mwambusi ni kama yule polisi, hana uwezo wa kutoa kauli inayohusu ugonjwa au tiba kana kwamba ni definitive. Kusema "alipata michubuko kidogo" ni kitu ambacho hata mtoto anaweza kukiona; lakini ni jinsi gani mtu ameumia ni madaktari na wataalamu wanaweza kusema. Wakati mwingine hata mgonjwa mwenyewe anaweza kufikiria amechubuka kidogo (kama mfano wa Pangu Pakavu hapo) lakini ni madaktari ndiyo wanaweza kusema ni kwa kiasi gani mtu ameumia.

Sasa, inakuwaje unayapa nguvu maneno ya watu wasio na utaalamu wa udaktari kinyume na maneno ya daktari!?

Hili bado silielewi.
 
Pole sana Dr. Mwakyembe na dereva wake. Mungu awajalie mpone haraka.
 
...Pangu pakavu, CT scanner ipo Muhimbili? (nikitia mchuzi)...ile mashine ya mionzi iliyoibiwa Ocean Rd Hosp ilipatikana?...

CT scanner imekuwepo Muhimbili kwa miaka kadhaa sasa. Whether inafanya kazi au la, hilo sijui. Habari nilizopata miezi kadhaa iliyopita, Muhimbili walikuwa wanajiimarisha baada ya ku-install machine ya uchunguzi ya Magnetic Resonance Imaging (MRI), ambayo ni advanced kwenye diagnosis ya matatizo ambayo inaweza kuwa vigumu kuyatambua kwa CT scan.

Whether hizo machine zinafanya kazi, sijui!
 
Nimeshaona mara nyingi tu TZ, kigogo anajichana huku dereva anahangaika na njaa kwenye gari, kisha wanaondoka safari ya mwendo. Looh! kutembea na dereva mwenye mjaa mbona ni kujitakia balaa? Kuna mambo mengi sana hayako sawa huko nyumbani!

Those are the field slaves, wanajitegemea na njaa zao. Lakini kuna wanaopewa chakula.

Ukimsubiri bosi atoke ndani unaweza na we ukaletewa chakula hapo nje ukala kala. Here's the catch though:

Ukigusa hicho chakula utashinda na hiyo familia from can't see in the morning to can't see at night. Saiti, shule, saluni, kanisani, kazini, kilabuni, Kibaha, mkutanoni, msikitini, mjini, mkesha, nyuma ndogo, nyumba ya Masaki, nyumba ya Mbezi, harusi, hospitali, hoi! Huendi kwa wanao, huendi break, huendi kwa mkeo, huna maisha.

Mtanzania ushaziona hizo? Ukipata ajali, dereva kivyako.
 
Back
Top Bottom