Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Sawa mzee wa bia nimekupata. Ila nafikiri walifanya makosa kupanua umbali kidogo namna hiyo hayo mabega. Ila kama zamani ilikuwa ni mita 3, kweli ilikuwa ni kidogo sana. Ila sema miaka hiyo hata magari yalikuwa na speed kidogo na siyo ya siku hizi.

NB: Nimeangalia lile gari na nimegundua kitu kimoja. Hata kama liligongwa ili lipinduke, huwezi kusema kuwa halina mikwaruzo. Sababu hasa ni hii kwamba, ili liangukie upande wa kushoto, inabidi uligonge kwa nyuma upande wa kushoto, na hapo husababisha gari kubadili mwelekeo na kuanza kwenda kushoto zaidi na hadi linakuja anguka kama kilichotokea. Sasa ili kujua kama maelezo ya driver ni kweli au laa, inabidi kuangalia upande wa kushoto mwa hilo gari kama halina alama zozote za kuonyesha kuwa lilikatwa mtama.
 
Hili la kupigwa mtama naona sio sahihi, ina maana hilo lori lilikuwa speed kubwa mno kiasi la kulifikia shangingi ambalo lilikuwa linaovatake lori lingine na kulipiga mtama?
 
Hili la kupigwa mtama naona sio sahihi, ina maana hilo lori lilikuwa speed kubwa mno kiasi la kulifikia shangingi ambalo lilikuwa linaovatake lori lingine na kulipiga mtama?

Unazikumbuka zile roli za NISSAN? Ziliuwa sana watu barabara ya Mandela/port Acc. Kuna roli zina uwezo wake wa speed Kibunango.
Kupigwa mtama inawezekana ila tu hata mie siamini kama kweli Shangingi likifukuzwa na roli, roli litapata kitu. Labda kama jamaa alikuwa anawanyemelea kimya kimya wakipunguza speed. Kama walikuwa wanakwenda 90km/hr na roli linakwenda 120km/hr, hilo lawezekana.
 
Mungu yuko pamoja nawe mpiganaji Dr. Mwakyembe.

Miaka 25 iliyopita, tulimpoteza mpiganaji Moringe Sokoine katika mazingira kama haya haya; tukaambiwa ni ajali ya kawaida tu.

Tuwe macho kwani Mapambano ndio kwanza yameanza!
 
Unazikumbuka zile roli za NISSAN? Ziliuwa sana watu barabara ya Mandela/port Acc. Kuna roli zina uwezo wake wa speed Kibunango.
Kupigwa mtama inawezekana ila tu hata mie siamini kama kweli Shangingi likifukuzwa na roli, roli litapata kitu. Labda kama jamaa alikuwa anawanyemelea kimya kimya wakipunguza speed. Kama walikuwa wanakwenda 90km/hr na roli linakwenda 120km/hr, hilo lawezekana.
Nakumbuka sana zile Nissan, NMC walikuwa nazo zikibeba mahindi to Big 4. Kuna kipindi zilijulikana kama kiboko ya Wabena, baada ya Nissan moja kuua wabena 40 katika moja ya ajali mbaya sana tokea kufunguliwa kwa barabara ya Makambako Songea katika kiwango cha lami.

Hata hivyo kipindi cha Nissan hizo Tanzania ilikuwa na 109 Land Rover kibao, Hivyo Nissan zile ziliweza kuzinyanyasa sana 109 na aina zingine za magari makubwa kwa madogo.
 
mimi mtu anifafanulie tu.. ni jinsi gani tairi linachomoka kwa sababu gari limepita kwenye shimo... maana ingekuwa hii ni kweli at face value nadhani ajali zingekuwa nyingi sana kuliko ilivyo sasa.. tairi lingepata pancha ningeelewa sana.. Ni kwa namna gani tairi linachomoka baada ya kupita kwenye shimo maana ukiniuliza mimi kuna vitu zaidi 100 ambavyo vingeweza kutokea kwenye gari, axel, steering rod n.k lakini hadi kuchomoka tairi...
 
A new story:

[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]•[/FONT]Mwakyembe apata ajali (Uhuru) NA ANITA BOMA, IRINGA

MBUNGE wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM), amenusurika kifo katika ajali ya barabarani iliyotokea jana asubuhi katika eneo la Ihemi, Iringa Vijijini.

Ajali hiyo iliyotokea saa 1.10 asuhuhi, pia ilimhusisha dereva wake Joseph Msuya (36), ambapo gari walilokuwa wakisafiria kutoka Mbeya kuelekea Dar es Salaam liligonga mti na kupinduka.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Advocate Nyombi, alisema Dk. Mwakyembe alipata ajali akiwa kwenye gari lake lenye namba za usajili T 362 ACH, Toyota Land Cruiser.

Kwa mujibu wa Kamanda Nyombi, chanzo cha ajali hiyo ni dereva kutaka kulipita lori, ambapo ghafla gurudumu la mbele lilitumbukia kwenye shimo lililokwa katikati ya barabara, hivyo tairi kuchomoka na baadaye gari kuacha njia na kugonga mti kabla ya kupinduka. (gademu!! we could call this the Unified Theory of all Tanzanian Accidents! M.M.)

Baada ya ajali hiyo, Dk. Mwakyembe na Msuya walipelekwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa kwa matibabu.

Nyombi alisema Msuya alipata majeraha kichwani, ambapo alitibiwa na kuruhusiwa.

Akizungumzia hali ya Dk. Mwakyembe jana mchana kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Mganga Mkuu Mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Iringa, Dk. Oscar Gabon, alisema hali yake si mbaya kwani alikuwa akizungumza.

Dk. Gabon alisema Dk. Mwakyembe amepata michubuko usoni na ameumia taya la upande wa kushoto. (kuna mataya mangapi? M.M.)

Wakati huo huo, Hamis Shimye anaripoti kuwa, madaktari katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), baada ya kumuhudumia Dk. Mwakyembe jana jioni, walishauri ahamishiwe hospitali ya Regency Mikocheni kwa matibabu zaidi, ushauri ambao ulitekelezwa.

Katibu wa Bunge Dk. Thomas Kashilillah, alithibitisha kuhamishwa kwa Dk. Mwakyembe.

Alisema Waziri Mkuu Mizengo Pinda, leo atakwenda kumjulia hali Dk. Mwakyembe na kwamba, alishindwa kufanya hivyo jana ili kutoa nafasi kwa madaktari kufanya kazi yao.

Akizungumza katika hospitali ya MOI, mke wa Dk. Mwakyembe, Lina, alisema hali ya mumewe jana jioni ilikuwa ikiendelea vizuri tofauti na ilivyokuwa muda mfupi baada ya ajali.

“Namshukuru Mungu, hali yake inaridhisha, anaongea ni jambo la kutia moyo,” alisema Lina.

Kwa upande wake, Dk. Francis Nyabusani wa hospitali ya mkoa wa Iringa, aliyefuatana na Dk. Mwakyembe kutoka Iringa, alisema hali yake ilikuwa mbaya alipompokea baada ya kupata ajali. (pamoja na hayo angesimama na kuonesha uongozi! according to somebody..)

Mbunge wa Viti Maalumu, Hilda Ngoye, alisema amepata mshtuko mkubwa baada ya kusikia habari za kutokea kwa ajli hiyo na kuwa, ni jambo la kumshukuru Mungu kuwa Dk. Mwakyembe ametoka akiwa hai.

Kwa upande wake, mfanyabiashara Reginald Mengi, alisema anaomba Mungu amsaidie Dk. Mwakyembe apone haraka ili aendelee na kazi za ujenzi wa taifa.

Wabunge wengine waliofika hospitalini hapo ni Wilson Masilingi, Victor Mwambalaswa, Lucas Selelii, Beatrice Shellukindo, Kilontsi Mporogomyi na Aloyce Kimaro.

Dk. Mwakyembe alihamishiwa Dar es Salaam kutoka Iringa alikopata ajali kwa ndege ya kampuni ya TanzanAir iliyokodiwa na Bunge, ambayo ilitua Dar es Salaam saa 9.50 alasiri.

Uwanjani hapo kulikuwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge ambao waliongozana na Dk. Mwakyembe aliyekuwa kwenye gari la wagonjwa la kampuni ya Ultimate Security hadi Muhimbili alikofika saa 10.20.

Msafara wa magari zaidi ya 30 yakiongozwa na lile la polisi wa TAZARA yalimsindikiza Dk. Mwakyembe kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere hadi hospitali ya Muhimbili, ambako pia kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakimwangalia akiingizwa MOI.

Wakati huo huo, Estherina Kilasi (Mbarali– CCM) pia alipata ajali juzi, mkoani Morogoro na hali yake inaendelea vizuri.

Katibu wa Bunge Dk. Kashilillah alithibitisha mbunge huyo kupata ajali, lakini hakuweza kueleza kwa undani kuhusu tukio hilo.

Hata hivyo, habari zilisema baada ya mbunge huyo kupata ajali, vibaka walifika eneo la tukio na kumpora mbunge huyo vitu vyote.

Mbali na kupora, vibaka hao wanadaiwa kumpiga na kumjeruhi dereva wa mbunge huyo, ili kufanikisha uporaji. (hii nayo mbona hatukusikia, btw sikujua kuna mbunge anaitwa Kilasi! M.M)
 
mimi mtu anifafanulie tu.. ni jinsi gani tairi linachomoka kwa sababu gari limepita kwenye shimo... maana ingekuwa hii ni kweli at face value nadhani ajali zingekuwa nyingi sana kuliko ilivyo sasa.. tairi lingepata pancha ningeelewa sana.. Ni kwa namna gani tairi linachomoka baada ya kupita kwenye shimo maana ukiniuliza mimi kuna vitu zaidi 100 ambavyo vingeweza kutokea kwenye gari, axel, steering rod n.k lakini hadi kuchomoka tairi...

Kuchomoka tairi ni ktu ambacho mimi nimekishuhudia kikitokea bila hata ya pothole sasa sijui hapo chaajabu nini.. At high speed tairi ikichomoka lazima mle udongo kidogo.. gari inakuwa kama ina rabis... Any good driver will concur when I say that kuchomoka tairi is simply a matter of loose nuts on the wheel.. au saanyingine zinalika zile and then what happens happens. That is what I have seen and had happen to me in my years on the road. As for Mwakiembe sijui.. hope he recovers soon.
 
Waandishi wetu Iringa na Dar es Salaam

MBUNGE wa Jimbo la Kyela kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dkt. Harrison Mwakyembe (CCM),amenusurika kufa baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Mbeya kwenda Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka eneo la Ifunda mkoani Iringa.

Ajali hiyo ilitokea jana saa 1.10 asubuhi baada ya gari hilo Toyota Land Cruiser,namba T362ACH, kuchomoka tairi ya mbele likiwa kwenye mteremko wa mlima Ihemi, kuacha njia na kupinduka porini.

Dkt.Mwakyembe alikimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa kwa matibabu na kulazwa wodi namba tano ya hosptali hiyo kabla ya kusafirishwa jana mchana kwa ndege kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, Dkt. Oscar Gabone alisema hali ya Mbunge huyo inaendelea vizuri, ameumia taya baada ya kujibamiza, dereva wake alitibiwa na kuruhusiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Bw. Advocate Nyombi alithibitisha kutokea ajali hiyo na kueleza kuwa chanzo chake ni gari hilo kuingia kwenye shimo lililokuwa barabarani na kusababisha tairi la mbele kulia kuchomoka na kupoteza mwelekeo.Gari hilo lilikuwa likiendeshwa na Bw. Joseph Msuya (30).

Alieleza kuwa baada ya kuchomoka tairi, liliyumba upande wa kushoto wa barabara, kuacha njia na kugonga mti kabla ya kupinduka.

Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Isaya Ng'ande,makazi wa Ifunda, tairi hiyo ilichomoka wakati dereva wa Mbunge huyo akijaribu kuyapita magari mawili makubwa na kukuta shimo lilisaababisha kuchomoka tairi hiyo.

Kamanda Nyombi aliwaambia waandishi wa habari kuwa, Dkt. Mwakyembe aliondoka juzi jioni saa mbili usiku jimboni kwake Kyela na kulala Makambako, Njombe kabla ya kuendelea na safari jana asubuhi.

Wakati huo huo waandishi wetu wanaripoti kuwa ndege iliyomchukua Dkt. Mwakyembe, iliwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana saa 10 jioni. Ndege hiyo ndogo yenye namba 5H TZT inayomilikiwa na Shirika la Ndege ya Tanzania(ATC) ilitua huku mamia ya wanasiasa ndugu jamaa na marafiki wakisubiri kumpokea mgonjwa huyo.

Akizungumza na Majira uwanjani hapo, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dkt. Thomas Kashililah alisema kuwa Bunge limepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali hiyo na linashughulikia matibabu ambapo wanatarajia atafanyiwa uchunguzi katika Taasisi ya mifupa Muhimbili (MOI) na kama itabainika kuwa ameumia zaidi, atapelekwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi.

''Sisi tunasubiri taarifa za madaktari watakavyoshauriana kutegemea na hali yake kama atatibiwa hapa au nje watatueleza lakini kwa sasa hatuna cha kuzungumza zaidi ya kumwombea apone haraka,'' alisema, Dkt. Kashililah.

Naye Mbunge wa Jimbo la Lupa mkoani Mbeya, Bw. Victor Mwambalaswa ambaye ni rafiki wa karibu wa Dkt. Mwakyembe, alisema wananchi wanapaswa kumwombea Mbunge huyo ili apate nafuu haraka na aendeleze harakati zake za kupinga ufisadi.

"Dkt. Mwakyembe ni mtu niliye karibu naye sana, nimepokea taarifa hizi kwa majonzi, na kwa sasa anaongea kwa taabu lakini kikubwa tunatoa mwito kwa Watanzania wote tumuombee ili apone haraka kwani karibuni tutaanza vikao vya Bunge na amekuwa kinara wa kupinga ufisadi" alisema Bw. Mwambalaswa.

Aidha Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Bw. Nape Nnauye alisema kuwa kuna haja ya vyombo vya usalama kuchunguza kwa makini ajali hiyo ili Watanzania waweze kuelewa chanzo cha ajali hiyo.

Alisema wiki ijayo Mkutano wa Bunge unaanza na yeye ni mtu muhimu katika vikao hivyo hasa katika Bunge la Bajeti, kumkosa ni hasara kubwa kwani ni mpigania haki za wanyonge.

''Vyombo vya usalama vichunguze kama kuna njama zozote zimefanyika ibainike ili sheria ichukue mkondo wake'' alisema, Bw. Nape.

Ajali ya Dkt. Mwakyembe ambaye amekuwa kinara wa kundi la wabunge walio mstari wa mbele katika mapamabano dhidi ya ufisadi, imepokewa kwa hisia tofauti huu baadhi ya wanasiasa wakidai imekuja wakati mbaya karibu na Mkutano wa Bunge la Bajeti, unaotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao mjini Dodoma ambapo mwanasiasa huyo amekuwa kivutio kutokana na ujasiri wake.

Chati ya mwanasiasa huyo, msomi wa sheria, ilipanda zaidi pale alipoteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mchakato wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura uliyoipa ushindi kampuni ya Richmond.

Taarifa ya Tume hiyo iliyowasilishwa Bungeni Februari 6 mwaka jana, ilipendekeza kuchukuliwa hatua kali wote waliohusika kwa njia moja ama nyingine na suala hilo. Katika sakata hilo, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Nizir Karamagi na mwenzake wa Afrika Mashariki, Dkt. Ibrahim Msabaha waliachia ngazi,sambamba na aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa ambaye Tume hiyo ilimtaka apime.

Aidha kamati hiyo iliitaka Serikali kuacha utaratibu wa kutumia mawakala katika ununuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme.

Mbali ya ripoti kumpa umaarufu, ilimjengea maadui wengi ambao kwa njia moja ama nyingine waliathirika.Hata hivyo Dkt. Mwakyembe ameendelea kubainisha waziwazi kuwa ataendeleza mapambano dhidi ya vitendo vyote vya ufisadi na kamwe hatarudi nyuma.

Gazeti hili Jumatatu iliyopita, lilichapisha habari ikieleza kundi la mafisadi kutenga kiasi cha sh. bilioni 2.7 kuwashughulika wabunge wote wanaoonesha kimbelembele kupinga ufisadi kwa kuhakikisha hawarudi tena bungeni baada ya uchaguzi mkuu mwakani.

Dkt. Mwakyembe alitajwa kuwa mmoja wa wabunge walio katika kundi la kwanza la utekelezaji wa mkakati huo, wengine waliotajwa kwenye kundi hilo ni pamoja na Spika wa Bunge, Bw.Samuel Sitta (Urambo Mashariki), Bw. William Shellukindo (Bumbuli) pamoja na Bi. Stella Manyanya, (Viti Maalum).

Kundi la pili ni wabunge wanaoonesha waziwazi kuchukizwa na vitendo vya ufisadi na kutoa kauli nzito kukemea tabia hiyo chafu hadharani bila woga. Hao ni pamoja na Bi. Anne Kilango Malecela (Same Mashariki), Bw. Lucas Selelii (Nzega) na Bw.Christopher Ole-Sendeka (Simanjirao).

Kundi la tatu kushughulikiwa ni la wabunge wanaonekana kuwa karibu na kundi la kwanza na kuonekana kupinga ufisadi kwa kuunga mkono hoja za makundi hayo mawili na kushauriana kwa karibu mambo mbalimbali, hawa ni pamoja na Bi. Hilda Ngoye (Viti Maalum), Bw. Godfrey Zambi (Mbozi Mashariki), Prof. Mark Mwandosya (Rungwe Mashariki), Bw. Victor Mwambalaswa (Lupa) pamoja na Bw. Benson Mpesya (Mbeya) mjini.

Mbali na wabunge, wapo wengine wasiopungua sita wanaodaiwa kuwa mstari wa mbele kukemea vitendo vya ufisadi bila woga. Miongoni mwao ni Bw.Fredy Mpendazoe (Kishapu), Bw.James Lembeli(Kahama) na Bw. Aloyce Kimaro(Vunjo), ambao wote walengwa wa hasira ya mafisadi.

Habari hizo zilisema majimbo hayo tayari yametengewa milioni 400/- kila moja kwa ajili ya utekelezaji wa mkakati huo na kwamba mgawo wa kwanza wa fedha hizo tayari umetua jimboni Kyela ambapo kata moja imepewa sh. milioni 5.

Hivi karibuni, Dkt. Mwakyembe na Mwenyekiti wa CCM wilayani Kyela, Bw.Japhet Mwakasumi walituhumiwa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya hiyo kuwa ni vinara wa kukigawa chama hicho katika makundi, hali iliyosababisha baadhi ya makatibu kata kuwashambulia na kuwapiga viongozi wa chama wilayani humo.

Katika kikao hicho kilichofanyika Jumapili iliyopita, wajumbe wengi walimshushia makombora, Dkt. Mwakyembe na kudai kuwa tangu awe Mbunge wa jimbo hilo, ametengeneza makundi ndani ya chama huku akidaiwa 'kummiliki' Mwenyekiti wa chama wa wilaya ambaye ameonekana kuyumba katika
maamuzi mbalimbali.

Walisema kufuatia hali hiyo, ndani ya chama hicho, kumekuwepo kutokuelewana na kujengeka
uhasama mkubwa jambo linalowafanya baadhi yao kudai wananyanyaswa
na hawana haki hivyo kuamua kudai haki hiyo kwa kutumia nguvu,
kama walivyofanya viongozi hao wa kata.

Mmoja wa wajumbe hao, Bw.Christopher Mulemwah ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ipinda
alisema, Kamati ya siasa ilikurupuka kufikia uamuzi wa kuwavua uanachama
makatibu kata hao badala ya kukaa na kutafakari chanzo cha viongozi hao kuchukua
uamuzi kuwapiga viongozi wao wa wilaya

Dkt.Mwakyembe kwa upande wake alijitetea na kupinga tuhuma dhidi yake huku akieleza
kuwa makundi yanayoendelea ndani ya chama hicho wilayani Kyela yanazorotesha maendeleo. Alisema
kana kwamba haitoshi, mgawanyiko huko umewakumba hata wakazi wa
Kyela waishio Dar es Salaam.

Alisema binafsi hapendi kuona viongozi hao wanafikishwa mahakamani na kufungwa
bali kilichopo ni chama kuchagua wazee wenye busara kwenda kuwaombea radhi
makatibu kata hao kwa viongozi waliopigwa ili mambo hayo
yaishe

Hata hivyo Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya wilayani, Kyela juzi kilitengua adhabu
ya kufutwa uanachama kwa makatibu kata hao.

Maoni:
Kinyambiss.. sisemi matairi hayachomoki.. point ndiyo hiyo uliyoisema loose nuts.. kabla mtu yeyote hajaanza safari ndefu kuna vitu unavihakikisha vipo katika hali nzuri.. miongoni mwa vya muhimu ni hewa kwenye matairi, wheel alignment na balancing na kuhakikisha kuwa hakuna loose nuts. Kama ulivyosema pia ni kama kitu cha kawaida sana kitu ambacho siamini ni kweli kwani ingekuwa ni cha kawaida hivyo ajali za kuchomoka matairi zingekuwa ni nyingi mno..
 
mimi mtu anifafanulie tu.. ni jinsi gani tairi linachomoka kwa sababu gari limepita kwenye shimo... maana ingekuwa hii ni kweli at face value nadhani ajali zingekuwa nyingi sana kuliko ilivyo sasa.. tairi lingepata pancha ningeelewa sana.. Ni kwa namna gani tairi linachomoka baada ya kupita kwenye shimo maana ukiniuliza mimi kuna vitu zaidi 100 ambavyo vingeweza kutokea kwenye gari, axel, steering rod n.k lakini hadi kuchomoka tairi...

Mwanakijiji yule dereva aliyegonga gari la Salome Mbatia alipatikana? Vipi Dereva wa ile Bajaji iliyokuwa imewabeba marehemu wale waliouawa na gari la Chenge umewahi kusikia jina lake alikuwa anaitwa nani. Nasikia gari lililosababisha ajali ya Mwakiyembe lilikuwa halina namba,dereva wake naye kakimbia? Hawa madereva huwa ni kina nani?
 
Kigarama.. umegusa vitu ambavyo watu hawajavigusa:

Hilo lori lililokuwa linawapita/kuwagonga linajulikana au ilikuwa ni 'hit and run'?

sasa hivi I'm more concerned na hali ya Mwakyembe kwa sababu anaweza kuwa amejeruhiwa zaidi ya tunavyofikiria. Sijaona wakisema kama anaweza kusimama au kama ana movement kwenye lower body. Sijui ni 'taya la kushoto" tu ndio linamfanya aendelee kukaa hospitali....!
 
Sipendi speculation,lakini kuna maswali muhimu ya kujiuliza kabla hatujaconclude kuhusiana na ajali hii.
Dereva anadai kuna gari lililokuwa likiwafuata nyuma kwa mwendo mkali na yeye alijaribu kulikwepa na kwamba gari hilo liliwagonga kwa nyuma...Halafu kuna story ambayo polisi wanaipenda zaidi,kuwa aliovertake na kukutana na shimo,na mara baada ya hapo tairi ikachomoka na gari kuacha njia kwenda kuparamia mti.. Hatuajasikia bado upande wa Mwakyembe,Mungu ampe uzima ili aweze kuongea sawia kwani imani ni kubwa kuwa hatoficha lolote.
Swali kubwa na la msingi;je ni kwanini polisi watoe taarifa tofauti na ya dereva? Nani ni mkweli? Dereva alikuwa akiovertake,akifuatwa na gari jingine nyuma ama both?
 
Mwakyembe ataweza kuongea baada ya kupata nafuu, atatoa upande wake wa story. Kama alikuwa hajasinzia au kulala atakuwa alishuhudia picha nzima. Anaujua ukweli.

Mwanakijiji yule dereva aliyegonga gari la Salome Mbatia alipatikana? Vipi Dereva wa ile Bajaji iliyokuwa imewabeba marehemu wale waliouawa na gari la Chenge umewahi kusikia jina lake alikuwa anaitwa nani. Nasikia gari lililosababisha ajali ya Mwakiyembe lilikuwa halina namba,dereva wake naye kakimbia? Hawa madereva huwa ni kina nani?

Kigarama unajua huwa kuna coincidences,hilo lipo,kwamba muda huu upo kwenye eneo hili na jambo hili linatokea,kwasababu uko mahali pale.
Lakini coincidences ambazo zinalead kwenye upotevu wa ushahidi ni za kutupiwa macho,kwamba gari lisilokuwa na namba ni coincidence?
 
Last edited:
Mwakyembe ataweza kuongea baada ya kupata nafuu, atatoa upande wake wa story. Kama alikuwa hajasinzia au kulala atakuwa alishuhudia picha nzima. Anaujua ukweli.

na kama alikuwa amesinzia? swali litakuwa ni kwanini alikuwa amesinzia wakati dereva wake yuko macho?
 
Mwakyembe ataweza kuongea baada ya kupata nafuu, atatoa upande wake wa story. Kama alikuwa hajasinzia au kulala atakuwa alishuhudia picha nzima. Anaujua ukweli.

Sawa kabisa! La kuongezea hapo ni kwamba walishalala huko makambako na ilikuwa ni asubuhi ya saa moja baada ya kudamka....Nadhani walilala Makambako ili kuondoa uchovu na risks za kuendesha gari usiku. Inawezekana alisinzia ama kulala kama unavyohisi,lakini kwamba walipumzika kwasababu ya safari ya kesho yake hilo liko wazi,kwamba hakuutumia muda huo kupumzika,hilo sifahamu...Na hata Mwakyembe akisema wewe utaamini? Mbona alisema RA ni fisadi na hukuamini?
Lets wait and see,maana hata GT naye eti anapinga ufisadi kwa kuonyesha picha za wanafunzi wanaokaa chini na wakati huo huo anasema kelele za ufisadi ni enough,yani ni sawa na kujali kuwa huyu kauwawa lakini mwenye bunduki iliyouwa hana kesi ya kujibu,kudai kuwa anajali shida ya wanafunzi na wakati shida hiyo imesababishwa na mafisadi anaowakingia kifua ni undumilakuwili wa ajabu ambao ni watu fyatu tu wanaweza ku ubuy.
 
mimi mtu anifafanulie tu.. ni jinsi gani tairi linachomoka kwa sababu gari limepita kwenye shimo... maana ingekuwa hii ni kweli at face value nadhani ajali zingekuwa nyingi sana kuliko ilivyo sasa.. tairi lingepata pancha ningeelewa sana.. Ni kwa namna gani tairi linachomoka baada ya kupita kwenye shimo maana ukiniuliza mimi kuna vitu zaidi 100 ambavyo vingeweza kutokea kwenye gari, axel, steering rod n.k lakini hadi kuchomoka tairi...
Baada yakumsikiliza Mh na driver wake wakieleza jinsi walivyopata ajali ni very possible ajali ilipangwa. Inawezekana tairi ililegezwa nuts usiku wakati wako Makambako. Kama ni kweli kuna mikono ya watu WASHINDWE KATIKA JINA LA YESU NA WALEGEE
 
na kama alikuwa amesinzia? swali litakuwa ni kwanini alikuwa amesinzia wakati dereva wake yuko macho?

Mheshimiwa Mwakyembe ameweza kuongea leo, yeye amesema amemwachia Mungu kwa maana yeye ni Mkristo na kama ilikuwa ni ajali ya kawaida basi anamwachia Mungu na kama kuna mkono wa mtu yaani hiyo ajali ilikuwa planted basi anamshitakia Mungu, ameweza kudeclair yeye mwenyewe kuwa gari lake liligongwa kwa nyuma ingawa anasema liligongwa kidogo kwenye taa ya nyuma so likaongeza motion ya gari lae na dereva waka akapanic baada ya kuona hawezi kulimudu ndo akalitoa nje ya road reserve sasa hapa nafurahi mno kusikia yeye mwenyewe amesema hivyo sijui kamanda Nyombi ataendelea kushikilia msimamo wake kuwa tairi imechomoka dah... Namuamini sana huyu mtu maana anasimama kwenye ukweli daima... Go Mwakyembe Gooo tupo nyuma yako
 
na kama alikuwa amesinzia? swali litakuwa ni kwanini alikuwa amesinzia wakati dereva wake yuko macho?

Mwakyembe apone haraka labda atafanya interview na KLH news au ataita press conference kueleza kilichojiri, mazingira ya ajali yalikuwaje, na kuprove au kudisapprove conspiracy theories wafuasi wake wateule.

Ashukuriwe baba wa mbinguni kwa kumnusuru kwenye hii ajali.
 
Baada yakumsikiliza Mh na driver wake wakieleza jinsi walivyopata ajali ni very possible ajali ilipangwa. Inawezekana tairi ililegezwa nuts usiku wakati wako Makambako. Kama ni kweli kuna mikono ya watu WASHINDWE KATIKA JINA LA YESU NA WALEGEE

Je Mh Mwakyembe naye keshaongea? Aliyoyasema ni sawa na dereva? Tuwekee hapa maelezo ya alichosema kama ukiweza. Maana kama unafutilia mjadala huu utaweza kuona kuwa tunasubiri Mwakyembe apate nafuu ili na yeye aseme yaliyowasibu.
 
Back
Top Bottom