Kuchomoka tairi ni ktu ambacho mimi nimekishuhudia kikitokea bila hata ya pothole sasa sijui hapo chaajabu nini.. At high speed tairi ikichomoka lazima mle udongo kidogo.. gari inakuwa kama ina rabis... Any good driver will concur when I say that kuchomoka tairi is simply a matter of loose nuts on the wheel.. au saanyingine zinalika zile and then what happens happens. That is what I have seen and had happen to me in my years on the road. As for Mwakiembe sijui.. hope he recovers soon.
Waandishi wetu Iringa na Dar es Salaam
MBUNGE wa Jimbo la Kyela kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dkt. Harrison Mwakyembe (CCM),amenusurika kufa baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Mbeya kwenda Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka eneo la Ifunda mkoani Iringa.
Ajali hiyo ilitokea jana saa 1.10 asubuhi baada ya gari hilo Toyota Land Cruiser,namba T362ACH, kuchomoka tairi ya mbele likiwa kwenye mteremko wa mlima Ihemi, kuacha njia na kupinduka porini.
Dkt.Mwakyembe alikimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa kwa matibabu na kulazwa wodi namba tano ya hosptali hiyo kabla ya kusafirishwa jana mchana kwa ndege kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, Dkt. Oscar Gabone alisema hali ya Mbunge huyo inaendelea vizuri, ameumia taya baada ya kujibamiza, dereva wake alitibiwa na kuruhusiwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Bw. Advocate Nyombi alithibitisha kutokea ajali hiyo na kueleza kuwa chanzo chake ni gari hilo kuingia kwenye shimo lililokuwa barabarani na kusababisha tairi la mbele kulia kuchomoka na kupoteza mwelekeo.Gari hilo lilikuwa likiendeshwa na Bw. Joseph Msuya (30).
Alieleza kuwa baada ya kuchomoka tairi, liliyumba upande wa kushoto wa barabara, kuacha njia na kugonga mti kabla ya kupinduka.
Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Isaya Ng'ande,makazi wa Ifunda, tairi hiyo ilichomoka wakati dereva wa Mbunge huyo akijaribu kuyapita magari mawili makubwa na kukuta shimo lilisaababisha kuchomoka tairi hiyo.
Kamanda Nyombi aliwaambia waandishi wa habari kuwa, Dkt. Mwakyembe aliondoka juzi jioni saa mbili usiku jimboni kwake Kyela na kulala Makambako, Njombe kabla ya kuendelea na safari jana asubuhi.
Wakati huo huo waandishi wetu wanaripoti kuwa ndege iliyomchukua Dkt. Mwakyembe, iliwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana saa 10 jioni. Ndege hiyo ndogo yenye namba 5H TZT inayomilikiwa na Shirika la Ndege ya Tanzania(ATC) ilitua huku mamia ya wanasiasa ndugu jamaa na marafiki wakisubiri kumpokea mgonjwa huyo.
Akizungumza na Majira uwanjani hapo, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dkt. Thomas Kashililah alisema kuwa Bunge limepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali hiyo na linashughulikia matibabu ambapo wanatarajia atafanyiwa uchunguzi katika Taasisi ya mifupa Muhimbili (MOI) na kama itabainika kuwa ameumia zaidi, atapelekwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi.
''Sisi tunasubiri taarifa za madaktari watakavyoshauriana kutegemea na hali yake kama atatibiwa hapa au nje watatueleza lakini kwa sasa hatuna cha kuzungumza zaidi ya kumwombea apone haraka,'' alisema, Dkt. Kashililah.
Naye Mbunge wa Jimbo la Lupa mkoani Mbeya, Bw. Victor Mwambalaswa ambaye ni rafiki wa karibu wa Dkt. Mwakyembe, alisema wananchi wanapaswa kumwombea Mbunge huyo ili apate nafuu haraka na aendeleze harakati zake za kupinga ufisadi.
"Dkt. Mwakyembe ni mtu niliye karibu naye sana, nimepokea taarifa hizi kwa majonzi, na kwa sasa anaongea kwa taabu lakini kikubwa tunatoa mwito kwa Watanzania wote tumuombee ili apone haraka kwani karibuni tutaanza vikao vya Bunge na amekuwa kinara wa kupinga ufisadi" alisema Bw. Mwambalaswa.
Aidha Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Bw. Nape Nnauye alisema kuwa kuna haja ya vyombo vya usalama kuchunguza kwa makini ajali hiyo ili Watanzania waweze kuelewa chanzo cha ajali hiyo.
Alisema wiki ijayo Mkutano wa Bunge unaanza na yeye ni mtu muhimu katika vikao hivyo hasa katika Bunge la Bajeti, kumkosa ni hasara kubwa kwani ni mpigania haki za wanyonge.
''Vyombo vya usalama vichunguze kama kuna njama zozote zimefanyika ibainike ili sheria ichukue mkondo wake'' alisema, Bw. Nape.
Ajali ya Dkt. Mwakyembe ambaye amekuwa kinara wa kundi la wabunge walio mstari wa mbele katika mapamabano dhidi ya ufisadi, imepokewa kwa hisia tofauti huu baadhi ya wanasiasa wakidai imekuja wakati mbaya karibu na Mkutano wa Bunge la Bajeti, unaotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao mjini Dodoma ambapo mwanasiasa huyo amekuwa kivutio kutokana na ujasiri wake.
Chati ya mwanasiasa huyo, msomi wa sheria, ilipanda zaidi pale alipoteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mchakato wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura uliyoipa ushindi kampuni ya Richmond.
Taarifa ya Tume hiyo iliyowasilishwa Bungeni Februari 6 mwaka jana, ilipendekeza kuchukuliwa hatua kali wote waliohusika kwa njia moja ama nyingine na suala hilo. Katika sakata hilo, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Nizir Karamagi na mwenzake wa Afrika Mashariki, Dkt. Ibrahim Msabaha waliachia ngazi,sambamba na aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa ambaye Tume hiyo ilimtaka apime.
Aidha kamati hiyo iliitaka Serikali kuacha utaratibu wa kutumia mawakala katika ununuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme.
Mbali ya ripoti kumpa umaarufu, ilimjengea maadui wengi ambao kwa njia moja ama nyingine waliathirika.Hata hivyo Dkt. Mwakyembe ameendelea kubainisha waziwazi kuwa ataendeleza mapambano dhidi ya vitendo vyote vya ufisadi na kamwe hatarudi nyuma.
Gazeti hili Jumatatu iliyopita, lilichapisha habari ikieleza kundi la mafisadi kutenga kiasi cha sh. bilioni 2.7 kuwashughulika wabunge wote wanaoonesha kimbelembele kupinga ufisadi kwa kuhakikisha hawarudi tena bungeni baada ya uchaguzi mkuu mwakani.
Dkt. Mwakyembe alitajwa kuwa mmoja wa wabunge walio katika kundi la kwanza la utekelezaji wa mkakati huo, wengine waliotajwa kwenye kundi hilo ni pamoja na Spika wa Bunge, Bw.Samuel Sitta (Urambo Mashariki), Bw. William Shellukindo (Bumbuli) pamoja na Bi. Stella Manyanya, (Viti Maalum).
Kundi la pili ni wabunge wanaoonesha waziwazi kuchukizwa na vitendo vya ufisadi na kutoa kauli nzito kukemea tabia hiyo chafu hadharani bila woga. Hao ni pamoja na Bi. Anne Kilango Malecela (Same Mashariki), Bw. Lucas Selelii (Nzega) na Bw.Christopher Ole-Sendeka (Simanjirao).
Kundi la tatu kushughulikiwa ni la wabunge wanaonekana kuwa karibu na kundi la kwanza na kuonekana kupinga ufisadi kwa kuunga mkono hoja za makundi hayo mawili na kushauriana kwa karibu mambo mbalimbali, hawa ni pamoja na Bi. Hilda Ngoye (Viti Maalum), Bw. Godfrey Zambi (Mbozi Mashariki), Prof. Mark Mwandosya (Rungwe Mashariki), Bw. Victor Mwambalaswa (Lupa) pamoja na Bw. Benson Mpesya (Mbeya) mjini.
Mbali na wabunge, wapo wengine wasiopungua sita wanaodaiwa kuwa mstari wa mbele kukemea vitendo vya ufisadi bila woga. Miongoni mwao ni Bw.Fredy Mpendazoe (Kishapu), Bw.James Lembeli(Kahama) na Bw. Aloyce Kimaro(Vunjo), ambao wote walengwa wa hasira ya mafisadi.
Habari hizo zilisema majimbo hayo tayari yametengewa milioni 400/- kila moja kwa ajili ya utekelezaji wa mkakati huo na kwamba mgawo wa kwanza wa fedha hizo tayari umetua jimboni Kyela ambapo kata moja imepewa sh. milioni 5.
Hivi karibuni, Dkt. Mwakyembe na Mwenyekiti wa CCM wilayani Kyela, Bw.Japhet Mwakasumi walituhumiwa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya hiyo kuwa ni vinara wa kukigawa chama hicho katika makundi, hali iliyosababisha baadhi ya makatibu kata kuwashambulia na kuwapiga viongozi wa chama wilayani humo.
Katika kikao hicho kilichofanyika Jumapili iliyopita, wajumbe wengi walimshushia makombora, Dkt. Mwakyembe na kudai kuwa tangu awe Mbunge wa jimbo hilo, ametengeneza makundi ndani ya chama huku akidaiwa 'kummiliki' Mwenyekiti wa chama wa wilaya ambaye ameonekana kuyumba katika
maamuzi mbalimbali.
Walisema kufuatia hali hiyo, ndani ya chama hicho, kumekuwepo kutokuelewana na kujengeka
uhasama mkubwa jambo linalowafanya baadhi yao kudai wananyanyaswa
na hawana haki hivyo kuamua kudai haki hiyo kwa kutumia nguvu,
kama walivyofanya viongozi hao wa kata.
Mmoja wa wajumbe hao, Bw.Christopher Mulemwah ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ipinda
alisema, Kamati ya siasa ilikurupuka kufikia uamuzi wa kuwavua uanachama
makatibu kata hao badala ya kukaa na kutafakari chanzo cha viongozi hao kuchukua
uamuzi kuwapiga viongozi wao wa wilaya
Dkt.Mwakyembe kwa upande wake alijitetea na kupinga tuhuma dhidi yake huku akieleza
kuwa makundi yanayoendelea ndani ya chama hicho wilayani Kyela yanazorotesha maendeleo. Alisema
kana kwamba haitoshi, mgawanyiko huko umewakumba hata wakazi wa
Kyela waishio Dar es Salaam.
Alisema binafsi hapendi kuona viongozi hao wanafikishwa mahakamani na kufungwa
bali kilichopo ni chama kuchagua wazee wenye busara kwenda kuwaombea radhi
makatibu kata hao kwa viongozi waliopigwa ili mambo hayo
yaishe
Hata hivyo Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya wilayani, Kyela juzi kilitengua adhabu
ya kufutwa uanachama kwa makatibu kata hao.
Maoni:
Kinyambiss.. sisemi matairi hayachomoki.. point ndiyo hiyo uliyoisema loose nuts.. kabla mtu yeyote hajaanza safari ndefu kuna vitu unavihakikisha vipo katika hali nzuri.. miongoni mwa vya muhimu ni hewa kwenye matairi, wheel alignment na balancing na kuhakikisha kuwa hakuna loose nuts. Kama ulivyosema pia ni kama kitu cha kawaida sana kitu ambacho siamini ni kweli kwani ingekuwa ni cha kawaida hivyo ajali za kuchomoka matairi zingekuwa ni nyingi mno..