Ajali ya Gari Karatu Arusha: Coaster yaua Wanafunzi na walimu wa Lucky Vincent (karibu wote)

Asante sana mkuu. Ndio maana nimesafiri mara tu nilipopata taarifa. Ndugu zangu wengine bado hawaamini na hawataki kuamini. Kaka alikuwa na watoto hao hao ndio walikuwa wanampa faraja baada ya mke wake kuitwa na Mungu mwezi wa pili mwaka huu.

Pole sana ndugu pamoja na wote waliofiwa.

Mwenyezi Mungu awape nguvu, faraja katika kipindi hiki kigumu cha misiba.

Marehemu wapumzike kwa amani.
 
Hlf sasa hao madereva wanaendesha kama wamebeba gunia za viazi na si watoto... pale fire siku moja mpk trafik alimpa vitasa dereva karibu asababishe ajali aue watoto wa watu
 
Poleni sana wafiwa.

Binafsi huwa sipendi kabisa hizo safari za kishule maana naona zipo kibiashara zaidi. Ni kama miradi ya shule vile!
 
Mkuu unahuzunisha na kuchekesha.
Umeshaenda kwa doctor kujifunza mbinu mbalimbali za kupanga jinsia ya mtoto??
Usendelee kuchepuka tafadhari

hahahahahahahahahahaha.....kwel nahuzunisha na kuchekesha!
 
Poleni sana wafiwa.

Binafsi huwa sipendi kabisa hizo safari za kishule maana naona zipo kibiashara zaidi. Ni kama miradi ya shule vile!
ukitaka kugombana na mtoto mkataze kwenda hizo tour sijui walimu wanawapaga nini watoto?
 
Nooooo jaman sitaki kuamini shule nnayoifaham na mwanang alisoma hapo kabla hajahama
Mtt wa mpangaj mwwnzang anasoma hapo ahaaa kwann lkn kifo watt wetu wapendwa mmeondoka mapema sana
We ntakufahamu tutakuwa tunakaa mtaa mmoja
 
Kwanza pole kwa wafiwa. Jambo la msingi ni kufahamu chanzo hasa cha ajali hiyo. Ila nikitazama hilo basi, inaonekana kama abiria hawakuwa wamefunga mikanda kabisa.
 
13 mega pixel ajali haichagui kuwa mko mkwenye private or public transport. Ni kumuomba Mungu aziepushe tu.
Ni kweli ndugu,wiki hii tumepoteza ndugu watano wa familia moja pale Mwidu kabla ya kufika Chalinze ukitokea Moro,walikuwa na private car tairi la mbee likapasuka,ajali haichagui,ni kuomba tu Mola atusimamie.
 
Daaah Mungu awapumzishe kwa Amani, Amina.
 
poleni sana wafiwa tukubali ni kazi ya mungu ,haina makosa poleni sana wafiwa
 
Kuna watu nimewampa hizi habari hapa wameangua kilio, si mchezo.
Inauma sana
 
Amen ndugu yangu. Mungu ni mwema.
 
pongezi kwa kutujuza na poleni sana .
 
School bus ni vichaka vya magari mabovu, RIP taifa la kesho
 
Asante sana mkuu. Ndio maana nimesafiri mara tu nilipopata taarifa. Ndugu zangu wengine bado hawaamini na hawataki kuamini. Kaka alikuwa na watoto hao hao ndio walikuwa wanampa faraja baada ya mke wake kuitwa na Mungu mwezi wa pili mwaka huu.
Hakika ni mtihani ila Mungu atabaki kuwa Baba naye atawapa faraja iliyo kuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…