King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 56,205
- 79,515
Kwani ACT ndio wenye dhamana ya uokoaji? Ndio wanaongoza Serikali? Acha upuuzi hata kama mnalipwa na SICM kupinga wanaokosoa serikali.ACT wazalendo mmefanya nini kwenye zoezi la uokoaji?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani ACT ndio wenye dhamana ya uokoaji? Ndio wanaongoza Serikali? Acha upuuzi hata kama mnalipwa na SICM kupinga wanaokosoa serikali.ACT wazalendo mmefanya nini kwenye zoezi la uokoaji?
Hata Alhaj Ali hassan Mwinyi alimuandikia barua J.K Nyerere mwaka 1976 kujiuzulu baada ya kutokea mauaji shinyanga maana yeye ndio aliyetekeleza hayo mauaji au siyo Troll?Ni kweli kwa sababu Kangi Lugola, Jenista ni Captains wa MV Nyerere
Nasikitika sana kiongozi mkubwa kama wewe huna ufahamu jinsi gani Kamati za maafa zinavyofanya kazi au labda unaenjoy kukashifu Serikali na kuichonganisha Serikali na wananchi.Ajali ya Mv Nyerere: Kangi, Jenista na Kamwelwe Bado mawaziri?
Ni masikitiko makubwa kwamba, Serikali ya wanyonge imeokoa mtu mmoja, wakati wananchi wenyewe wameweza kuokoa watu 40..... hii ni aibu kubwa sana. Watu 225 wamepoteza maisha sababu ya uzembe.
Tuache kujidanganya na mapenzi ya Mungu. Mungu katupa akili, namna ya kuzitumia ni sisi wenyewe. Huwezi kupata Habari ya ajali saa nane mchana halafu ukaitisha Kamati ya Usalama mkoa saa 11 jioni ( yaani mwendo wa Dreamliner Dar-Mwanza mara 4 ). Rais naye hakuitisha Cabinet ya dharura wala Baraza la Ulinzi na Usalama Taifa kuratibu uokoaji. Uokoaji unasitishwa sababu ya GIZA? Tukihoji mnasema tunaleta Siasa? Nonsense!
Kwa nchi zilizoendelea Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri wa Ujenzi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu walitakiwa wawe wamekwishafutwa kazi au wamejiuzulu wenyewe.
Miaka 57 baada ya uhuru...Jeshi la uokozi linapoishia kuwa jeshi la UOPOZI, ni wakati wa rafiki nyangu Kangi Lugola kupumzika. Waziri Kamwelwe, Jenista na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wanapaswa kufukuzwa kazi mara moja. Bahati mbaya sana Rais amechoka na hivyo hajali tena. Wazembe Ndio wameongoza mazishi ya ndugu zetu leo.
Kuna janga lolote duniani ambalo wananchi hawashiriki na kuokoa wahanga wengi zaidi ya Serikali?Tupe mfano.Uongo wa huyo jamaa upo wapi? Je si kweli kuwa wananchi waliokoa wahanga wengi zaidi? Tujibu hoja badala ya kumshambulia mtoa hoja..
Nashukuru wananchi tumeanza kulitambua hili. Jamaa anafanya kila awezalo akamatwe.Lengo la zitto ni kutaka akamatwe au ajibiwe na serikali ili apate kiki. Bahati mbaya haitakua hivyo.
Waliokufa juzi kwenye kimbunga cha marekani, kuna kiongozi wa marekani aliyejiudhuru?Wenzetu huko duniani ajali zikitokea kizembe mtu anawajibika, Angalia Waziri mkuu wa Korea alivyojiuzulu kwa sababu ya ajali ya kivuko!, Sisi kwetu eti tunavunja bodi tunaacha watendaji
South Korean prime minister resigns over ferry sinking
Taa za tronic ndio unaweza ingia nazo majini?Nina mashaka na maharamia kutumia ziwa victoria kutuvamia au kuingiza mambo yao kwa udhaifu wa kutokuwa na taa basi wangechukuwa hata za TRONIC
Mkuu tupe vitu hapa, Zitto anaelimu ganiHakuna wa kumzuru huyu, lakini anachokifanya ni kutumia huu msiba kuiprovoke Serikali ili aakamatwe and it is for his own gain, political stunts, and nothing else, vijana wa umri wake Europe wapo busy kubuni vitu vya msingi kwa ajiri ya Nchi zao, yeye yupo busy kuitumia elimu yake na akili yake kupigania Maslahi ya tumbo lake!
MAJANGA: Serikali ifanye mchakato kukasimu uratibu majanga kwa wizara ya ulinzi - JamiiForumsMi nadhan badala ya kuwataka wakina kangi na wenzake kujiuzuru huu ungekuwa muda sasa wa kujitathmini nini tufanye kama taifa kukabiliana na majanga kabla na baada ya kutokea
Dah kweli kuna watu mna roho mbaya yaani ww huelewi ata ni nn kimetokea umeamua kutetea tu,ipo siku zamu yako wataahirisha kukuokoa namuomba Mungu kesho yake uokolewe ukiwa hai apo nadhani utaijua thamani ya uhai, yaani uzembe wote huo tokea usimamizi wake mpka janga lenyewe na uokoaji wa kizembe kabisa huoni?Mkuu ni bora sana kueshimu taalamu sio kwa kuwa wewe mwana siasa ndio ukajiona bora na mwenye akili hata kwa fani usizozijua kusema watu wamesitisha uokoaji kwa ajili ya giza ni nonsense huwatendi haki if you know nothing kwenye rescue at sea bora ukae kipya ni kweli tuna jeshi la uokozi lakini uokozi wa nini? rescue at sea ni tafauti sana na rescue za aridhini je kuna sheria au taasisi mahususi ya ukoaji wa majini tz na kama hakuna nyie kam wabunge mmechukua hatua gani?