Nasikitika sana kiongozi mkubwa kama wewe huna ufahamu jinsi gani Kamati za maafa zinavyofanya kazi au labda unaenjoy kukashifu Serikali na kuichonganisha Serikali na wananchi.
Naomba nikuulize maswali muhimu kwa niaba ya umma wa wapenda ukweli.
1-Unafahamu kamati ya maafa ya mkoa inaundwa na nani ?Mwenyekiti wa kamati hiyo ni nani?wajumbe wake ni kina nani?
2-Unafahamu ni wakati gani au kwa tukio gani kamati ya maafa ya wilaya inaitishwa?
3-Unafahamu ni wakati gani kamati ya maafa ya mkoa inaitishwa au kwa lugha ya kitaalamu inakuwa activated?
4-Je ni wakati upi kamati ya maafa ya kitaifa inaitishwa?kwa vigezo vipi?
unawafahamu wajumbe wake?
Furthemore bwana mdogo
Zitto
5-Unafahamu ni wakati gani kamati za maafa za kikanda au kimataifa zinaundwa?ni matukio ya aina gani yana-activate kamati tajwa?
Acha kupotosha umma kijana huu sio ushabiki wa liverpool na Southampton haya ni maafa na Taifa lipo msibani...
Eti unasema Serikali imeokoa mtu mmoja tu?...Hii ni insanity....hivi watu walinusurika walitibiwa na yule babu yako unayetishiaga naye watu au ACT Wazalendo?
Zitto do you know ABCs za uokoaji kwenye maji?Je una thamini usalama wa wataalamu wa uokozi au wataalamu wa kukabiliana na majanga?
Kwa nini basi kama uliona mambo hayaendi vizuri hukutoka huko majuu ulipo ili kuja kusaidia uokoaji Gizani?
Hivi
Zitto nikuulize je pale Katika jimbo lako au wilaya yako wewe sio mjumbe wa kamati ya maafa ya wilaya au hata mkoa wenu? Je hufahamu au hujawahi kuhusishwa kwenye Maandalizi ya Disaster Management and preparedness.
Hakuna contigency plan ya kupambana na majanga katika wilaya yako?
Kama ipo kwa nini unaisema Serikali ni zembe?
Kama hakuna je tukulaumu kwa kukaa kimya?
Zitto ni kama vile unalazimishia kukamatwa na kuhojiwa ili upate kiki ya aina mpya yaani eti umekamatwa kwa kuhoji...huu ni utoto na sio siasa bali ni ubaradhuli na roho mbaya kwa wafiwa na waathirika wa tukio hili.
Hivi ukihojiwa na sisi wananchi utupe makosa specific kwa kila unayemlaumu utaweza kujibu?
Nakushauri utulie na usisake kiki ya kisiasa ...wananchi wa Ukara ndio wanaojua kilichotokea ...wanaelewa uzembe upo wapi na wanajua nani awajibike ndio maana kwa sasa wapo msibani na wanaomboleza.
You have been shifting your line of attack yaani mara urukie kwa Rais,Mara JWTZ,Mara mawaziri Mwisho utataka hadi kumtusi Mwenyezi Mungu.
Zitto hebu tumia busara kidogo na ujaribu kukumbuka tweet yako mojawapo ya tarehe 1 juni 2014 na ulinganishe walioyasema watanzania siku hiyo kwako na kwa umma.
Ukiikumbuka siku hii vyema basi utaelewa thamani ya Mtu mmoja kuokolewa na Serikali.