Ajali ya Mwendokasi, Dereva akimbia

Ajali ya Mwendokasi, Dereva akimbia

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Kumetokea ajali inayohusisha basi la Mwendokasi na mtembea kwa miguu.

Ajali imetokea ahsubuhi hii kwenye barabara ya Mwendokasi mbele ya Hoteli ya Kempiski Hyatt
Zamani Kilimanjaro Hotel.

Basi la Mwendokasi likitokea Posta ya Zamani, dereva wake hakujali kivuko cha watembea kwa miguu alimgonga mtu aliyekuwa anavuka na kumkosakosa kumpanda.

Ajali imetokea mbele ya polisi ambao walikimbilia eneo la tukio na kuenda kumpa huduma ya kwanza maneruhi aliyekuwa anapaparika.

Dereva wa Mwendokasi alikimbia eneo la tukio na kupanda bodaboda mbele na kutokomea kusiko julikana.

Ajali za magari ya Mwendokasi zimezidi na kusababisha madhara na vifo kwa watembea kwa miguu. Mwaka jana jirani yangu aligongwa na kupoteza maisha kwenye zebra croasing pale eneo la Utumishi. Basi lililosababisha lilikuwa linatokea stand ya Kivukoni.

Mamlaka iangalie upya conducts za madereva wa mabasi hayo na kuwapa training za mara kwa mara kwa sababu hali ni mbaya. Na itakuwa mbaya zaidi endapo route ya Mbagala itafunguliwa
 
Madereva wa hayo mabasi wanajikuta miamba sana kuna mmoja alikatizaga taa nyekundu na spidi kama zote polisi alipomsimamisha akaanza kuporomosha mitusi ya nguoni, ooh mimi mwanajeshi tena nimekuzidi cheo unaanzaje kunisimamisha ,sijui mbwa wewe sijui nini yaani kipindi kile nilijisikia aibu kwa niaba ya askari yule wa usalama barabarani, inatakiwa wawe wanawajibishwa kama watu wengine tu, hakuna mtu mwenye ruhusa ya kuua mwenzake hata kama unaendesha treni
 
Polisi walikuwepo hapo. Nnachojiuliza huyo bodaboda ni mpumbavu kiasi gan
Ninachowapongeza polisi ni kumkimbilia majeruhi kwanza na kuzuia mabasi mengine ya mwendokasi yaliyokiwa yanakuja kwa kasi, ndipo dereva akapata mwanya kutoka nduki. Bodaboda amepandia mbele ya Mahakama Kuu.

Bodaboda aliyemchukua alikiwa anajua kabisa anamtorosha dereva kwa sababu alitokea nyuma ya dereva aliyekuwa anakimbia na dereva akamdandia wakatoka nduki

Polisi wakijaribu kumfukuza wakamkosa. Hawakuwa na means ya matairi
 
madereva wa hayo mabasi wanajikuta miamba sana kuna mmoja alikatizaga taa nyekundu na spidi kama zote polisi alipomsimamisha...
Serikali ni kama imewaruhusu jamaa wajiendeshe nje ya sheria na kanuni za usalama barabarani.

Unapoona watumishi wa Mwendokasi wanawatunishia mpaka Polisi wasitumie barabara ile wakati wa dharura ujue kuna shida kubwa sana iliyotawaliwa na kiburi
 
madereva wa hayo mabasi wanajikuta miamba sana kuna mmoja alikatizaga taa nyekundu na spidi kama zote polisi alipomsimamisha akaanza kuporomosha mitusi ya nguoni, ooh mimi mwanajeshi tena nimekuzidi cheo unaanzaje kunisimamisha ,sijui mbwa wewe sijui nini yaani kipindi kile nilijisikia aibu kwa niaba ya askari yule wa usalama barabarani, inatakiwa wawe wanawajibishwa kama watu wengine tu, hakuna mtu mwenye ruhusa ya kuua mwenzake hata kama unaendesha treni
Namshukuru Mungu sana,siku moja Jioni nilikua navuka barabara ya mwendokasi pale Utumish kwenye Zebra cross huku nachati na simu yangu,sikujua kua nimemaliza kuvuka kumbe bado niko ndani ya barabara,Basi kumbe upande wa pili bus la mwendokasi linakuja wangu wangu kutoka kivukoni,huku upande wa pili wafanyabiashara ndogo ndogo wapale pembeni wananiita kwa sauti kubwa sana nitoke barabarani,lakini masikini nilikua siwaasiki kabisa! Mungu ni mwema sana yule dereva wa mwendokasi alisimama karibu yangu kabisa,na ndiyo nastuka kua kumbe bado niko barabarani!! Kwa kweli namshukuru Mungu hadi Leo kwa kuniponya kwa hiyo ajali!!!!
 
Back
Top Bottom