Namshukuru Mungu sana,siku moja Jioni nilikua navuka barabara ya mwendokasi pale Utumish kwenye Zebra cross huku nachati na simu yangu,sikujua kua nimemaliza kuvuka kumbe bado niko ndani ya barabara,Basi kumbe upande wa pili bus la mwendokasi linakuja wangu wangu kutoka kivukoni,huku upande wa pili wafanyabiashara ndogo ndogo wapale pembeni wananiita kwa sauti kubwa sana nitoke barabarani,lakini masikini nilikua siwaasiki kabisa! Mungu ni mwema sana yule dereva wa mwendokasi alisimama karibu yangu kabisa,na ndiyo nastuka kua kumbe bado niko barabarani!! Kwa kweli namshukuru Mungu hadi Leo kwa kuniponya kwa hiyo ajali!!!!