Ajali ya Mwendokasi, Dereva akimbia

Ajali ya Mwendokasi, Dereva akimbia

Ninachowapongeza polisi ni kumkimbilia majeruhi kwanza na kuzuia mabasi mengine ya mwendokasi yaliyokiwa yanakuja kwa kasi, ndipo dereva akapata mwanya kutoka nduki. Bodaboda amepandia mbele ya Mahakama Kuu.

Bodaboda aliyemchukua alikiwa anajua kabisa anamtorosha dereva kwa sababu alitokea nyuma ya dereva aliyekuwa anakimbia na dereva akamdandia wakatoka nduki

Polisi wakijaribu kumfukuza wakamkosa. Hawakuwa na means ya matairi
Bado nasisitiza bodaboda hana kosa. Amechangamkia fursa ya abiria aliyekuwa na uhitaji wa dharula
 
Kumetokea ajali inayohusisha basi la Mwendokasi na mtembea kwa miguu.
Ajali imetokea ahsubuhi hii kwenye barabara ya Mwendokasi mbele ya Hoteli ya Kempiski Hyatt
Zamani Kilimanjaro Hotel.

Basi la Mwendokasi likitokea Posta ya Zamani, dereva wake hakujali kivuko cha watembea kwa miguu alimgonga mtu aliyekuwa anavuka na kumkosakosa kumpanda.

Ajali imetokea mbele ya polisi ambao walikimbilia eneo la tukio na kuanda kupa huduma ya kwanza maneruhi aliyekuwa anapaparika.

Dereva wa Mwendokasi alikimbia eneo la tukio na kupanda bodaboda bele na kutokomea kusiko julikana.

Ajali za magari ya Mwendokasi zimezidi na kusababisha madhara na vifo kwa watembea kwa miguu. Mwaka jana jirani yangu aligongwa na kupoteza maisha kwenye zebra croasing pale eneo la Utumishi. Basi lililosababisha lilikuwa linatokea stand ya Kivukoni.

Mamlaka iangalie upya conducts za madereva wa mabasi hayo na kuwapa training za mara jwa mara kwa sababu hali ni mbaya. Na itakuwa mbaya zaidi endapo route ya Mbagala itafunguliwa
Madereva wengi hawafatilii sheria na alama za barabarani, matokeo yake wanaendesha vyombo husika kwa mazoea tu,usiku wa kuamkia leo mataa Kimara Kibo nikiwa natokea Ubungo ili nifanye U turn kurudi tena Ubungo gari ya mwendokosi nilishuhudia ikipita bila kufuata Taa za kuongoza barabara {Namaanisha basi la mwendokosi wakati linakatiza Taa nyekundu ilikuwa imeshawaka na sekunde zilishakatika takribani kumi hivi}.
 
Namshukuru Mungu sana,siku moja Jioni nilikua navuka barabara ya mwendokasi pale Utumish kwenye Zebra cross huku nachati na simu yangu,sikujua kua nimemaliza kuvuka kumbe bado niko ndani ya barabara,Basi kumbe upande wa pili bus la mwendokasi linakuja wangu wangu kutoka kivukoni,huku upande wa pili wafanyabiashara ndogo ndogo wapale pembeni wananiita kwa sauti kubwa sana nitoke barabarani,lakini masikini nilikua siwaasiki kabisa! Mungu ni mwema sana yule dereva wa mwendokasi alisimama karibu yangu kabisa,na ndiyo nastuka kua kumbe bado niko barabarani!! Kwa kweli namshukuru Mungu hadi Leo kwa kuniponya kwa hiyo ajali!!!!
Sio wewe ulivunjiwa simu na wasamaria wema baada kukuita huku umevaa earphone husikii hata kidogo?kama ni wewe endelea kuomba Mungu maana siku ile usingepona.
 
kwa jinsi DART ma watumishi wake walivyoranduka ni wazi kwa sasa ni idara yenye serikali na sheria zake nje ya hizi za kawaida.

jambo la msingi ni kuwaacha na magari yao.
 
Kuna mdau kanijibu hiyo barabara ni ya mwendokasi haihitaji matuta, nadhani yuko sahihi pia
ndio hivyo na hata zebra zipo kwenye vituo vya mwendokasi tu, so hata hapo hayyt kempiski hakuna zebra, zebra zipo huku kituoni posta mpya nbc bank.
Hapo dreva wa mwendokasi kosa lake ni kukimbia baada ya kutokea hiyo ajali
 
Dereva yuko sahihi kukimbia kwani wangempiga.
Bila shaka atajisalimisha.
Siku hizi wavukaji kwenye zebra wanatamani kulala kabisa sijui nini kimewapata watu.
Ukisimama kuwapisha wapite ndio kwanza wanatamani kusimama barabarani
Walijazwa vichwa na trafiki, kuwa ni haki yao, wanavuka wanachat na simu,

Hawajui kesi za trafiki sio nzito kama kujeruhi au kuuwa kwa panga,

Wengine wanavimba kabisa, wanasema nigonge uone,
Bila kujua kuna wakati gari inaweza kupata tatizo la brake na kusaababisha ajali bila kutarajia,

Dereva mwenye akili timamu huwezi kumsababishia mtu ulemavu au kifo kwa kukusudia,
 
Pamoja ni haki yetu kwenye zebra tahadhari muhimu, magari yanaendeshwa na binadamu wenye misongo ya mawazo tele hivyo tahadhari muhimu
 
Serikali ni kama imewaruhusu jamaa wajiendeshe nje ya sheria na kanuni za usalama barabarani.

Unapoona watumishi wa Mwendokasi wanawatunishia mpaka Polisi wasitumie barabara ile wakati wa dharura ujue kuna shida kubwa sana iliyotawaliwa na kiburi
Kwani hyo barabara ni ya polisi. Watu tuzingatie matumiz Sahihi ya barabara... Hyo dharura unaijuaje?
 
Pale mm nilisha wahi koswa koswa niliangalia upande mmoja kutoka kivukoni sikungalia upande wa kutoka posta ila naanza kuvuka tu nilisikia honii harafu jamaa wanajua kabisa pale kuna zebra ila speed wanazokuja nazo sio kabisa...wanatakiwa wawe wastaarabu kwa kweli sehem za watu wengi wapite taratibu.
Vivuko viwekwe matura hoja mshana Jr Ina mashiko
 
Namshukuru Mungu sana,siku moja Jioni nilikua navuka barabara ya mwendokasi pale Utumish kwenye Zebra cross huku nachati na simu yangu,sikujua kua nimemaliza kuvuka kumbe bado niko ndani ya barabara,Basi kumbe upande wa pili bus la mwendokasi linakuja wangu wangu kutoka kivukoni,huku upande wa pili wafanyabiashara ndogo ndogo wapale pembeni wananiita kwa sauti kubwa sana nitoke barabarani,lakini masikini nilikua siwaasiki kabisa! Mungu ni mwema sana yule dereva wa mwendokasi alisimama karibu yangu kabisa,na ndiyo nastuka kua kumbe bado niko barabarani!! Kwa kweli namshukuru Mungu hadi Leo kwa kuniponya kwa hiyo ajali!!!!
We ni mcenge,hivyo vya kuchati huwa haviwezi kungoja!?
 
Kwani hyo barabara ni ya polisi. Watu tuzingatie matumiz Sahihi ya barabara... Hyo dharura unaijuaje?

Dharura ni kama vile unavyoshikwa na tumbo la makande na ukienda chooni unakuta kipo occupied na unapaswa kusubiri wakati rinda zinashishwa kukaba mzigo usichuruzike mwendo wa kulipuka
 
Back
Top Bottom