Ajali ya Mwendokasi, Dereva akimbia

Ajali ya Mwendokasi, Dereva akimbia

Kwani hyo barabara ni ya polisi. Watu tuzingatie matumiz Sahihi ya barabara... Hyo dharura unaijuaje?

Dharura ni kama vile unavyoshikwa na tumbo la makande na ukienda chooni unakuta kipo occupied na unapaswa kusubiri wakati rinda zinashishwa kukaba mzigo usichuruzike mwendo wa kulipuka
 
Ilibidi ugongwe ufe kabisa kwa uzembe wako.
Unachati na simu barabarani ukivuka, un faida gani?
Namshukuru Mungu Dereva alikua na ubinaadamu hadi akasimama hakua dereva wa hovyohovyo, hao ndiyo madereva wanaoendesha chombo huku wakijua kua barabarani kuna watu wengine pia wanatumia,na kila Mtu na mawazo yake! Kuna madereva wengi tu wa mwendokasi ni wastaarabu sana na wanahuruma sana,tena wengine utawaona wanavipanga hadi vitoto vya shule kwa upole sana!!
 
Kwani hyo barabara ni ya polisi. Watu tuzingatie matumiz Sahihi ya barabara... Hyo dharura unaijuaje?

Dharura ni kama vile unavyoshikwa na tumbo la kuhara na ukienda chooni unakuta kipo occupied na unapaswa kusubiri wakati rinda zinashishwa kukaba mzigo usichuruzike mwendo wa kulipuka

Huo ndo mfano wa dharura
 
We nae unaonekana ni zuzu sana.

Wangekugonga utawanyike mapafu.
Siyo zuzu basi tu kuna Kama kitu kilinifunga kwa muda, maana hadi wale wafanyabiashara ndogo ndogo walikua wananiita kwa sauti lakini eti nilikua siwaasiki kabisa hadi gari iliposimama karibu yangu ndiyo ufahamu ukarudi na kuaanza kusikia hadi yale Makelele ya wafanyabiashara ndogo ndogo tena!!!
 
Sio wewe ulivunjiwa simu na wasamaria wema baada kukuita huku umevaa earphone husikii hata kidogo?kama ni wewe endelea kuomba Mungu maana siku ile usingepona.
Sikua na earphone,nilikua nachati kawaida tu! Sema Kama kuna kitu kilinifunga kwa muda!!
 
Namshukuru Mungu sana,siku moja Jioni nilikua navuka barabara ya mwendokasi pale Utumish kwenye Zebra cross huku nachati na simu yangu,sikujua kua nimemaliza kuvuka kumbe bado niko ndani ya barabara,Basi kumbe upande wa pili bus la mwendokasi linakuja wangu wangu kutoka kivukoni,huku upande wa pili wafanyabiashara ndogo ndogo wapale pembeni wananiita kwa sauti kubwa sana nitoke barabarani,lakini masikini nilikua siwaasiki kabisa! Mungu ni mwema sana yule dereva wa mwendokasi alisimama karibu yangu kabisa,na ndiyo nastuka kua kumbe bado niko barabarani!! Kwa kweli namshukuru Mungu hadi Leo kwa kuniponya kwa hiyo ajali!!!!
Uache na upumbavu bwana mdogo wa kuvuka huku unachat na simu.
 
Yale mabasi huwa yanajipata kama treni vile...
 
Namshukuru Mungu Dereva alikua na ubinaadamu hadi akasimama hakua dereva wa hovyohovyo, hao ndiyo madereva wanaoendesha chombo huku wakijua kua barabarani kuna watu wengine pia wanatumia,na kila Mtu na mawazo yake! Kuna madereva wengi tu wa mwendokasi ni wastaarabu sana na wanahuruma sana,tena wengine utawaona wanavipanga hadi vitoto vya shule kwa upole sana!!
Una bahati sana.
Kosa kubwa ambalo pedestrians wanafanya ni kufikiri dereva anaona kila kitu.
Watu wengi wanauawa barabarani kwa kutochukua tahadhari, wanaongea na simu na hawana concentration ya magari yanayopita.
Kwenye barabara za kawaida tu unaona mtu anaongea na simu , dereva mstaarabu anasima, lakini huyo pedestrian anauwawa na gari linalo uvertake kwa soidi kali.
Mlinzi wa maisha barabarani ni wewe mwenyewe, si dereva.
 
ndio hivyo na hata zebra zipo kwenye vituo vya mwendokasi tu, so hata hapo hayyt kempiski hakuna zebra, zebra zipo huku kituoni posta mpya nbc bank.
Hapo dreva wa mwendokasi kosa lake ni kukimbia baada ya kutokea hiyo ajali
Kapaniki ajali si kitu kidogo
 
waliopanga na kupitisha plan za huu mradi waliwaza makusanyo na mfumo wa uendeshaji wa yale magari uwe kama wa treni
Huku mbagala sijui itakuwaje maana boda boda wa huku wote akili hawana ,wao wanaangalia tu mbele pikipiki zao hazina site mirrow , na wengi wao hata sheria za kuvuka barabara hawazijui,

Wanajua mwendokasi hata na wao waendesha boda boda ni mwendo kasi wanatakiwa kupita njia moja.
 
Zile ndude kwa sasa speed 50! Lakini ajabu nusu ya madereva wa vile vidubwana wanakula Ugoro
 
Back
Top Bottom