Swali ndugu yangu Barafu.
Kwenye issue ya Mlango unaozungumziwa ulikuwa ni ule wa "emmergency exit" au hii milango ya kawaida ya mbele na nyuma?.
Je "emmergency exit" doors za ATR zinafunguka kwenda chini na kuwa ngazi balanced na small hydraulic cylinders left and right au ni ule unaofunguka kwa kwenda juu ukifyatua latch kwa ndani?
Kwa maelezo ya Victor, mmoja wa survivors, aliuzuia mlango kwa mguu usijifunge. Hii inatoa picha ni mlango wa kufungua kama wa gari na sio juu kwenda chini na kugeuka kuwa ngazi, ambapo utatulizwa na gravity pengine.
Pamoja na yote, inawezekana Majaliwa anaonekana kushambuliwa na baadhi lakini naye ni victim tu wa kuingiza sasa. Kwa akili ya kawaida, watu Baki wana sababu gani kumshambulia Majaliwa? Kunaweza kukawa na wivu au baadhi ya waokozi wenzake kuhisi mchango wao haujathaminiwa, lakini Kwa wengi wetu, chochote alichoweza kufanya Majaliwa si cha kubeza.
Siasa iliingia pale ambapo pengine kwa kupelekwa na public pressure, kuchutama (save grace) baada ya mapungufu yetu kukabiliana na tukio kuonekana wazi, kum contain Majaliwa ili ku control narrative, na sababu nyingine wanazozijua wao, viongozi wetu wakambeba Majaliwa na kuanza kumparade na kumpa mengi ambayo pengine baadhi yetu (umma) uliona anastahili. Haraka iliyotumika kufanya maamuzi hayo inaonyesha mapungufu ya uongozi, maana ukijuiliza kulikuwa na haja gani ya msingi kufanya maamuzi Kwa spidi hiyo sijui kama utapata majibu. Muda kidogo na utulivu ungewapa nafasi ya kuwasikia akina Victor na wahanga wengine, wavuvi, mashuhuda, kufanya maamuzi ambayo yangepata utetezi wa kimantiki hadi kesho. Milioni 5 na ajira kwa Majaliwa hata vingetoka mwezi ujao kusingepungua kitu. Kwenye mazingira ambapo siasa ilitangulia, pengine si ajabu kuona siasa imetamalaki mpaka kesho. Na Majaliwa yuko katikati ya mapambano yasiyomhusu. Risasi zinaonekana kutupwa kwake ni stray, lakini mlengwa halisi ni perceived ubovu wa taasisi zetu na viongozi, ambavyo pia vinajionyesha kwenye hayo anayosema mtoa mada ya kufanya emergency drill kwa mazoea. Performative actions kwenye maeneo ambapo kinachotakiwa ni substantive, thought through practices.
Kwenye mazingira ya kazi ambapo inatangulizwa siasa, najiuliza kama hata TCAA na vyombo vyake viko kwenye mazingira sahihi kufanya majukumu yake, hata kama uwezo wanao. Kumbuka vyombo hivi viliooifungia Fastjet, sababu zilizowekwa wazi ni za kulinda usalama. Wakiingiliwa na siasa kama hivi, tunazipa nguvu hoja za wanaodai walifungiwa ili wamwachie ruti ATC.