Ajali ya ndege Bukoba ni matokeo ya uzembe na kufanya kazi kwa mazoea.Tuwajibishane ili tusirudie makosa

Ajali ya ndege Bukoba ni matokeo ya uzembe na kufanya kazi kwa mazoea.Tuwajibishane ili tusirudie makosa

Swali ndugu yangu Barafu.

Kwenye issue ya Mlango unaozungumziwa ulikuwa ni ule wa "emmergency exit" au hii milango ya kawaida ya mbele na nyuma?.

Je "emmergency exit" doors za ATR zinafunguka kwenda chini na kuwa ngazi balanced na small hydraulic cylinders left and right au ni ule unaofunguka kwa kwenda juu ukifyatua latch kwa ndani?
 
"Mlango wa ATR42 unafungukia kwa nje,anayefungua anapaswa kuwa ndani,lakini ni lazima apate msaada wa mtu wa nje.Sababu unapoufungua mlango wa ATR42 hutumika kama mlango na ndio ngazi pia ya kuingia na kutoka katika ndege.Hivyo unapofunguliwa mtu wa nje ni lazima auishike,aweke stabilize stick itakayofanya mlango usijifunge."

Maelezo ya Majaliwa, taarifa ya awali ya wizara na haya yako yana utofauti. Majaliwa anadai yeye aliupiga mlango na kasia ndiyo ukafunguka kwa maelezo yake haya unapata picha kuwa wa ndani hawakushughulika kbs ni yeye aliyesababisha mlango ufunguke na ndiyo maana credit alijichukulia, baadaye ndiyo tulipata taarifa walioufungua mlango ni watu wa ndani mhudumu na abiria na baada ya wao dk 5 mbele ndiyo boti zikafika kwa wao Majaliwa hakupiga mlango na kasia maana walishaufungua mlango tyr wavuvi walikuja tu kuwasaidia kuwaondoa wahanga toka kwenye ndege mpk nchi kavu

Kwa mkanganyiko huo ndiyo maana mjadala wa majaliwa umekuwa mkubwa na kuchukua hisia za wengi

Hayo mengine nakubaliana na wewe ila kwa Majaliwa hapana
 
Matukio 3 ya ajali kubwa ndani ya ziwa viktoria
Ya kuzama MV Bukoba,MV Ukara na hii ndege PW inaonyesha wazi kuwa liko tatizo la kutokuwa na miundo mbinu kwenye ziwa hilo pendekezo
1.kianzishwe kikosi cha wanamaji waokoaji (wazamiaji)kiwe makao makuu Mwanza na matawi yake yawe Musoma na Bukoba/ukerewe
2. Kwa mazingira ya ziwa viktoria kutumika na vyombo vikubwa vya usafiri na viwanja vya ndege kuzunguka ziwa vifaa vya kuokoa vinavyoendena na uokoaji majini speed boat 1 kila tawi,mitungi ya oksjeni,magari na vituo vidogo vya afya kwa dharura vijengwe pembezoni mwa ziwa yenye madaktari wabobezi.
3.ukaguzi wa vyombo vya majini ufanyike barabara
4. Viwanja vya Bukoba na Musoma vipewe control tower
5.elimu ya uokoaji kwa wavuvi na wanaoishi pembezoni mwa ziwa.
Haya ni mambo ambayo mamlaka za usafiri wa anga na majini vinapaswa viangazie kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola.
 
Hayo mambo yote uliyoyataja ni theory tu na hayatumiki Tanzania, tungeanza na bajeti, Serikali inatenga bajeti kiasi gani kwa kikosi cha uokoaji na usalama wa wananchi hata tu kwenye huo uwanja? Meneja wa Uwanja ana bajeti kiasi gani kwa ajili ya dharura?

Serikali imetumia Mabilioni kwa ajili ya matangazo tu ya majibu sensa.
Serikali KUU inawajibika kwa yaliyotokea kwa 100% kwani walipaswa kuokoa watu na siyo sijui vidagaa kama Meneja wa Kiwanja, shida iko kwa Kiongozi Mkuu na siyo vidagaa!

Swali langu kwako Meneja wa Uwanja ana bajeti ya kiasi gani kuweza kutoa huduma za dharura? Je, ana vifaa na manpower yenye ujuzi wa kutosha kudili na maafa?
 
Mengine yoote umeyaainisha kitalaam kwa uzoefu na ukongwe wako kwenye Aviation industry, wahusika wanapaswa kujitathmini na Wenye mamlaka wanapaswa kuwajibisha wazembe na hata kuwafungulia mashitaka ya kusababisha vifo kizembe wakiwa na dhamana ya kufanya uokozi.

Kama ulivyosema, all important aspect for safety katika uwanja huo ni mashaka mashaka tu na watu kila siku wako maofisini kuanzia Mawaziri mpaka wakurugenzi na hata baada ya kupotea roho za watu bado wanaleta blah blah tu..
Yupi wa kujotathmini?
 
Swali ndugu yangu Barafu.

Kwenye issue ya Mlango unaozungumziwa ulikuwa ni ule wa "emmergency exit" au hii milango ya kawaida ya mbele na nyuma?.

Je "emmergency exit" doors za ATR zinafunguka kwenda chini na kuwa ngazi balanced na small hydraulic cylinders left and right au ni ule unaofunguka kwa kwenda juu ukifyatua latch kwa ndani?
Kwa maelezo ya Victor, mmoja wa survivors, aliuzuia mlango kwa mguu usijifunge. Hii inatoa picha ni mlango wa kufungua kama wa gari na sio juu kwenda chini na kugeuka kuwa ngazi, ambapo utatulizwa na gravity pengine.

Pamoja na yote, inawezekana Majaliwa anaonekana kushambuliwa na baadhi lakini naye ni victim tu wa kuingiza sasa. Kwa akili ya kawaida, watu Baki wana sababu gani kumshambulia Majaliwa? Kunaweza kukawa na wivu au baadhi ya waokozi wenzake kuhisi mchango wao haujathaminiwa, lakini Kwa wengi wetu, chochote alichoweza kufanya Majaliwa si cha kubeza.

Siasa iliingia pale ambapo pengine kwa kupelekwa na public pressure, kuchutama (save grace) baada ya mapungufu yetu kukabiliana na tukio kuonekana wazi, kum contain Majaliwa ili ku control narrative, na sababu nyingine wanazozijua wao, viongozi wetu wakambeba Majaliwa na kuanza kumparade na kumpa mengi ambayo pengine baadhi yetu (umma) uliona anastahili. Haraka iliyotumika kufanya maamuzi hayo inaonyesha mapungufu ya uongozi, maana ukijuiliza kulikuwa na haja gani ya msingi kufanya maamuzi Kwa spidi hiyo sijui kama utapata majibu. Muda kidogo na utulivu ungewapa nafasi ya kuwasikia akina Victor na wahanga wengine, wavuvi, mashuhuda, kufanya maamuzi ambayo yangepata utetezi wa kimantiki hadi kesho. Milioni 5 na ajira kwa Majaliwa hata vingetoka mwezi ujao kusingepungua kitu. Kwenye mazingira ambapo siasa ilitangulia, pengine si ajabu kuona siasa imetamalaki mpaka kesho. Na Majaliwa yuko katikati ya mapambano yasiyomhusu. Risasi zinaonekana kutupwa kwake ni stray, lakini mlengwa halisi ni perceived ubovu wa taasisi zetu na viongozi, ambavyo pia vinajionyesha kwenye hayo anayosema mtoa mada ya kufanya emergency drill kwa mazoea. Performative actions kwenye maeneo ambapo kinachotakiwa ni substantive, thought through practices.


Kwenye mazingira ya kazi ambapo inatangulizwa siasa, najiuliza kama hata TCAA na vyombo vyake viko kwenye mazingira sahihi kufanya majukumu yake, hata kama uwezo wanao. Kumbuka vyombo hivi viliooifungia Fastjet, sababu zilizowekwa wazi ni za kulinda usalama. Wakiingiliwa na siasa kama hivi, tunazipa nguvu hoja za wanaodai walifungiwa ili wamwachie ruti ATC.
 
Back
Top Bottom