Ajali ya ndege Bukoba ni matokeo ya uzembe na kufanya kazi kwa mazoea.Tuwajibishane ili tusirudie makosa

Analysis ya barafu ni funga kazi. Ngoja nipumzishe fuvu nikiamka bdae I will dot the i's and cross the t's.
Hawa watu wenye ujuzi na mambo ya Usimamizi wa miradi ya ndege ndio wanapewa kupewa vitengo. Lakini hapa kwetu si ajabu kukuta mtu anayesimamia viwanja vya ndege hana utaalam wowote na mambo ya ndege! Barafu mama kuonesha akupe majukumu akutoe huko uliko!
 
Mkuu asante kwa maelezo mazuri
Ila kwa namna ulivyolielewa hili sakata naomba ufafanuzi wa haya;

1.Ilikuwaje marubani wakafa wakati Majaliwa aliongea nao mpaka akawaaga?

2.Hii ndege ilipataje ajali? Je iliamua kutua kwenye kiwanja ndio ikasukumwa kuelekea majini au ilizunguka(Orbiting)kama ulivyosema kisha rubani kwa kuishiwa mafuta akaamua atue baharini au akiwa anazunguka ilipata hitilafu ndio ikaangukia ziwani?

3.Je ndege ina milango mingapi? Na mlango wa ndege uliofunguliwa ni upi?ni huo ambao hugeka ngazi kuna mlango mwingine?

Nadhani baada ya hizi ripoti kutoka kuna haja ya Majaliwa kuhojiwa upya ili kuondoa mkanganyiko,maana sisi tunamuona kama shujaa lakini kuna mambo aliyosema bado yanaligawa taifa kama aaminike au asiaminike,Kumbuka hata waziri Mbarawa kasema mlango ulifunguliwa na watumishi kwa ndani na sio kwa kushirikiana na wavuvi,sidhani kama amelisema hili kwa bahati mbaya hasa akijua kabisa kwamba tayari Majaliwa alishasema yeye ndio aliupiga mlango kwa kasia ukafunguka na kuanza kuwatoa watu.
 
Ukila biskuti za bangi usitegemee kumuelewa mbobezi wa Aviation anapochanganuwa mambo.

Wewe nenda boomplay huko ndio level yako utawaelewa kina Mboso, Zuchu na Diamond.
Mbobezi my foot. Ila sishangai humu wajinga mpo wengi sana na kibaya zaidi huwa mnatoa mawazo yenu. Bora mngekua kimya
 
Hiyo ripoti ningeshangaa kama ingetoka tofauti na hivyo.

Ni aibu sana kwa mamlaka husika kukubali uzembe wao.

Lazima tu Majaliwa aaibishwe.
 

Mlango wa ATR unafunguka kwa kwenda chini,upo sahihi,unakuwa supported kushoto na kulia.
 
Sidhani kama kuna mtu anabeza mchango wa wavuvi katika kuokoa maisha ya abiria. Watu wanachopinga ni kumfanya mmoja wao ndio steling wakati waliohusika ni wengi. In fwakt kwa kufanya hivyo mchango wa wavuvi wenzake walioshirikiana nae ulipuuzwa kiasi cha kuwafanya walalamike. Aidha, mchango mkubwa wa mhudumu na yule jamaa nao ulionekana hauna maana sana kwa sababu tayari tulishamtunuku Majaliwa u Superman.

Nina shaka na hilo unalosema kuwa mlango wa ATR ni lazima awepo mtu nje ndio ufunguke. Unataka kutuambia kuwa ajali ikitokea mahali ambapo hamna mtu wa kusaidia kutoka nje (porini, baharini n.k.) waliomo ndani watapoteza maisha yao? Utakuwa ni emergency exit ya ajabu sana ambayo haiwezi kutumika mpaka mtu afungue kwa nje.

Amandla...
 
Umemaliza kila kitu mkuu barafu hujawahi kuniangusha tangu enzi za mlazo mapera mengi na migori zaidi zambarau umewamaliza Sasa tujadili hizo power bank zilizowasili za TRC tukisubiri mabehewa sijui yatafika lini shukrani
 
Mbobezi my foot. Ila sishangai humu wajinga mpo wengi sana na kibaya zaidi huwa mnatoa mawazo yenu. Bora mngekua kimya
Jipigepige kifuani huku ukijisemesha Mimi ni mchawi kasoro vitendea kazi ndio sina.

Hapa JF ni barafu ndio amekuwa ngumu wa kuchambuwa industry ya Aviation unless kama ndio leo umeanza kuna Uzi wake.

Fistula inatibika wahi matibabu.
 
Nimekuja , unasemaje ?
 
Walamba asali awatopenda kusikia haya, wana hoja zao eti kadi ya CUF ndugu barafu umerudisha lini? Awakumbuki tunaongelea ishu za kitaifa na sio kadi za chama.
 
Mbobezi my foot. Ila sishangai humu wajinga mpo wengi sana na kibaya zaidi huwa mnatoa mawazo yenu. Bora mngekua kimya
Mkuu usilazimishe mkyundu kutafuna muwa basi wajulishe watu kile unachokijua wewe wapate Elimu kutoka kwako Kisha tulinganishe na maelezo ya upande wa pili.
 


Milango inavyofunguka kwenye ATR wakati wa emergency. Hamna mahali wanaposema lazima awepo mtu nje wa kuifungua.

Amandla...
 
CCM ni wajinga. Ila wanatawala kwa sababu wapinzani wao ni wajinga zaidi.

Ndege imepata ajali kwa uzembe, watu wamepoteza maisha, hakuna aliewajibika, hakuna hatua zilizochukuliwa kuhakikisha hili halijirudii tena. Ila hoja kuu ya wapinzani imekua "Majaliwa alifungua mlango au hakufungua". PATHETIC!

Elekezeni nguvu kwa serikali, iwajibike kwa yaliyotokea na ihakikishe hayatokei tena!

CCM wamemkuza Majaliwa ili awe smoke screen kwenye hii ajali, ili msihoji mambo ya maana kama alivyofanya mkuu Barafu. Na nyinyi mnafuata kama vipofu, kelele zote kwa majaliwa badala ya kuuliza serikali inatenga bajeti kiasi gani kwa jeshi la zimamoto na uokozi!

Kumjadili Majaliwa badala ya kuhoji hali ya viwanja vyetu vya ndege, au utayari wa vikosi vya uokoaji, ni kudhihirisha kua wapinzani ni wajinga kuliko hao wajinga wanaotuongoza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…