Ajali ya ndege Bukoba ni matokeo ya uzembe na kufanya kazi kwa mazoea.Tuwajibishane ili tusirudie makosa

Ajali ya ndege Bukoba ni matokeo ya uzembe na kufanya kazi kwa mazoea.Tuwajibishane ili tusirudie makosa

Analysis ya barafu ni funga kazi. Ngoja nipumzishe fuvu nikiamka bdae I will dot the i's and cross the t's.
Hawa watu wenye ujuzi na mambo ya Usimamizi wa miradi ya ndege ndio wanapewa kupewa vitengo. Lakini hapa kwetu si ajabu kukuta mtu anayesimamia viwanja vya ndege hana utaalam wowote na mambo ya ndege! Barafu mama kuonesha akupe majukumu akutoe huko uliko!
 
Mkuu asante kwa maelezo mazuri
Ila kwa namna ulivyolielewa hili sakata naomba ufafanuzi wa haya;

1.Ilikuwaje marubani wakafa wakati Majaliwa aliongea nao mpaka akawaaga?

2.Hii ndege ilipataje ajali? Je iliamua kutua kwenye kiwanja ndio ikasukumwa kuelekea majini au ilizunguka(Orbiting)kama ulivyosema kisha rubani kwa kuishiwa mafuta akaamua atue baharini au akiwa anazunguka ilipata hitilafu ndio ikaangukia ziwani?

3.Je ndege ina milango mingapi? Na mlango wa ndege uliofunguliwa ni upi?ni huo ambao hugeka ngazi kuna mlango mwingine?

Nadhani baada ya hizi ripoti kutoka kuna haja ya Majaliwa kuhojiwa upya ili kuondoa mkanganyiko,maana sisi tunamuona kama shujaa lakini kuna mambo aliyosema bado yanaligawa taifa kama aaminike au asiaminike,Kumbuka hata waziri Mbarawa kasema mlango ulifunguliwa na watumishi kwa ndani na sio kwa kushirikiana na wavuvi,sidhani kama amelisema hili kwa bahati mbaya hasa akijua kabisa kwamba tayari Majaliwa alishasema yeye ndio aliupiga mlango kwa kasia ukafunguka na kuanza kuwatoa watu.
 
Ukila biskuti za bangi usitegemee kumuelewa mbobezi wa Aviation anapochanganuwa mambo.

Wewe nenda boomplay huko ndio level yako utawaelewa kina Mboso, Zuchu na Diamond.
Mbobezi my foot. Ila sishangai humu wajinga mpo wengi sana na kibaya zaidi huwa mnatoa mawazo yenu. Bora mngekua kimya
 
Hiyo ripoti ningeshangaa kama ingetoka tofauti na hivyo.

Ni aibu sana kwa mamlaka husika kukubali uzembe wao.

Lazima tu Majaliwa aaibishwe.
 
Swali ndugu yangu Barafu.

Kwenye issue ya Mlango unaozungumziwa ulikuwa ni ule wa "emmergency exit" au hii milango ya kawaida ya mbele na nyuma?.

Je "emmergency exit" doors za ATR zinafunguka kwenda chini na kuwa ngazi balanced na small hydraulic cylinders left and right au ni ule unaofunguka kwa kwenda juu ukifyatua latch kwaPicha ya kwanza mlango wa mbele anapoonekana rubani kasimama ni mlango wa kuweka mizigo,karibu na panga boi ni exit door na kule nyuma ndio mlango wa kushukia ambao ndio ngahuu mlango wa nyuma kwa ajili ya huduma ya Catering,mwenye gari ya Catering ndio anaingizia hapo chakula.

Mlango wa ATR unafunguka kwa kwenda chini,upo sahihi,unakuwa supported kushoto na kulia.
Swali ndugu yangu Barafu.

Kwenye issue ya Mlango unaozungumziwa ulikuwa ni ule wa "emmergency exit" au hii milango ya kawaida ya mbele na nyuma?.

Je "emmergency exit" doors za ATR zinafunguka kwenda chini na kuwa ngazi balanced na small hydraulic cylinders left and right au ni ule unaofunguka kwa kwenda juu ukifyatua latch kwa ndani?
 
Sidhani kama kuna mtu anabeza mchango wa wavuvi katika kuokoa maisha ya abiria. Watu wanachopinga ni kumfanya mmoja wao ndio steling wakati waliohusika ni wengi. In fwakt kwa kufanya hivyo mchango wa wavuvi wenzake walioshirikiana nae ulipuuzwa kiasi cha kuwafanya walalamike. Aidha, mchango mkubwa wa mhudumu na yule jamaa nao ulionekana hauna maana sana kwa sababu tayari tulishamtunuku Majaliwa u Superman.

Nina shaka na hilo unalosema kuwa mlango wa ATR ni lazima awepo mtu nje ndio ufunguke. Unataka kutuambia kuwa ajali ikitokea mahali ambapo hamna mtu wa kusaidia kutoka nje (porini, baharini n.k.) waliomo ndani watapoteza maisha yao? Utakuwa ni emergency exit ya ajabu sana ambayo haiwezi kutumika mpaka mtu afungue kwa nje.

Amandla...
 
Yamesikika mengi kuhusiana na ajali ya ndege ya PW kule Bukoba,yamesemwa mengi na wanasiasa na wasio wanasiasa.Kila mtu anasema la kwake,lakini moja na lenye uhakika ni kuwa,kuna watu wanapaswa kuwajibishwa kwa ajali ya ndege Bukoba.

Tumepoteza ndugu,marafiki na jamaa zetu kwa sababu ya uzembe na mazoea(bussiness as usual).Tuliowapa dhamana ya kusimamia viwanja vyetu vya ndege,tunawatengea bajeti kila mwaka katika kitengo cha majanga na uokozi na wale tunaowategemea katika ulinzi na usalama wa nchi,wanapaswa kuwajibika.

Tuwapuuze wanasiasa aina ya wale wa zambarau ambao wanaingiza siasa na kubeza juhudi za wavuvi katika uokozi.Ni mtu asiye na shukrani ndio atashindwa kutambua nafasi ya kijana Majaliwa katika kuwanusuru wale wote walionusurika.Ni ajabu pia hata wale walionusirika kuikosa pumzi ya dunia hii,wanaingia katika mkumbo wa kuona "walijiokoa" kwa juhudi zao,na sio msaada wa wavuvi aina ya Majaliwa.

Ingetokea Majaliwa amekufa,tusingekuwa na shukrani...kuumia kwake na kuzimia kwake katika harakati za kufanya uokozi,ni jambo kubwa kuliko hata kuanza kumshambulia kwa kuingiza siasa za kijinga.Ni ajabu sana kukuta kuna wanasiasa wanapitia katika "kick" ya kutoona ushiriki wa Majaliwa katika uokozi.

Uwanja wa ndege Bukoba,ni moja kati ya viwanja vya Tanzania vilivyo katika Code 3C inayotambuliwa na ICAO(International Civil Aviation Organization).Code 3C ni kiwanja chenye uwezo wa kuchukua ndege size ya kadi kama vile Dash8-Q400 na ATR42 na hata ATR72.ni kiwanja kinachofanya kazi kwa mawio na machweo kwa siku 7 za week.

Hivyo tukio linalotokea saa 08:45 asubuhi ni tukio ambalo linapaswa kukuta watu wapo ofisini katika maandalizi ya kuona lolote linaweza" kutokea.

Kwa kadili ya dodoso za Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania,kikosi cha Zimamoto kilichopo Bukoba kinadondokea katika Category 5,na Category inayotaka RFFS(Rescue and Fire Fighting Services) iwe na gari lenye uwezo wa kubeba lita za ujazo 5800(?),na kama kiwanja kipo kando ya ziwa au mto basi wafanyakazi wa uokozi wawe na mafunzo ya uogeleaji na respiratory equipments za kutosha.Na uwanja unapaswa kuwa na nguvu kazi isiyopungua wafanyakazi 25.

Zaidi ya hapo,inatakiwa wakati wa kutua na kupaa kwa ndege,gari la zimamoto linatakiwa kufanya huduma ya "standby" kwa kutumia taxway na wakati wa kuruka gari la zimamoto linatakiwa kufanya "escort".

Hili ni swali la kujiuliza,Je uwanja wa Bukoba lina gari la zimamoto lenye uwezo wa kubeba maji lita ngapi?kuna wafanyakazi wangapi katika kituo cha Zimamoto uwanja wa ndege?na je askari wa uokozi waliopo wana mafunzo ya uogeleaji endapo ndege imetokea kudondoka katika maji?Au wote wanasubiri watokee akina "Majaliwa" kuokoa?Ni ajabu sana kuona hata wanasiasa aina ya yule wa Zambarau anataka kuifanya ajenda ya Majaliwa kuwa kubwa na ya kupigia siasa badala ya kushukuru kazi na jitihada za kijana yule.

Tunapoona kuwa ndege ilishindwa kutua kwa zaidi ya mara moja,Je kitengo cha Zimamoto na uokoaji kilijiandaaje?Kulikuwa na gari eneo la Airside likiwa "standby" kufanya uokozi?

Annex 14 ya ICAO inanukuliwa ikisema “ The principal objective of a rescue and fire fighting service is to save lives”. Airports need a RFFS/ARFF even during “periods of reduced activity, irrespective of the number of movements” because accidents happen… when they happen


Meneja wa Uwanja na kamanda wa Zimamoto/Msimamizi wa kamandi ya Jeshi la Zimamoto uwanja wa Bukoba wanatakiwa wajibu hitaji hili la kiviwango.
Kama ulivyo uwanja wa Lindi unaotegemea Control Tower kutoka Mtwara au uwanja wa Nachingwea nyumbani kwa Waziri Mkuu unavyotegemea Control tower kutoka Mtwara mjini,ndivyo ilivyo kwa Bukoba na Mpanda.

Kwa miaka mingi marubani wengi katika uwanja wa Bukoba wamekuwa wakishuka kwa kutumia "uzoefu",na uzoefu unakuwa na umuhimu sana katika nyakati zenye hali mbaya ya hewa.Unapokuwa na kiwanja chenye "scheduled Flights" na huazingatii kufuata viwango vya kuwa na mnara wa kuongoza ndege,ajali ya aina hii ikitokea,mwanasiasa mwenye uweledi,hapambani na Majaliwa,anatakiwa kupambana na wale wenye bajeti na dhamana ya kukamilisha hayo yanayotakiwa.

Mjadala kuwa "nani alifungua mlango au nani hakufungua" ni mjadala wa aibu sana.Majaliwa angeweza kupoteza uhai ama kwa kuzama wakati akiwaokoa abiria au kwa kuumia.Kwa wanaoujua "scene" ya eneo la ajali,maelezo ya Majaliwa yamenyooka kabisa.Panapokuwa na ajali ya ndege,kama ambavyo emergency drill hufanyika,lazima kuwepo na "On Scene Commander" au "Incident Commander".Huyu anakuwa na kipaza sauti na hutoa muongozo wa nini kufanyike.Kwa hiyo Majaliwa anaposema kuna "mtu alikuwa ana kipaza sauti" alinikataza nisivunje kioo kumtoa rubani,basi huyu ni "Incident Commander".

Mtiririko huu wa maongezi unaonyesha jinsi bwana mdogo huyu alivyojitoa kuokoa maisha ya watu.Rubani alikufa sababu Bukoba hakuna control Tower,alikosa mawasiliano ya moja kwa moja ya nini afanye na msaada gani apate.Mawasiliano ya Walkie Talkie Radio ambayo hutumika tu na wafanyakazi wa Precision Bukoba tena wasio na uzoefu wa kazi hiyo yasingetosha kuweka uimara wa taarifa kati ya rubani na walio nje.Ni uzembe mkubwa sana kupoteza watu waliopata ajali mita 500 toka kwenye threshold,mita 500 ni vacinity ya aerodrome.NI AIBU SANA.

Mlango wa ATR42 unafungukia kwa nje,anayefungua anapaswa kuwa ndani,lakini ni lazima apate msaada wa mtu wa nje.Sababu unapoufungua mlango wa ATR42 hutumika kama mlango na ndio ngazi pia ya kuingia na kutoka katika ndege.Hivyo unapofunguliwa mtu wa nje ni lazima auishike,aweke stabilize stick itakayofanya mlango usijifunge.

Hii ni hata katika nchi kavu ndege inapokuwa uwanjani...NI LAZIMA MTU WA NJE AUSHIKE NA KUWEKE STABILIZE STICK...hata kama walifungua abiria na muhudumu,kwa nature ya mlango-ngazi wa ATR42 isingewezekana kufunguka kama hakuna mtu nje,tena katika maji.Hapa ndio Majaliwa anaposema alitumia kasia kuufungua,ili watu watoke.Hata katika hili kuna watu wanataka mashindano na Majaliwa.

Ni mambo ya aibu sana...tushukuru sana akina Majaliwa na wavuvi wengine,kama ndege hii ingedondoka mita 1500 kutoka uwanjani,hata hao waliodhani ni abiria tu na mhudumu wa ndege ndio walifungua mlango na kutokea wangekuwa wanaongea mengine.Tuwaache hawa akina Majaliwa,tuwashukuru na tafadhali tusiwaingize katika mjadala unaoelekea kuwa na aina ya kutokushukuru msaada wao.Watu waliojitolea tu kwanini wasimangwe?hao wenye mafunzo,hao wenye kitengo cha dharula na majanga na wanaotengewa bajeti walifika masaa 6 baada ya ajali wakiwa na boti iliyo na mafuta kidogo na hawakuwa na mitungi.

Ni bahati mbaya kuwa jambo hili limebebwa kisiasa,ili kufunika udhaifu wa wanasiasa.Ajali ya mita 500,tena ndani ya maji katika kiwanja ambacho ndege ni "!scheduled Flight" ni aibu sana kumpoteza rubani na abiria.Kama tungekuwa na control tower,jeshi imara la zimamoto na uokozi maanake wakati ndege ikifanya orbiting(kuzunguka angani kutafuta uwezekano wa kutua) maanake team nzima ya kiwanja,ambayo miezi kadhaa nyuma ilishatumia zaidi ya milioni 20 kuandaa igizo la uokoaji(emergency drill) tena kwa kuhusisha hadi watu wa makao makuu waliokula posho na marupurupu na kuitangazia dunia kuwa wapo tayari kukabiliana na ajali muda wowote.Ni ajabu sana kama hizi roho za watu zilizopotea hazitaondoka na watu...Yaani kwanza katika dhana ya uwajibikaji,mpaka sasa kuna watu walitakiwa kuwa wameshawajibishwa.

USHAURI:
i)Serikali ifanye hima kwa kushirikiana na Tanzania Civil Aviation Authority ambao ndio wamepewa dhamana ya kusimamia usafiri wa anga kuweka control tower katika uwanja wa Bukoba ambao unapokea ndege ambazo ni "scheduled Flights".Ni aibu sana kukosa huduma hii.

ii)Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika viwanja vya ndege liboreshwe.Na ikiwezekana ili kufuata Standard za ICAO kwa uzuri,Mamlaka ya Viwanja vya Ndege iachiwe kitengo hiki kwa 100% ili iweze kuwasimamia na pengine kuwawajibisha wafanyakazi wa kitengo hiki kwa asilimia zote.Kama ilivyo Mamlaka ya Bandari au Zimamoto KIA.Zimamoto za Viwanja vilivyo chini ya TAA ni waajiliwa wa Wizara ya mambo ya ndani,na sio TAA kwa hiyo mamlaka ya kinidhamu inakuwa Wizara ya Mambo ya ndani,kumekuwa na ugumu wa kuwawajibisha hata kama mtu anakuja kazini saa 4 badala ya saa 07:30 kwa sababu Meneja wa kiwanja sio mamlaka yake ya nidhamu.Hili liangaliwe kwa mapana.Kuna udhaifu mkubwa sana katika Kitengo cha Zimamoto na uokoaji katika viwanja vya ndege.

iii)Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tz(TAA) ifanye kwa mkazo zoezi la emergency drill kwa umakini na sio mazoea.Ni aibu kuwa Bukoba ndani ya miezi 10 ilifanya emergency drill lkn ajali imetokea na imeonyesha kuwa kiwanja hakikuwa tayari kabisa katika kukabiliana na majanga.Watu wanafanya kazi kwa mazoea,na hii imedhirika baada ya ajali hii kutokea.Ukiangalia records za mtoa taarifa kutoka katika ofisi ya operations kwenda kwa wadau wengine na ule mtiririko wa mawasiliano,inaonyesha TAA bado ina staffs ambao wanafanya kazi kama wapo sokoni tu.Training ziongezwe ili kuwajengea uwezo wafanyakazi.

iv)Serikali ione umuhimu wa kuweka control towers katika viwanja ambavyo ndege hutua mara kwa mara.

v)Serikali ihakikishe inaboresha vituo vya zimamoto katika viwanja vya ndege,magari ya kisasa na askari walio na mafunzo.Vifaa vya zimamoto kama vile foam na horse za kutosha.Na kwenye maeneo ya mwambao mwa maji,wakati wa kutua na kuruka kwa ndege kuwepo na ushirikiano wa kutosha na askari wa majini kuwa na utayari wa uokozi mara tu ajali inapotokea.Hii ni kwa aina ya viwanja kama Bukoba na Mwanza.

Ikumbukwe kuwa ndege kuahirisha kutua au kuruka sababu ya hali ya hewa mbaya,hakuna uhusiano na ubovu wa kiwanja.Sehemu nyingi duniani kwenye viwanja vilivyo bora,bado ndege hushindwa kutua.Ni ajabu kuona mwanasiasa aina ya Lugangila kuhusisha hali ya hewa na ubovu wa kiwanja.

Pole kwa manusura,na pole kwa wafiwa na Mungu awapokee wote waliopoteza maisha yao mita 500 kutoka uwanjani.
Umemaliza kila kitu mkuu barafu hujawahi kuniangusha tangu enzi za mlazo mapera mengi na migori zaidi zambarau umewamaliza Sasa tujadili hizo power bank zilizowasili za TRC tukisubiri mabehewa sijui yatafika lini shukrani
 
Mbobezi my foot. Ila sishangai humu wajinga mpo wengi sana na kibaya zaidi huwa mnatoa mawazo yenu. Bora mngekua kimya
Jipigepige kifuani huku ukijisemesha Mimi ni mchawi kasoro vitendea kazi ndio sina.

Hapa JF ni barafu ndio amekuwa ngumu wa kuchambuwa industry ya Aviation unless kama ndio leo umeanza kuna Uzi wake.

Fistula inatibika wahi matibabu.
 
Zitto Kabwe .. Erythrocyte

Mko wapi mlambwe za Uso hizi.
Maana kwa Uchwara wenu!

Mnaishi Siasa kwa kutumia Matukio badala ya "Hoja" na "Sera!"

Mnaishi Siasa kwa kutafuta Wachawi badala ya Ufumbuzi!

Mnaishi Siasa kwa kutafuta Riziki zenu binafsi badala ya Wapiga kura wanaovifanya vyama vyenu viendelee kuwepo!

Mnaishi Siasa kwa kuangalia "Political Mileage",badala ya "Political Influences!"

Huyu Member barafu amekuja wakati muafaka na sahihi kabisa!

barafu amekuja kuondoa mzizi wa Fitina kwenu team Sumu!

Hatujui kama yoote hii,ilikuwa dhidi ya Majaliwa mkubwa au Majaliwa mdogo?

Hongera sana barafu Mtanzania mwenye uwezo wa kujenga hoja yenye Mashiko na wenye kuelewa Tumekuelewa!

Wasiokuelewa ni wale tu waliolewa Majungu!
Nimekuja , unasemaje ?
 
Walamba asali awatopenda kusikia haya, wana hoja zao eti kadi ya CUF ndugu barafu umerudisha lini? Awakumbuki tunaongelea ishu za kitaifa na sio kadi za chama.
 
Mbobezi my foot. Ila sishangai humu wajinga mpo wengi sana na kibaya zaidi huwa mnatoa mawazo yenu. Bora mngekua kimya
Mkuu usilazimishe mkyundu kutafuna muwa basi wajulishe watu kile unachokijua wewe wapate Elimu kutoka kwako Kisha tulinganishe na maelezo ya upande wa pili.
 




Milango inavyofunguka kwenye ATR wakati wa emergency. Hamna mahali wanaposema lazima awepo mtu nje wa kuifungua.

Amandla...
 
CCM ni wajinga. Ila wanatawala kwa sababu wapinzani wao ni wajinga zaidi.

Ndege imepata ajali kwa uzembe, watu wamepoteza maisha, hakuna aliewajibika, hakuna hatua zilizochukuliwa kuhakikisha hili halijirudii tena. Ila hoja kuu ya wapinzani imekua "Majaliwa alifungua mlango au hakufungua". PATHETIC!

Elekezeni nguvu kwa serikali, iwajibike kwa yaliyotokea na ihakikishe hayatokei tena!

CCM wamemkuza Majaliwa ili awe smoke screen kwenye hii ajali, ili msihoji mambo ya maana kama alivyofanya mkuu Barafu. Na nyinyi mnafuata kama vipofu, kelele zote kwa majaliwa badala ya kuuliza serikali inatenga bajeti kiasi gani kwa jeshi la zimamoto na uokozi!

Kumjadili Majaliwa badala ya kuhoji hali ya viwanja vyetu vya ndege, au utayari wa vikosi vya uokoaji, ni kudhihirisha kua wapinzani ni wajinga kuliko hao wajinga wanaotuongoza!
 
Back
Top Bottom