Ajali ya treni Tabora, Rais Samia aagiza uchunguzi ufanyike na hatua zichukuliwe

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
287991612_702602054143986_770673014468231179_n.jpg
Rais Samia Suluhu ametuma salamu za rambirambi kutokana na tukio la treni ya abiria kuanguka na kusababisha vifo vya watu kadhaa eneo la Malolo Mkoani Tabora, pia ameagiza uchunguzi ufanyike kubaini chanzo na hatua zichukuliwe.

Ajali hiyo ilitokea jana Juni 22, 2022 ambapo baadaye Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa alisema kulikuwa na hujuma baada ya kukuta kipande cha reli kiliondolewa na kisha kurudishwa kwa kuegeshwa katika eneo la ajali.

“Nawapa pole wafiwa, nawaombea marehemu wapumzike kwa amani na majeruhi wapone haraka. Nimeagiza tuliowapa dhamana ya eneo hili kufuatilia na kubaini chanzo, na kuchukua hatua stahiki,” – Rais Samia.

Pia soma - TRC yasema Ajali ya treni ya abiria Juni 22, 2022 iliyosababisha vifo na majeruhi ni HUJUMA
 
Kwa Kiongozi wa nchi (Rais) kuanza Kukimbilia kuhisi kuwa kuna Hujuma ni Haatari sana kwani hakuna Mtanzania makini asiyejua kuwa huko TRL kuna Matatizo makubwa tu lakini pia hata Miundombinu yake nayo si ile iliyo Maadhubuti kwa Usalama wa Usafirishaji wa Abiria. Naogopa tu huu Mzigo wa Lawama usije ukawaangukia Raia (Wakazi) Wema wa hilo eneo ambalo Ajali hiyo imejitokeza ili Wahusika Kukwepa Uwajibikaji wao.
 
Kwa Kiongozi wa nchi ( Rais ) kuanza Kukimbilia kuhisi kuwa kuna Hujuma ni Haatari sana kwani hakuna Mtanzania makini asiyejua kuwa huko TRL kuna Matatizo makubwa tu lakini pia hata Miundombinu yake nayo si ile iliyo Maadhubuti kwa Usalama wa Usafirishaji wa Abiria. Naogopa tu huu Mzigo wa Lawama usije ukawaangukia Raia ( Wakazi ) Wema wa hilo eneo ambalo Ajali hiyo imejitokeza ili Wahusika Kukwepa Uwajibikaji wao.
Rais yupo informed kukuzidi wewe na anajua anachokifanya.
 
Wakuu

Tren haiwezi ua wanne tu!!
Yaani iachie mabehewa halafu mabehewa yapinduke Hadi kulalia watu waliopo nje na kuwaua!
Tujiulize je waliokuwa nje walikuwa wangapi?na walio ndani wasafiri ni wangapi!!?
 
Haya pia ni matokeo ya sisi kama taifa kukosa umoja, yaani kutokuwa wamoja.

Hii ilisababishwa na kuchangiwa sana na utawala wa dictator JPM ambapo aliwatreat baadhi ya watu kama wanyamulenge,

na hii ni cha mtoto ngoja iyo reli mpya ianze ndio ccm na washing wenzenu mtajua hamjui.
 
Kwa Kiongozi wa nchi (Rais) kuanza Kukimbilia kuhisi kuwa kuna Hujuma ni Haatari sana kwani hakuna Mtanzania makini asiyejua kuwa huko TRL kuna Matatizo makubwa tu lakini pia hata Miundombinu yake nayo si ile iliyo Maadhubuti kwa Usalama wa Usafirishaji wa Abiria. Naogopa tu huu Mzigo wa Lawama usije ukawaangukia Raia (Wakazi) Wema wa hilo eneo ambalo Ajali hiyo imejitokeza ili Wahusika Kukwepa Uwajibikaji wao.
Maneno yako yananipa tafakuri kubwa
 
Katika watu wenye uelewa mkubwa jf GENTAMYCINE na mrangi wamo. Wakisema kitu usikimbilie kujibu haraka haraka.
Soma Mara mbili, vuta pumzi Kisha kunywa maji ndio uanze kujibu.
Mkuu Asante kwa Kuutambua Uwezo wangu ila kwakuwa Umenisifia hivi jiandae Kisaikolojia kuambiwa hii ID ni yangu pia.

Cc: Prince Kunta
 
Haya pia ni matokeo ya sisi kama taifa kukosa umoja, yaani kutokuwa wamoja.

Hii ilisababishwa na kuchangiwa sana na utawala wa dictator JPM ambapo aliwatreat baadhi ya watu kama wanyamulenge,

na hii ni cha mtoto ngoja iyo reli mpya ianze ndio ccm na washing wenzenu mtajua hamjui.
Aliyemuelewa huyu anieleweshe
 
Katika watu wenye uelewa mkubwa jf GENTAMYCINE na mrangi wamo. Wakisema kitu usikimbilie kujibu haraka haraka.
Soma Mara mbili, vuta pumzi Kisha kunywa maji ndio uanze kujibu.
Narudia kama kuna mtu yupo well informed nchi hii ni Sponsor au CIC full stop and long brake.
 
Wakuu

Tren haiwezi ua wanne tu!!
Yaani iachie mabehewa halafu mabehewa yapinduke Hadi kulalia watu waliopo nje na kuwaua!
Tujiulize je waliokuwa nje walikuwa wangapi?na walio ndani wasafiri ni wangapi!!?

Mkuu ulitaka iue wa ngapi. Unaweza niambia watu waliokua nje ni wangapi. Maana me nafahamu reli upita porini porini?
 
“Nawapa pole wafiwa, nawaombea marehemu wapumzike kwa amani na majeruhi wapone haraka. Nimeagiza tuliowapa dhamana ya eneo hili kufuatilia na kubaini chanzo, na kuchukua hatua stahiki,” – Rais Samia.
Lugha ya namna hii katika maswala kama haya..., ahaaa, acha nisiseme mengi.
Inasikitisha sana. Na kama ni kweli ajali hiyo ni hujuma..., hujuma kwa nani?
 
Kwa Kiongozi wa nchi (Rais) kuanza Kukimbilia kuhisi kuwa kuna Hujuma ni Haatari sana kwani hakuna Mtanzania makini asiyejua kuwa huko TRL kuna Matatizo makubwa tu lakini pia hata Miundombinu yake nayo si ile iliyo Maadhubuti kwa Usalama wa Usafirishaji wa Abiria. Naogopa tu huu Mzigo wa Lawama usije ukawaangukia Raia (Wakazi) Wema wa hilo eneo ambalo Ajali hiyo imejitokeza ili Wahusika Kukwepa Uwajibikaji wao.
Nafahamu una fahamu kuwa, Rais pekee ndio kiongozi anaye pokea taarifa nyingi zaidi ziwe za kiuchumi, siasa, usalama na ulinzi!.

Katika hili sina shaka kuwa, tamko lake halikuja tu ivi ivi, ispokuwa ana abc za chanzo cha ajali, au anataka kujua nini chanzo cha ajali.

Kiufupi ni kuwa, Raisi huchukizwa na kifo cha mtanzania yeyote! na anatuonesha yeye ni Mtanzania na habagui maskini au Tajiri.
 
Haya mambo ya kuunda unda tume sijui za kuchunguza madubwana gani ni matumizi mabaya ya pesa ya umma Kuna muda hawa viongozi wetu watakaunda hata tume ya kuchunguza uji wanao kunywa wanafunzi na watu walio magereza.
 
Back
Top Bottom