TANZIA Ajali yaua 5 na kujeruhi 36 Shinyanga

TANZIA Ajali yaua 5 na kujeruhi 36 Shinyanga

Screenshot_20220903-085723.png
 
Trafiki sio suluhu ya ajali, huko barabarani kuna vipande vingi tu hawakai hao trafiki...

Mara nyingi sababu ya ajali za kugongana uso kwa uso ni uzembe katika kuendesha au mechanical failure, hivi vitu havizuiwi na uwepo wa askari barabarani bali uduni wa mifumo ya ukaguzi
Sahii kabisa, watu waache ushabiki
 
BREAKING NEWS

Watu watano wamepoteza maisha hapo hapo na wengine 36 wamejeruhiwa vibaya kwenye ajali iliyohusisha basi la kampuni ya Najmunisa T 413 DAY kugongana uso kwa uso na Fuso T 123 DJH katika eneo la Ibadakuli Shinyanga.

Mzee Kinana kama nakuona vile

Chanzo: ITV

====

Update

Watu watano wamepoteza maisha na wengine 36 kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya Najmunisa T 413 DAY kugongana uso kwa uso na Fuso T 123 DJH katika eneo la Ibadakuli Shinyanga, leo Septemba 3, 2022.-

Majeruhi wote wamekimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Leonard Nyandahu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Taarifa zaidi kuhusu ajali hii zitazidi kukujia.
Yaani watu wanaroho ngumu Sana na wepesi wa kusahau,watu bado kweli wanapanda mabasi ya kampuni hiyo? Tuliibatiza jina inaitwa
MAJINI YA MUSA.
 
Hili basi lilinipita juzi pale Moveck linaelekea Mbezi tayari kwa Safari, nikawa namwambia Mtu kuwa hii kampuni umefanikiwa kufanya maboresho makubwa kwenye speed, dah naamini ni Ajali kama Ajali zingine tu
Mungu wetu aendelee kuwapigania na kuwakumbatia mnaosafirisafiri🙏
 
BREAKING NEWS

Watu watano wamepoteza maisha hapo hapo na wengine 36 wamejeruhiwa vibaya kwenye ajali iliyohusisha basi la kampuni ya Najmunisa T 413 DAY kugongana uso kwa uso na Fuso T 123 DJH katika eneo la Ibadakuli Shinyanga.

Mzee Kinana kama nakuona vile

Chanzo: ITV

====

Update

Watu watano wamepoteza maisha na wengine 36 kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya Najmunisa T 413 DAY kugongana uso kwa uso na Fuso T 123 DJH katika eneo la Ibadakuli Shinyanga, leo Septemba 3, 2022.-

Majeruhi wote wamekimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Leonard Nyandahu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Taarifa zaidi kuhusu ajali hii zitazidi kukujia.
Polisi kukaa barabarani na kuchukua rushwa haijawahi kuwa suluisho la ajali!! Kinachotakiwa ni elimu ya kutosha Kwa madereva ili kupunguza ajali!! By the way hata Nchi zilizoendelea ajali zipo Cha Muhimu pia ni kuomba Mungu, RIP wahanga
 
Sasa ni muda wa kuanza kufikiria kujenga Highways za kueleweka. Hizo barabara za kuunga mikoa ziwe na njia hata 3 kwenda na 3 kurudi, magari yasiingiliane. Na kusiwe na zebra wala taa barabarani zaidi ya madaraja kama vivuko na njia za exit kutoka kwenye hiyo barabara kuu.

Wasomi wetu na mainjia muende UJERUMANI mkajifunze AUTOBAHN highway inavyofanya kazi na ilivyojengwa kwa ufanisi mkubwa. Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom