TANZIA Ajali yaua 5 na kujeruhi 36 Shinyanga

TANZIA Ajali yaua 5 na kujeruhi 36 Shinyanga

Alhmdllh mpwa wangu kanusurika. Madereva muda mwingine huwa wanajisahau sana.
 
Madereva wa malori ni wababe si mchezo japo madereva wa mabasi nao ni watu wa kuforce sana wakiwa barabarani.

Dereva wa bus anaona kabisa gari la mbele yake limekaribia lakini anavuta moto hadi apenye sasa wakati mwingine hesabu zinafeli tena akikutana na wa lori ndo kabisa wa roli anaweza kuona mwenzake kapiga hesabu vibaya lakini anakanyaga moto wakutane au bus lipenye kwa shida ilimradi liwalo na liwe yaan ni jeuri kweli kweliqs
😂😂😂😂😂 hapo inakuwa jino kwa jino dereva kashapagawa anataka amuwahi mkewe ww unaleta mambo ya kitoto
 
R.I.P JPM ulipochukua nchi ulikuta kuna ajali nyingi sana ukalifanyia kazi ajali zikapungua sana lakini sasa hivi zinarudi kwa kasi
 
hivi Madereva wanakuaga wamesinzia au nini hua kinatokea mpaka magari yanagongana uso kwa uso ?
 
Inasikitisha sana na tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Yani uso kwa uso useme ni udhembe !!!????

binafsi nasema wazee wa kafara walikua mzigoni.

Naam, zipo ajali za kugongana magari uso kwa uso zinazosababishwa na uzembe "wreck less driving"...

Kulazimisha kufanya overtaking eneo lisilo salama ni moja ya chanzo cha huo uzembe...
 
Trafiki sio suluhu ya ajali, huko barabarani kuna vipande vingi tu hawakai hao trafiki...

Mara nyingi sababu ya ajali za kugongana uso kwa uso ni uzembe katika kuendesha au mechanical failure, hivi vitu havizuiwi na uwepo wa askari barabarani bali uduni wa mifumo ya uukagu

Safiri salama ukirudi Dom tutafutane, mi ntaenda jumanne Dar, kikubwa Dua na TOBA
Nashukuru mkuu nimefika salama nimeanza safari SAA 3 asubuhi na nimeingia DAR SAA 12 jioni...
Ila Kwa style ambayo nimeona Leo jinsi madereva wa serikali wanavyosumbua njiani hawa jamaa wanajiona wao ndiyo barabara ya kwao hawana hata taadhari kabisaa
 
Usiogope Muamini Mungu ,ajali nyingi zinasababishwa na nguvu za Giza ajali halisi aiwezi kuuwa inajeruhi tu,Mungu sio katili kama wengi wanavyofikiri.kwenye basi inahitajika mwenye mamlaka mmoja tu dhidi ya nguvu za Giza ajali haiwezi kutokea .Muamini Mungu utabaki salama.Zaburi 91:3,16 .Mimi nasafiri Kila week mara mbili safari za dar -mwz-arsh lazima nifike namjua Mungu ninaye mwamini.
Pamoja mkuu hata hivyo nimefika salama nashukuru MUNGU
 
Breaking News

Watu watano wamepoteza maisha hapo hapo na wengine 36 wamejeruhiwa vibaya kwenye ajali iliyohusisha basi la kampuni ya Najmunisa T 413 DAY kugongana uso kwa uso na Fuso T 123 DJH katika eneo la Ibadakuli Shinyanga.

Mzee Kinana kama nakuona vile

Chanzo: ITV

====

Update

Watu watano wamepoteza maisha na wengine 36 kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya Najmunisa T 413 DAY kugongana uso kwa uso na Fuso T 123 DJH katika eneo la Ibadakuli Shinyanga, leo Septemba 3, 2022.-

Majeruhi wote wamekimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Leonard Nyandahu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Taarifa zaidi kuhusu ajali hii zitazidi kukujia.

acha ujinga hata kama matraffic wapo ajali zipo tu uliona wapi trafic wakawepo usiku
 
Omba usikutane na Tanker inawahi beba mzigo na dereva ana kimeo cha deni la mafuta
Umenikumba Jana tupo kwenye Costa ya abiria aisee ilipita tanker moja ina over take , adi nikaogopa ,nadhani ilikuwa empty inawahi mzigo uko daresalamu.
 
Back
Top Bottom