TANZIA Ajali yaua 5 na kujeruhi 36 Shinyanga

Sahii kabisa, watu waache ushabiki
 
Yaani watu wanaroho ngumu Sana na wepesi wa kusahau,watu bado kweli wanapanda mabasi ya kampuni hiyo? Tuliibatiza jina inaitwa
MAJINI YA MUSA.
 
Hili basi lilinipita juzi pale Moveck linaelekea Mbezi tayari kwa Safari, nikawa namwambia Mtu kuwa hii kampuni umefanikiwa kufanya maboresho makubwa kwenye speed, dah naamini ni Ajali kama Ajali zingine tu
Mungu wetu aendelee kuwapigania na kuwakumbatia mnaosafirisafiri🙏
 
Polisi kukaa barabarani na kuchukua rushwa haijawahi kuwa suluisho la ajali!! Kinachotakiwa ni elimu ya kutosha Kwa madereva ili kupunguza ajali!! By the way hata Nchi zilizoendelea ajali zipo Cha Muhimu pia ni kuomba Mungu, RIP wahanga
 
Sasa ni muda wa kuanza kufikiria kujenga Highways za kueleweka. Hizo barabara za kuunga mikoa ziwe na njia hata 3 kwenda na 3 kurudi, magari yasiingiliane. Na kusiwe na zebra wala taa barabarani zaidi ya madaraja kama vivuko na njia za exit kutoka kwenye hiyo barabara kuu.

Wasomi wetu na mainjia muende UJERUMANI mkajifunze AUTOBAHN highway inavyofanya kazi na ilivyojengwa kwa ufanisi mkubwa. Naomba kuwasilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…