Good Father
JF-Expert Member
- Feb 28, 2014
- 10,321
- 18,574
Hilo basi laonekana bovu
Malori yatafutiwe sehemu ya kupita
BREAKING NEWS
Watu watano wamepoteza maisha hapo hapo na wengine 36 wamejeruhiwa vibaya kwenye ajali iliyohusisha basi la kampuni ya Najmunisa T 413 DAY kugongana uso kwa uso na Fuso T 123 DJH katika eneo la Ibadakuli Shinyanga.
Mzee Kinana kama nakuona vile
Chanzo: ITV
====
Update
Watu watano wamepoteza maisha na wengine 36 kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya Najmunisa T 413 DAY kugongana uso kwa uso na Fuso T 123 DJH katika eneo la Ibadakuli Shinyanga, leo Septemba 3, 2022.-
Majeruhi wote wamekimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Leonard Nyandahu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Taarifa zaidi kuhusu ajali hii zitazidi kukujia.
Kumbe unajua! Sasa imekuwaje unasema ajali ni mambo ya kawaida?Na ufinyu wa akili pia kudhani Kinana kasababisha ajali.
Hawa ni wale trafiki wala rushwa, kwa sasa wanafanya kazi ya ulinzi kwenye mabenki, pale wanaondoka kama walivyokuja, hivyo wana hasira sanaWhat a pitful loss.
Mungu awapokee marehemu wetu.
nimeshangazwa kuona umemalizia post yako in bias manner. Ina maana zile ajali nyingi za kutisha huko nyuma zilitokea wakati Trafiki polisi hawapo barabarani?
Yani uso kwa uso useme ni udhembe !!!????Trafiki sio suluhu ya ajali, huko barabarani kuna vipande vingi tu hawakai hao trafiki...
Mara nyingi sababu ya ajali za kugongana uso kwa uso ni uzembe katika kuendesha au mechanical failure, hivi vitu havizuiwi na uwepo wa askari barabarani bali uduni wa mifumo ya ukaguzi
Safiri salama ukirudi Dom tutafutane, mi ntaenda jumanne Dar, kikubwa Dua na TOBANinasoma habari hii nikiwa hapa Dodoma nikianza safari ya kuelekea DAR hakika hizi safari ndefu ni MUNGU mwenyewe Tu anahitajika....namwomba MUNGU anifunike Kwa mikono yake na mimi
Tulia NapeKinana alimwaga ugali wako una hasira nae?
Ajali haizuiwi na trafiki tena kwa Bongo uwepo wa trafiki sehemu kubwa hakuna wanachosaidia zaidi ya kufanya makusanyo yao binafsi.
Barabara zetu ni nyembamba na sehemu zingine lami ni chakavu, mabonde, mashimo ya hapa na pale unakuta magari yanapishana kwa shida sana
Mabasi yanasifa sana anakuletea bodi ili umpisha sasa akikutana na dereva kichaa ndio haya yanatokea huwa always wanaharaka na wanafhani wana hatimiliki ya barabaraYani uso kwa uso useme ni udhembe !!!????
binafsi nasema wazee wa kafara walikua mzigoni.
Poti tuliza kipele hapo centralYes kinana ni kilaza kama mwigulu tu
Hela hakuna, meanwhile...Tumefunga njia ya Dar- Tunduma ili kuadhimisha MwengeSasa ni muda wa kuanza kufikiria kujenga Highways za kueleweka. Hizo barabara za kuunga mikoa ziwe na njia hata 3 kwenda na 3 kurudi, magari yasiingiliane. Na kusiwe na zebra wala taa barabarani zaidi ya madaraja kama vivuko na njia za exit kutoka kwenye hiyo barabara kuu.
Wasomi wetu na mainjia muende UJERUMANI mkajifunze AUTOBAHN highway inavyofanya kazi na ilivyojengwa kwa ufanisi mkubwa. Naomba kuwasilisha.
Mwenzetu kagoma kuwaza sahihiHawa ni wale trafiki wala rushwa, kwa sasa wanafanya kazi ya ulinzi kwenye mabenki, pale wanaondoka kama walivyokuja, hivyo wana hasira sana
Usalama wowote unaanzia na wewe/sisi wenyeweTrafiki sio suluhu ya ajali, huko barabarani kuna vipande vingi tu hawakai hao trafiki...
Mara nyingi sababu ya ajali za kugongana uso kwa uso ni uzembe katika kuendesha au mechanical failure, hivi vitu havizuiwi na uwepo wa askari barabarani bali uduni wa mifumo ya ukaguzi
Tulia Nape
Mle ndio unakutana na V8 zilizopagawaTena iyo njia ya Dom to Dar ...Ni balaa naa nusu ..inakuwaga na ajali Sana.
Wote hao wendawazimu tuMadereva wa malori ni wababe si mchezo japo madereva wa mabasi nao ni watu wa kuforce sana wakiwa barabarani.
Dereva wa bus anaona kabisa gari la mbele yake limekaribia lakini anavuta moto hadi apenye sasa wakati mwingine hesabu zinafeli tena akikutana na wa lori ndo kabisa wa roli anaweza kuona mwenzake kapiga hesabu vibaya lakini anakanyaga moto wakutane au bus lipenye kwa shida ilimradi liwalo na liwe yaan ni jeuri kweli kweli
Usiogope Muamini Mungu ,ajali nyingi zinasababishwa na nguvu za Giza ajali halisi aiwezi kuuwa inajeruhi tu,Mungu sio katili kama wengi wanavyofikiri.kwenye basi inahitajika mwenye mamlaka mmoja tu dhidi ya nguvu za Giza ajali haiwezi kutokea .Muamini Mungu utabaki salama.Zaburi 91:3,16 .Mimi nasafiri Kila week mara mbili safari za dar -mwz-arsh lazima nifike namjua Mungu ninaye mwamini.Ninasoma habari hii nikiwa hapa Dodoma nikianza safari ya kuelekea DAR hakika hizi safari ndefu ni MUNGU mwenyewe Tu anahitajika....namwomba MUNGU anifunike Kwa mikono yake na mimi