Ajali yaua Wanandoa Dodoma, kichanga wao anusurika

Ajali yaua Wanandoa Dodoma, kichanga wao anusurika

Hata kuweka tuta moja sehemu hatarishi ni mpaka watu wafe na waandamane
Sehemu za kivuko wanawekaga alama!
Kama unakaribia kivuko unatakiwa usipite mazimaaaa,simama sikilizia

Any way poleni kwa wafiwa

Ova
 
Oooh jmn nakihurumia sana kichanga wazazi wote wawili wamekufa ndani ya siku moja.Mungu akapiganie jmn dunia hii bila wazazi tena kwa umri huo sio rahisi
 
Watu wawili mke na mume wamefariki dunia kwenye ajali iliyohusisha gari ndogo na treni katika makutano ya reli, Kata ya Tambukareli, Dodoma.

Akizungumzia marehemu hao Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Ibenzi Ernest amesema walipokea mwili wa mwanamke Furaha Rashid huku mume wake Hussein Chilala akiwa katika hali mbaya.

“Ilikuwa majira ya saa tatu usiku mwanamke tulimpokea akiwa tayari amefariki, lakini mwanaume alikuwa na hali mbaya na wakati anapatiwa huduma akafariki muda mfupi baadaye,” amesema Ibenzi.

Ibenzi amesema marehemu waliumia zaidi kichwani hali iliyosababisha kuvuja damu nyingi na kupoteza maisha.

Hata hivyo, katika ajali hiyo ambapo marehemu walikuwa na mtoto wao anayekadiriwa kuwa na mwaka mmoja, Ibenzi amesema walimpokea mtoto huyo akiwa mzima na alisema amechukuliwa na mama yake mdogo kwani hakuumia sehemu yoyote.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema atamrudia mwandishi baada ya kumaliza kikao.

MWANANCHI
Kama Mkono wa MUNGU umeweza kumuokoa huyu mtoto bas hakika najua atakuja kuwa na mafanikio ingawa atapitia changamoto nyingi sana.
 
Tena sikuiz Kuna automated system za kila namna... ndio hivo tena labda kiongozi mkubwa yamkute ndio tupate hiyo neema...
Halafu hii Njia ndio Kuelekea Zile Nyumba Walipo Wabunge na baadhi ya Mawaziri
 
Kuna ajali moja staff mwenzetu amebeba milipuko ya migodini(baruti na fataki zake) kwenye hilux halafu kagonga treni .Mungu saidia kichwa cha gari tu ndo kilibamizwa vilipuzi havikuguswa .
Kama vingepata friction na impact yoyote ingekuwa historia duniani , hiyo shimo ingechimbwa hapo ni balaa.
 
Watu wengi ulimbukeni wa AC kwenye Gari ndiyo unawaponzaga! Hata Kama kuna hatari mbele,hata wakipigiwa kelelee hawasiki maana vio vyote vimefungwa hadi juu!!
Eeh! AC ni Ulimbukeni Kumbe?
 
Engineer Hussein chilala na mkewe wote wamefariki. Wameacha kichanga chao, inauma sana
Haya maisha kuna wakati yanaumiza na kutafakarisha sana.

Seems jamaa ndiyo alikuwa ameshaji-set aanze kula mema ya nchi lakini ndani ya dakika tu amepotea na mpendwa wake,Mungu awarehemu marehemu hako katoto akalinde kakue salama hakuna lingine tunaweza kusema kwa sasa.
 
Acha tu maisha bana haya eleweki.Jamaa kavuta gar na wife na mtt tayr kumbe ndo history inashia hapo.
 
Kuna ajali moja staff mwenzetu amebeba milipuko ya migodini(baruti na fataki zake) kwenye hilux halafu kagonga treni .Mungu saidia kichwa cha gari tu ndo kilibamizwa vilipuzi havikuguswa .
Kama vingepata friction na impact yoyote ingekuwa historia duniani , hiyo shimo ingechimbwa hapo ni balaa.
Mwamba alichomoka salama?
 
Dah aiseeee MUNGU yupo na malaika wake wanafanya kazi kisawa sawa. Tazama amemlinda mtoto huyo katika ajali ambapo angeweza na yeye kutoweka ila atakuja kuhadithiwa tu huko baadae.
 
Kivuko cha reli sio siri kama ni driver makini unajua nini cha kufanya iwe treni ipo au haipo. Mtu anaesema treni imemshtukiza, na kelele na muungurumo wote ule sio rahisi uwe hujaskia unless hauko makini.
Tatizo tunafunga vioo vyote ili tufaidi AC na hapo mziki upo sayti ya juu sana hio treni tutaisikia saa ngap
 
Nimemsikia mwanasheria wa PT usalama barabarani akidai madereva wote nchini wawe wanatembea na vyeti vyao vya kuhitimu mafunzo ya udereva pamoja na leseni zao.

Tunakoelekea watataka watu tutembee na madaftari ya notisi za driving schools.

BTW😛ale Isaka (Bandari kavu) palikuwepo na kizuizi (barrier) pamoja na kibanda cha mfanyakazi anayefunga na kufungua barabara.
Siku hzi hayupo
 
Watu wengi ulimbukeni wa AC kwenye Gari ndiyo unawaponzaga! Hata Kama kuna hatari mbele,hata wakipigiwa kelelee hawasiki maana vio vyote vimefungwa hadi juu!!
Na ukute ndani ya gari wameaachia sound kubwa!!
 
Back
Top Bottom