Ajali yaua Wanandoa Dodoma, kichanga wao anusurika

Hata kuweka tuta moja sehemu hatarishi ni mpaka watu wafe na waandamane
Sehemu za kivuko wanawekaga alama!
Kama unakaribia kivuko unatakiwa usipite mazimaaaa,simama sikilizia

Any way poleni kwa wafiwa

Ova
 
Oooh jmn nakihurumia sana kichanga wazazi wote wawili wamekufa ndani ya siku moja.Mungu akapiganie jmn dunia hii bila wazazi tena kwa umri huo sio rahisi
 
Kama Mkono wa MUNGU umeweza kumuokoa huyu mtoto bas hakika najua atakuja kuwa na mafanikio ingawa atapitia changamoto nyingi sana.
 
Tena sikuiz Kuna automated system za kila namna... ndio hivo tena labda kiongozi mkubwa yamkute ndio tupate hiyo neema...
Halafu hii Njia ndio Kuelekea Zile Nyumba Walipo Wabunge na baadhi ya Mawaziri
 
Kuna ajali moja staff mwenzetu amebeba milipuko ya migodini(baruti na fataki zake) kwenye hilux halafu kagonga treni .Mungu saidia kichwa cha gari tu ndo kilibamizwa vilipuzi havikuguswa .
Kama vingepata friction na impact yoyote ingekuwa historia duniani , hiyo shimo ingechimbwa hapo ni balaa.
 
Watu wengi ulimbukeni wa AC kwenye Gari ndiyo unawaponzaga! Hata Kama kuna hatari mbele,hata wakipigiwa kelelee hawasiki maana vio vyote vimefungwa hadi juu!!
Eeh! AC ni Ulimbukeni Kumbe?
 
Engineer Hussein chilala na mkewe wote wamefariki. Wameacha kichanga chao, inauma sana
Haya maisha kuna wakati yanaumiza na kutafakarisha sana.

Seems jamaa ndiyo alikuwa ameshaji-set aanze kula mema ya nchi lakini ndani ya dakika tu amepotea na mpendwa wake,Mungu awarehemu marehemu hako katoto akalinde kakue salama hakuna lingine tunaweza kusema kwa sasa.
 
Acha tu maisha bana haya eleweki.Jamaa kavuta gar na wife na mtt tayr kumbe ndo history inashia hapo.
 
Mwamba alichomoka salama?
 
Dah aiseeee MUNGU yupo na malaika wake wanafanya kazi kisawa sawa. Tazama amemlinda mtoto huyo katika ajali ambapo angeweza na yeye kutoweka ila atakuja kuhadithiwa tu huko baadae.
 
Kivuko cha reli sio siri kama ni driver makini unajua nini cha kufanya iwe treni ipo au haipo. Mtu anaesema treni imemshtukiza, na kelele na muungurumo wote ule sio rahisi uwe hujaskia unless hauko makini.
Tatizo tunafunga vioo vyote ili tufaidi AC na hapo mziki upo sayti ya juu sana hio treni tutaisikia saa ngap
 
Siku hzi hayupo
 
Watu wengi ulimbukeni wa AC kwenye Gari ndiyo unawaponzaga! Hata Kama kuna hatari mbele,hata wakipigiwa kelelee hawasiki maana vio vyote vimefungwa hadi juu!!
Na ukute ndani ya gari wameaachia sound kubwa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…