Tonytz
Senior Member
- Jul 18, 2022
- 159
- 1,142
UTANGULIZI
Nchini kwetu Tanzania kwa sasa kumekuwa na mwendelezo wa ajali mbalimbali ikiwemo za magari barabarani, mashuleni kuwepo na ajali za moto ambao vyanzo vyake havifahamiki kwa haraka. Ajali hizi zinaweza kusababishwa na hali ya kimazingira, kiufundi au kibinadamu. Hapa ina maana kuwa ajali inaweza kusababishwa kutokana na matatizo ya kiufundi kwenye chombo chenyewe au mazingira yaliyopo lakini pia hata mapungufu ya kibinadamu. Lakini binadamu yawezekana kuwa ndiyo chanzo kikubwa cha utokeaji wa ajali hasa za barabarani. Katika Makala hii nitaziangazia zaidi ajali za magari barabarani zinazochukua nafasi kubwa kwa sasa nchini kwetu Tanzania. Katika kuangazia ajali hizo, nitajikita hasa katika kuelezea vyanzo vya ajali, wenye dhamana ya kusimamia usalama barabarani, je wanatenda kazi zao (wajibu) wao ipasavyo? Je, ni kwa namna gani ajali hizo zinaathiri maendeleo katika nyanya mbalimbali (kiuchumi, kijamii na nyenginezo). Na mwisho nitajadili kwa uchache kuwa nini kifanyike ili kuepukana na athari za ajali za barabarani na namna ya kuziepuka.
VYANZO VYA AJALI ZA MAGARI BARABARANI.
Kama nilivyokwisha tangulia kusema hapo awali kuwa vyanzo vya ajali barabarani husababishwa na hali ya kibinadamu, kimazingira na kiufundi. Sasa tuzitazame kwa kina kwa kuangalia sababu zinazopelekea utokeaji wa ajali za magari ya barabarani;
Kwanza, uzembe unaosababishwa na madereva. Mara nyingi ajali hizi husababishwa na madereva wenyewe ambapo uzembe huo husababishwa na kuendesha gari huku akiwa amelewa, kutumia madawa ya kulevya kupitiliza, kuendesha gari huku akitumia simu pamoja na kutozingatia alama za barabarani.
Pili, ubovu wa miundombinu. Barabara zetu hapa nchini nyingi hazina ubora hususani za vijijini na hata zile zenye lami huwa hazina kiwango cha ubora cha lami. Hali hii hpelekea ajali kwa kiwango kikubwa sana.
Tatu, usimamizi mbovu wa sheria za barabarani, hili nalo limekuwa tatizo sugu sana hapa nchini kwetu. Waliopewa dhamana ya kuzisimamia sheria za barabarani hawawajibiki ipasavyo. Kutokana na kutokuwajibika huko ndipo hupelekea ajali nyingi. Mfano askari wa barabarani kutowadhibiti madereva wanaoendesha mwendo kasi, wasiozingatia alama za barabarani na wanaoendesha huku wakitumia simu.
Nne, mwendokasi, kwa sasa madereva wa magari hasa mabasi ya mikoani hutumia mwendokasi hatarishi sana pasipo kujali kama amebeba binadamu ambao ndiyo nguzu kazi ya Taifa kimaendeleo. Madereva wengine hudiriki kushindana barabarani, hii si sawa kabisa.
Tano, hofu na woga wa abiria(wanajamii) kutoa taarifa kwa kitengo husika hasa kwa madereva wanaovunja sharia za barabarani. Watu tumekuwa waoga sana katika kusema ukweli au kuweka wazi uharifu kwa faida ya maisha yetu.
Sita, magari kubeba mizigo mikubwa kulinganisha na ubora wa barabara zetu. Hili linaharaibu sana miundombinu ya barabara amabapo hali ikiwa endelevu husababisha utokeaji wa ajali ambazo hupelekea vifo vya watu wengi sana.
Hizo ni baadhi tu visababishi vya ajali za magari barabarani. Ijapokuwa kuna siku nilipokuwa nahojiana na dereva mmoja anayefanya safari zake kutoka Ifakara kwenda Dar es salaam kuwa nini hasa kinasabisha ajali za magari barabarani, pamoja na kutaja sababu miongoni mwa hizo lakini pia aliongezea kwa kusema kafara za mabosi au wamiliki wa magari pia ni chanzo cha ajali za magari barabarani.
JE WALIOPEWA DHAMANA YA KUSIMAMIA USALAMA BARABARANI WANATIMIZA WAJIBU WAO?
Hili ni swali la muhimu sana kujiuliza hapa, kuwa kwanini ajali zitokee huku sababu ikiwa ni mwendokasi, ulevi, au gari kujaza abiria wengi kupita kiasi ilihali askari wa barabarani wapo? Nilifanya mahojiano na dereva mmoja juu ya hilo akanipa visa vingi sana ambapo ni dhahiri wenye dhamana ya kusimamia usalama barabarani hawatimizi wajibu wao ipasavyo. Sasa tuanze tuangalia ni kwanini wenye dhamana ya kusimamia usalama barabarani hawatimizi wajibu wao ipasavyo, ambao sababu hizi husukumwa na hali ya maisha, tamaa, tabia, kukosa uzalendo na mengineyo.
Kwanza, askari wengi wa barabarani wanachukua rushwa kwa madereva vya vyombo vya usafiri (magari, pikipiki na bajaji). Utakuta gari imejaza abaria wengi, lakini utakuta anashuka kondakta na kupeleka kitu kidogo na hao askari hata hawahoji wanairuhusu gari itembee, hii ni hatari sana.
Pili, suala la kujuana au mazoea. Siku moja nikiwa kwenye basi kutoka sehemu moja kijini kwangu kwenda mjini, tukiwa katikati ya safari ambapo gari lilikuwa inakaribia sehemu ambapo askari wa barabarani hukaa kukagua magari, nikashuhudia kondakta akitoa simu na kupiga huku akisema “ oya poti, upo checkpoint au yupo nani” nikajua kabisa anampigia akari mwenye mazoea naye ili asipate usumbufu.
Tatu, kukosa uzalendo, Hali hii huwafanya wenye dhamana wengi kutotimiza wajibu wao wa kuokoa maisha ya raia.
Nne, kwenye suala la utoaji leseni kwa madereva. Hili linaendeshwa kiholela san asana. Dereva hajapitia mafunzo au ameonekana hajafanya vema ila taasisi au idara husika inampa mtu huyo leseni kinyume na sharia, hapa tunategemea nini?
AJALI HIZI ZINAATHIRI VIPI MAENDELEO YA NCHI YETU.
Hapa nitaeleza kwa kifupi sana athari za ajali katika maendeleo yetu hapa nchini Tanzania.
Kwanza, ajali inapotokea watu wengi hupoteza uhai, hivyo hupunguza nguvu kazi ya Taifa ambapo watu hao wangeweza kufanya shughuli mabalimabali za kimaendeleo hapa nchini.
Pili, huaribu miundombinu yetu, hali hii hukwamisha sekta ya usafirishaji ambayo ndiyo kiungo cha maendeleo kwa fursa zote. Mfano ajali ikitokea na kuharibu daraja la barabara kuu, nadhani hakutokuwa na usafirishaji wa haraka kama ilivyotokea jirani na mto wami na mkuranga.
Tatu, hukwamisha serikali katika kutimiza mipango elekezi yenye kipaumbele kwa maendeleo ya nchi. Ikumbukwe ikitokea ajali serikali huchukua hatua za kukarabati miundombinu na hivyo pengine kutumia pesa ambayo ilikuwa itumike kwa jambo linguine la kimaendeleo.
(Picha kutoka mtandaoni-JF)
NINI KIFANYIKE?
Kwa pamoja tuhakikishe tunasimaina haya;
Kwanza, kuwepo na usimamizi mzuri wa sharia za barabarani
Pili, jamii kupewa elimu Zaidi na kutoa taarifa kwa uvunjifun wowote wa sharia za barabarani
Tatu, miundombinu ijengwe kwa kiwango kinachotakiwa ili kuepusha ajali.
Nne, sheria kali zichukuliwe kwa askari wa usalama barabarani pale inapogundulika wameenda kinyume na wajibu wao.
HITIMISHO.
Hayo na mengine mengi yatasaidia sana kupepusha ajali na hivyo Taifa kuwa na watu wengi ambao kwa namna moja na nyingine kwa viwango vyetu vya uwajibikaji inaweza kupelekea maendeleo ya nchi yetu. Seriakali ijikite kutimiza wajibu wao kwa vitendo na siyo askari wa usalama barabarani kuchuka elfu mbili mbili za madereva. Wawe wazalendo na walizike na mishahara yao. Wazingatie uhai wa watu na siyo kujali matumbo yao.
Picha: Mtandao

Upvote
98