Ajinyonga baada ya kuamka usiku na kukuta mkewe ametoroka nyumbani

Ajinyonga baada ya kuamka usiku na kukuta mkewe ametoroka nyumbani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
c75650390cac90fcad1c7fd80efd7d1a

Gurian Adolf-Sumbawanga

WATU wanne wamefariki dunia katika matukio tofauti wilayani Nkasi mkoani Rukwa, likiwemo la mwanaume kujinyonga kwa kutumia kamba ya nailoni baada ya kugundua mke wake amemtoroka usiku na kwenda kwa mwanaume mwingine.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Justine Masejo, alisema katika tukio la kwanza lililotokea Novemba 24 saa 6 usiku, mwanaume aliyefahamika kwa jina la Rafael Leonard (49) mkazi wa Kijiji cha Bumanda Kata ya Korongwe wilayani Nkasi, alijinyonga chumbani kwake kwa kutumia kamba ya nailoni.

Alisema kabla ya kujinyonga alikuwa amelala na mkewe alipo shtuka usingizini alikuta mke wake ametoroka na kwenda kwa mwanaume mwingine ndipo alipokasirika na kupatwa na wivu wa kimapenzi na kuamua kujinyonga.


Katika tukio la pili lililotokea Novemba 23 saa 8 mchana, katika Kijiji cha Mwai Kata ya Namanyere, kamanda huyo alisema watu wawili waliofahamika kwa majina ya Japhet Jelazi (25) na Peter Silunde (8) walikufa papo hapo baada ya kupigwa na radi wakiwa wamejikinga mvua chini ya mti.

Alisema Jelazi ambaye alikua akilima shambani na Silunde aliyekuwa akichunga mbuzi baada ya kuona mvua imeanza kunyesha, waliamua kukimbilia chini ya mti ili kujikinga wasilowane na mvua hiyo ndipo radi ilipo wapiga na kufariki dunia papo hapo.

Katika tukio la mwisho lililotokea katika Kitongoji cha Milundikwa Kijiji cha Nkundi, Kamanda Masejo alisema mtoto Emiliana Kauzeni (3) alikufa maji baada ya kutumbukia kwenye dimbwi la maji yaliyokuwa yametuama nyuma ya nyumba yao kufuatia mvua zinazo endelea kunyesha mkoani humo.

Alisema mtoto huyo alikuwa akicheza peke yake alizunguka nyuma ya nyumba, alikwenda kwenye dimbwi la maji na kisha kutumbukia, na kufariki huku mama yake akiwa amelala ndani akijipumzisha kutokana na uchovu wa shughuli za kilimo.

Kamanda huyo alisema hakuna watu wanaoshikiliwa kufuatia matukio hayo bali aliwaasa wakazi wa mkoa huo kuwa waangalifu katika kipindi hiki cha mvua za masika ili kujiepusha na madhara yanayoweza kujitokeza.
 
"Alisema kabla ya kujinyonga alikuwa amelala na mkewe alipo shtuka usingizini alikuta mke wake ametoroka na kwenda kwa mwanaume mwingine ndipo alipokasirika na kupatwa na wivu wa kimapenzi na kuamua kujinyonga"
Mkewe ndiye kashuhudia hayo? au walimuuliza marehemu? maana muelezeaji ni kama alikuwepo.
 
maisha ni fumbo! Mungu atuhurumie tu!
 
"Alisema kabla ya kujinyonga alikuwa amelala na mkewe alipo shtuka usingizini alikuta mke wake ametoroka na kwenda kwa mwanaume mwingine ndipo alipokasirika na kupatwa na wivu wa kimapenzi na kuamua kujinyonga"
Mkewe ndiye kashuhudia hayo? au walimuuliza marehemu? maana muelezeaji ni kama alikuwepo.
[emoji28][emoji28]
 
Mkuu unaujua uchungu wa mke!!?

Hayo maneno anatakiwa aandike paroko!
Mkuu uhai ni zaidi ya mke, marehemu hajafikilia wangapi wanamhitaji.Wanawake waliojazana hawa ufikie uamuzi wa kujinyonga? ona Sasa yeye kafa mwanamke waachia wenzie na yeye kaacha huzuni kwa familia yake,Kwanza ningekuwa naweza mrudisha ningempa kipondo kizito kwa uamuzi mbovu Kama huo.
 
Huyu aliyejinyonga ni popoma kweli kweli, mungu amlaze anapostahili

Yeye kajinyonga kafwa, huku watu wanatomba tu kiuhuru.
Kuna baadhi ya mijitu haifai kuwa wanaume kabisa, hii ni fedheha kubwa.
 
Utamu unatofautiana mama, jamaa unakuta kashatest sample mbalimbali lakini huyo mkewe yuko vizuri, ufundi pia unatofautiana na Wanamume hapo ndipo tunakwama..

Yes na hao wa vijijini wapo nachulo...kitu hakina mambo ya miski sijui maspray ya k mara vurugu gan!😉😉! Ngoma lazima ikeshe!ila sijajiua bado
 
Yes na hao wa vijijini wapo nachulo...kitu hakina mambo ya miski sijui maspray ya k mara vurugu gan!😉😉! Ngoma lazima ikeshe!ila sijajiua bado

huwezi kwasababu sio Mwanaume wewe..
Ukiyafikilia ya chumbani ni hatari, watu mafundi mama unatamani uwe unashinda nyumbani tu.. Ukijinyoosha tu unalazwa chini inapigwa massage, mwanga mdogo, mafuta ya nazi au machicha ya nazi, kamziki kwambali..baada ya hapo abdala kichwa wazi anasagwa kichwani mdogo mdogo hahahaahaahahaha lazima umnunulie mama Harrier latest version au kitu cha Audi Q7.. HAHAHAHHA dunia tamu asikwambie mtu..
 
Back
Top Bottom