Ajira 17,412 kwa kada za Elimu na Afya zatangazwa. Wananchi wenye sifa wahimizwa kuomba nafasi

Ajira 17,412 kwa kada za Elimu na Afya zatangazwa. Wananchi wenye sifa wahimizwa kuomba nafasi

Hii nchi ubabaishaji mwingi sana...
Waziri mzima unatoa matamko ambayo hayajathibiti!
Tangazo linasema wamefungulia dirisha la kutuma maombi kuanzia tarehe 20/04 lakin cha ajabu hadi sasa mfumo umefungwa!

Nashauri mamlaka zetu ziwe zinafanya maandalizi ya kutosha kwanza na kuhakikisha kila kitu kiko sawa ikiwemo mfumo wenyewe kabla ya kutoa matamko/press release za kisenge kama hizi
🤝🤝
 
Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa, amewataka Watanzania wenye sifa waombe nafasi za kazi kuanzia leo, baada ya serikali kutangaza nafasi za ajira 17,412, kwa kada ya elimu na afya.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Aprili 20, 2022, Bungeni Dodoma, wakati akihitimisha hoja ya bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

"Nimshukuru Rais Samia kwa kutoa idhini ya ajira za watumishi wa afya na elimu 17,412, ambapo nafasi 9,800 ni za walimu na 7,612 ni kada za afya ambao wataajiriwa mwaka huu wa fedha 2021/22, nitoe taarifa rasmi kwamba Watanzania wenye sifa wanaelekezwa kuomba kuanzia leo, maombi ya ajira hizi ni bure," amesema Waziri Bashungwa.
Iviiiiii kada ni mbili tu ajira ma afyaaa baaaas
 
System haipo vizuri
Nataka kusign up hata sioni sehemu ya kubonyeza
 
Iviiiiii kada ni mbili tu ajira ma afyaaa baaaas
We umesoma kozi ipi.. hiz Ajira mpya zimetoka kwa kada zenye kipaumbele.. kama umesoma uhasibu Kuna Ajira za TRA Omba chap..
Kuna kuna Kilimo, mifugo na sheria hizi sijui watatangaza lini maombi Ila zilikuwa na idadi yake chache kimtindo
 
Mfumo siuelewi elewi...

Hivi tuliomba mwaka jana tukakosa tunatumia username na passwords zilezile au ndo tunafungua upyaa
 
Ajira za Sheria zitasimamiwa na Mahakama kuu..? maana Hadi leo hatujaona matangazo ya zile Ajira na walisema ziko 500+

Hata watu wa Kilimo na mifugo.. zote kimya...
 
Ajira za Sheria zitasimamiwa na Mahakama kuu..? maana Hadi leo hatujaona matangazo ya zile Ajira na walisema ziko 500+

Hata watu wa Kilimo na mifugo.. zote kimya...

Kama afya na ualimu wametoa leo, kwanini usiamini kuwa sheria wanaweza kutoa kesho au siku nyingine?

Ulitaka zitoke siku moja!
 
Hiv inakuaje kama nimeomba ajira za wizara ya afya then nikaomba na ajira za TAMISEMI ?
 
Back
Top Bottom