msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 863
- 1,534
Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu amesema kuna Watu wamejitokeza mitaani ambao wanawadanganya Walimu ambao hawajaajiriwa kuwa wanatakiwa kutoa Tsh. Milioni moja ili wapate ajira kwa haraka kwani nafasi hizo hazitatangazwa na Serikali bali zitatolewa kisirisiri.
Waziri Ummy ameyasema hayo mapema hii leo wakati akiwa katika ziara ya kikazi katika Shule ya Sekondari Zingibari Wilayani Mkinga, Tanga.
Waziri Ummy amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kufanya uchunguzi ili kujua kama Watu hao wapo ndani ya Wizara au nje na kuwachukulia hatua za kisheria haraka.
Ummy pia amesema ajira hizo zikiwa tayari basi watatangaza kwa utaratibu unaotakiwa na kila mmoja anayehitaji atafuata utaratibu na hakuna atakayependelewa.
Chanzo: MillardAyoUPDATES
Pia soma,
1. TAMISEMI ninyi ndio chanzo cha rushwa na utapeli ajira za walimu
2. Anton Mtweve ni nani huko TAMISEMI?
3. TAMISEMI: Acheni kuajiri kimya kimya, mchakato wa ajira 6000 za walimu ufanyike kwa uwazi