Ajira hakuna ila kazi zipo nyingi sana vijana tutumie akili

Wengi wanasoma kwa ajili ya kuajiriwa. Shida ndo inaazia hapo.. 🙂 🙂
Hakuna mtu anatoka katika familia masikini anayesoma akajiajiri, kujiajiri ni matokeo otherwise hakuna familia amsikini inayoweza kupoteza pesa yote kumsomesha mtoto hadi chuo halafu akajiajiri kwenye shughli za genge, kilimo, bodaboda. Kama ni hayo angeanza mapema tu kuwa mkulima au boda boda maana uhitaji kuwa na degree kufanya hayo.
 
Fikra za kikenge sana za kukaririshwa na wasira et al, yani kila mtu akawe kubarua na bodaboda? Hao waliojaa hd njia za kupita hamna hawatoshi?
 
. Ulicho zungumza hiki ndo uhalisia wenyewe ambao serikali na wadau wa elimu wanatakiwa kuliweka wazi..

. Nyumbani kuna mifugo ya kutosha, lakini kwa vile hatuna maoni ya mbali unaamua kumpeleka mwanao akosomee ualimu au nurse, kwa nini Mtoto asipelikwe tu moja kwa moja kusomea mifugo ili aje kuendeleza mifugo ya nyumbani??
 
Hivi mtu ukimaliza chuo unashindwa kwenda kujifunza ujuzi wowote kama kushona, kusuka, kufuma, kupika keki n.k

Hadi ukae nyumbani uanze kulia. Haya subirini serikali iwatafutie kazi huko Katavi, Mpimbwe.
 
Wazazi wako wana mbuzi wangapi wakusomeshe uje kufuga? Wabongo kwa kujitoa ufahamu kwenye keyboard hamjambo! Wazazi wa kawaida wana kuku na ng’ombe 3-20 wakiuza wakusomeshe wanabaki na nini ili ulete huo ujuzi wako kuwasaidia kuwafuga kwa tija? Mnapokaririshwa tumieni akili kdg zinazobaki kujiuliza na kujijibu
 
Watu wanachukulia simple sana hivi vitu, na wengi wanaosema hivyo wao ukiwaambia wakafanye hizo kazi hawawezi.
Wabunge tu wakipoteza ubunge wanalia lia. Wassira kazeeka lakini bado anang'ang'ana.
Kujiajiri si kitu rahisi plus TRA, mara selikali za mitaa wote wana vitozo na kodi ambavyo muda mwingine vinaua biashara.
 
Ety watu wanaunda umoja wa waalimu wasio na ajira(NETO)

Hivi kazi zote hizi kitaa wewe una shahada unashindwa kufanya mpaka ulalamike??

Ajira hakuna ila kazi ni nyingi tumieni akili
Yaweza kuwa hiyo Ndo fursa yenyewe,
Wacha vijana waichangamkie
 
Kuajiriwa sio Serikalini tu, heshimuni hizo ajira zenu mnazozipata shule binafsi
 
Wabunge tu wakipoteza ubunge wanalia lia. Wassira kazeeka lakini bado anang'ang'ana.
Kujiajiri si kitu rahisi plus TRA, mara selikali za mitaa wote wana vitozo na kodi ambavyo muda mwingine vinaua biashara.
Kabisa mkuu, shida ya viongozi wetu wakishaingia kwenye system wanajifanya kusahau kabisa na life la mtaa... Inshort mtaa ni mgumu sana so hata ukimuona mtu ameanzisha biashara yake na imesimama hadi kuanza kuajiri unapaswa umuheshimu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…