Gatabhanya
JF-Expert Member
- Nov 16, 2024
- 2,644
- 5,178
Kazi ya ualimu ni ya hovyo sana unashinda kutwa nzima unapiga fujo na kukimbizana na watoto.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uko kwenye ualimu kumejaaa sasa ndio maana wameweka usaili kuwapunguza vilaza...basi subiri hapo hapo ufe.Kwahiyo mnataka wimbi lote la wasio na ajira waende wakusaidie fundi? Hivi mmeshawahi kukaa na kupiga hesabu hata za roughly tu ya vijana wanaomaliza vyuo kwa Kila mwaka na ajira zinazotoka huwa ziko na uwiano gani?.
Unadhani hao vijana wote wakienda kwenye hiyo bodaboda thing, huo upande utakuaje? Na vipi kuhusu hao wadada nao umewafikiria? Au mnataka na wao waanze kuamka asubuhi waende huko kwenye kusaidia fundi au kukaa vijiweni kula vichwa?
Hizo ni kazi?Saidia fundi kwenye ujenzi.
Bodaboda...
Kwani hao ni waafrika? Nenda kwao india ukajionee. Kule hukuti mwafrika akiranda randa mitaani.Mfano jamii za wahindi hauwezi kukuta wanaranda randa mitaani
Mtaani sio pagumu ..sema kichwa chako ndio kigumu thus why na usaili umefeli😂😂😂.Kabisa mkuu, shida ya viongozi wetu wakishaingia kwenye system wanajifanya kusahau kabisa na life la mtaa... Inshort mtaa ni mgumu sana so hata ukimuona mtu ameanzisha biashara yake na imesimama hadi kuanza kuajiri unapaswa umuheshimu sana.
Unadhani kila mtu anaweza kuajiri (Ukizingatia hizo self employment ni Uchuuzi na Udalali kuanzia Serikali hadi muuza uji kitaa) ?Wengi wanasoma kwa ajili ya kuajiriwa. Shida ndo inaazia hapo.. 🙂 🙂
😂😂😂Ety watu wanaunda umoja wa waalimu wasio na ajira(NETO)
Hivi kazi zote hizi kitaa wewe una shahada unashindwa kufanya mpaka ulalamike??
Ajira hakuna ila kazi ni nyingi tumieni akili
😂😂Ety watu wanaunda umoja wa waalimu wasio na ajira(NETO)
Hivi kazi zote hizi kitaa wewe una shahada unashindwa kufanya mpaka ulalamike??
Ajira hakuna ila kazi ni nyingi tumieni akili
Kumbe ualimu ni deal.Ety watu wanaunda umoja wa waalimu wasio na ajira(NETO)
Hivi kazi zote hizi kitaa wewe una shahada unashindwa kufanya mpaka ulalamike??
Ajira hakuna ila kazi ni nyingi tumieni akili
Mkuu Mimi sijawahi kwenda kwenye hizo usahili thing tangu nimalize chuo miaka kadhaa iliyopita na wala sitawahi kufanya hivyo.Mtaani sio pagumu ..sema kichwa chako ndio kigumu thus why na usaili umefeli😂😂😂.
Mtaani mambo mepesi sana.. biashara zipo nyingi..fremu za kutosha..wateja wa kutosha...mamb ya kusema mtaani pagumu ukome!!!
Kikwete atoe mbinu aliyotumia kuajiri waalimu wote.
Atakua mccm huyu! Wanajua kila tatizo linatatuliwa kwa nyundo tu nayo ni wasira na polisi, msamehe bure! Out of contact with the reality, anaongea mambo ya 1971 wakati tupo 2025 akiamka ataona, unaweza kukuta anatumia simu ya dada yake na anaishi kwa shemeji wala usishangae! Muulize yeye anayo hiyo fremu tumuuingishe ndo utaona atakavyoingia chakaMkuu Mimi sijawahi kwenda kwenye hizo usahili thing tangu nimalize chuo miaka kadhaa iliyopita na wala sitawahi kufanya hivyo.
Na hii comment yako umeiandika kwakua wewe ni mbinafsi kwa maana unajiangalia tu wewe na kuifananisha au kutaka jinsi ilivyo wewe na wengine wawe kama wewe which is wrong.
Usichokijua ni kwamba vijana wengi wamesomeshwa na pesa za maandazi na vitumbua tena kwa kuunga unga sana, kwahiyo hizo habari zako za mtaani frem kibao na wateja kibao inawezekana ni sahihi(ingawa kwa Mimi nnaoujua mtaa hii point yako haina ukweli huo ambao wewe umeiandika nao) lakini watu hawana hiyo mitaji ya kukodisha hizo frem na kuweka mzigo waanze kufanya hizo biashara unazo sema.
Lakini pia wewe ni mbinafsi kwasababu unadhani Kila mtu anaouwezo wa kufanya biashara kama wewe.
Lakini pia ni dhahiri kuna jambo la muhimu ni either haulijua au unalijua ila haulichukulii serious ni kwamba vijana wengi wa kitanzania wakishafaulu na kujiunga na vyuo vikuu wanapoteza plan B zote za maisha na kubaki na hiyo plan A ya ajira na ndio maana walio wengi huwa wanakomaa ili watakapomaliza wapate sehemu ya kulipwa mshahara wa Kila mwezi.
Lakini pia ni dhahiri haujui ya kwamba pesa huwa iko na kawaida ya kumzingatia mtu ambae haizingatii na hii ni kitu ambayo watu wengi hawaijui na ndio maana vijana wengi wanaoingia kwenye upande huo wa kujiajiri huwa wanastruggle na kuuwa mitaji yao mara kadhaa kabla hawajajipata kibiashara na ndio maana walio wengi wanakua mguu ndani mguu nje kwa maana kijana anaweza akawa amejiajiri ila pia akiskia hizi ajira zimetangazwa ni haraka sana anatuma maombi.
Lakini pia usichokielewa ni kwamba asilimia karibia 90 ya vijana wa kitanzania huwa wanakwenda shule kwa lengo la wakimaliza waweze kuajiriwa katika taasisi za hapa na pale wafanye kazi, sasa mambo yakienda ndivyo sivyo huwa hata uwezo wao wa kufikiri unaharibiwa, kwa maana walio wengi wanakua na uhitaji mkubwa sana wa fedha baada ya kusubiri kwa muda fulani hadi pale ajira zinapotangazwa.
Mwisho ni kwamba ukiwa na uhitaji wa fedha kwa kiasi kikubwa huwa ni ngumu sana kujiajiri kwa maana ya kuwa mfanya biashara ila labda ujiajiri kwa maana ya kujitengenezea kazi wewe mwenyewe, na hauwezi kufanya hivi kama hauna mtaji ila pia lazima mjifunze kuiheshimu Juhudi za watu kwakutowashauri waende wakafanye kazi ambazo haziendani na hadhi ya elimu zao kwa lazima.
Kabisa mkuu, mtu anaejua maisha ya mtaani hawezi kuongea kama alivyoongea jamaa... Usikute ni wasira ameingia humu kutetea hoja zake🤣🤣🤣Atakua mccm huyu! Wanajua kila tatizo linatatuliwa kwa nyundo tu nayo wasira na polisi, msamehe bure! Out of contact with the reality, anaongea mambo ya 1971 wakati tupo 2025 akiamka ataona, unaweza kukuta anatumia simu ya dada yake na anaishi kwa shemeji wala usishangae! Muulize yeye anayo hiyo fremu tumuuingishe ndo utaona atakavyoingia chaka