Ajira hakuna ila kazi zipo nyingi sana vijana tutumie akili

Mbona wasomi muna uelewa mdogo sana,? Kazi zipo nyingi zaidi ya hizo huku mtaani kuna dada namfahamu anahudumia watoto saba kama house girl kwa mwezi anachukua hela wengine wanauza matunda, juice, salon n.k. kwa sasa idadi ya walimu inakaribia idadi ya wanafunzi, hata wakiajiriwa wengi bado wengine watakosa
 
. Nilicho gundua wewe unaangalia leo na jana, huna mawazo mbadala ya kupambana na ukosefu wa ajira Nchini,

. Kuna watu nyumbani kwao kuna lasilimali za asili ni nyingi kuliko kawaida lakini wameamua kuachana na hayo, then wakaenda kusomea fani za kuajiriwa..( mfano mdogo kuna jamaa nipo naye karibu hapa ana biashara ya duka limejaa lakini kutwa zima yupo kwenye interview


. Kwa hiyo unataka serikali iwaajiri wahitimu wote????
 
Kuajiriwa sio Serikalini tu, heshimuni hizo ajira zenu mnazozipata shule binafsi
Watu wanataka uhakika mkuu, unamuajiri mtu unampa mkataba wa mwaka mmoja, na kwenye sector ya elimu serikali inatakiwa iwe ndio muajiri mkuu na kwenye hiyo sector pamoja na ile ya afya watu walishazoeshwa hivyo, kwahiyo haya mabadiliko ingawa watu watayazoea ila yatachukua muda kidogo.

Kama inawezekana course ambazo hazina tija zingepunguzwa tu ili ziache kuendelea kurundika watu wengi mtaani, ofcoz serikali haiwezi kuajiri watu wote ila inaouwezo wa kujua watu wangapi ambao wana uhakika wa kuwasajiri Kila mwaka na wangetumia hili kutrack selection za wanafunzi kwenye vyuo mbalimbali katika Kila course ambazo wao ndio waajiri wakuu.

Angalau ile idadi ya kuajiri ambayo wao wana uhakika nayo waidouble au waitriple sio wahitimu laki mbili halafu ajira elfu kumi, hao laki na tisini wanaenda wapi? Kwa maana hata hizo sector binafsi haziwezi waajiri wote.

Au kwenye mifumo ya kuchagua course za kusoma chuo kikuu (TCU or NACTE) Kila course pale chini iweke uwezo wa serikali kuajiri Kila mwaka ni watu wa ngapi kwa wahitimu wa course hiyo na idadi kamili ya wanafunzi wanaochukuliwa nchi nzima itajwe ili mtu ajipime mwenyewe au achague kwa hali ya kujua angalau hii itapunguza taharuki.
 
Kwamba mtu asome miaka yote hiyo halafu awe house girl? Hizi mindset nazo nizakukemea... Kama wanajua walimu wamejaa kwanini wanaendelea kuwaruhusu watu wachukue hizo course za uwalimu? Kuna ulazima gani ya kujaza wasomi ambao hakuna pahala pa kuwatumia?
 
Zifutwe kwa muda kozi za ualimu,zibaki zinafundishwa hizo kazi NYINGI unazozisema.
 
Sijakataa na wala sijakupinga boss wangu, Nimeshauri tu mifano tunayotoa iwe realistic na inareflect watanzania wa kawaida. Hao wenye mifugo unayosema watoto wao hawana shida ya ajira kwa sababu wengi wapo connected na watawala na maccm! Hawa vijana wanaohangaika hapo hata kumaliza hizo shule wazazi wamepumua, hivi ni Watz wangapi wana hayo maduka na hiyo mifugo hadi wtt wao wote wakasome na warudi kuendeleza. Tunawakosea sana tunaposhauri tukiwa nje ya hali halisi! Hao vijana wote wanaograduate wakifanya bodaboda nani atakua mteja sasa? Waliopo tu ni chaos then uingize say hao walimu 200k waliofanya interview majuzi ni nini kitatokea? Mambo haya sio mepesi kama kutype hapa kwa keyboard kiongozi ukitafakari kwa kina
 
Kikwete atoe mbinu aliyotumia kuajiri waalimu wote.
Kwa Sasa wasomi ni wengi, tofauti na awamu ya Kikwete, nakumbuka kipindi cha Kikwete fani yetu watu walikuwa wanaajiriwa huku bado wapo darasani wanasoma(wakiwa mwaka wa mwisho walikuwa wanapata ajira) ...
 
Najua mkuu namna gani unasikia Uchungu kama Mtanzania, lakini mpaka Sasa mambo ni magumu tayari,

. serikalii imezidiwa,
. serikali haina mbadala wa ku waajiri wahitimu wote ,
. serikali inawaza uchaguzi zaidi na kujimilikisha mali kuliko maslahi ya wa Tanzania,
. Private sectors zimegeuza watoto wa maskini kama vitega uchumi vikuu
. Private sectors wanazidi kufungua college huku wanajua kabisa ajira hamna.
 
Private sector ya Tanzania ipo narrow sana Inatakiwa affirmative action ya serikali kupromote private sector kwa nguvu kubwa sana ili ikue! Tatizo inakua slow na serikali inaiumiza muda wote ikiongeza kasi watawala wanaipiga nyundo so vijana wanalazimika kuomba serikali tu ndio iajiri wakati nchi zote ajira kubwa zipo private sector, tunafanya matajiri maadui na mashetani huku tunataka pia watengeneze ajira
 
Ndiyo Nini hiki umecomment??
 
Ety watu wanaunda umoja wa waalimu wasio na ajira(NETO)

Hivi kazi zote hizi kitaa wewe una shahada unashindwa kufanya mpaka ulalamike??

Ajira hakuna ila kazi ni nyingi tumieni akili
Mkuu ifikie hatua waAfrika hasa sisi WaTz tuwe tunajaribu kutumia akili zetu kwa kina katika kufikiria mambo mbali mbali hasa yale yasiyohitaji kuweka masihala.

Hivi umepata nafasi ya kuwasikiliza hao vijana ukakaa chini ukafikiria kabisa yale waliyo yawasilishwa ukafikia muafaka kuwa walichokuwa wakikisema sio cha maana yaani haki make sense kabisa?.

JF ni jukwaa huru ila kwakweli kuna wanJF wengine hamna akili.
 
Hakika mkuu huyu kijana ni mpuuzi sana na bila shaka atakua hana elimu yoyote labda ya darasa la saba. Uwenda ni boda boda.
 
Mimi siungi mkono yanayo endelea ila ni bora ujishikize mahali kuliko kulalamika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…