Ajira mpya za Walimu wa Sekondari zasitishwa kwa muda ili kurekebishwa

Ajira mpya za Walimu wa Sekondari zasitishwa kwa muda ili kurekebishwa

Status
Not open for further replies.
Huu ni uzembe hicho chuo kilichowasilisha majina ya Mwaka Jana kimechukuliwa hatua gani? Na inakuwaje unawasilisha majina ya Nyuma hapa napata shaka inawezekana vilevile kuna watu wanapelekwa majina yao TAMISEMI hata chuo hawajagusa kwani Tamisemi hawafanyi verification ya Wahitimu TCU and a bit background ya sifa alizoingilia chuo Jamani hivi nchi hii Viongozi mnafikiri kwa kutumia nini! Maana ya Kuwa na E-Govenment ni nini? Kwa nini msiwe na software inayolink vyuo vyote nchini ambayo inakuwa na uwezo wa Ku export report zozote mnazozitaka ziwe za wahitimu au Taarifa zingine ambapo issue ya kuwapangia vituo walimu ingekuwa ya siku 2 au 3 tu

...Inawezekana Mkuu Kuwa Nahiyo Software Ila Sasa Magumashi Yatafanyikaje?
 
Nimasikitiko yangu kuona walimu wenzangu wa BEDECE UDSM ,mmewapa ajira walimu watano tu na kuacha zaidi ya 25.Waliobaki wanajiuliza ,mumezingatia vigezo gani kuwapa wachache na kuacha wengi bila ajira? au wao hawana haki ya kupewa ajira? Naomba wahusika mchukue hatu ilikuondoa utata. Nawasilisha.
 
walimu kibao wamekosa tena wa vyuo vingi tu so ni bahati nasibu
 
Hv walimu wenzangu hebu tufikirie! Hiv n kweli chuo kinaweza kuwasilisha majina ya mwaka juzi badala ya wahitimu wanaotarajiwa???? Je hyo sekuco ina utaratibu gani wa ajabu kiasi hcho?? Kama ni kweli kwann tamsemi waondoe majina yetu kwa mda wakat tatzo ni la chuo???? Hapa n changa la macho....mr j4 sagin kuwa wazi
 
Vipi kaka unadhani watakuwa wanafanya nini mi nadhani tuvute subira watakuwa ni kweli wanafanya marekebisho
 
Jamani waalimu nendeni Kuripoti mbona tangazo lipo wazi wanaohusika ni waanafunzi Wa secuko tu,kama uliona jina Na sehemu uliyopangia hujaambiwa usiende kuripoti.eleweni kiswahili wandugu tarehe mosi kuripoti hakuna tamko lililotolewa kukanusha kuhusu kuripoti.
 
majina 491 yatibue majina maelf na maelfu hata kama uoni papasa utagusa
 
Hawa walimu wetu hawa nina mashaka nao lile tangazo halijasema kuwa ajira zenu zimesitishwa bali limesema kuwa "kuondolewa kwa muda majina" na wala sio kusitoshwa kwa ajira mbona nyie walimu hamjiamini mnaboa sasa embu jiaminini.
 
Wanarekebisha mpaka wa sapu walioclear so wanaingiza majina upya,kazi ngumu kidogo hapo...
Vuteni sibira
 
majina 491 yatibue majina maelf na maelfu hata kama uoni papasa utagusa
Chichimizi rafiki yangu acha uoga unapaswa kujua unapoweka majina katika list ili kuyachomoa ni lazima kufanya editing sasa unafikiri watafanyaje editing majina yakiwa hewani so vuteni subira mtajipa stress bure hlf baadaye majina yatolewe tena mr jumanne sagini hawezi kudanganya umma wa watanzania na tangazo liko wazi limeelezea matatizo ya uongozi wa sekomu katika kupeleka majina sahihi wizarani.
 
Tangazo mbona liko wazi tu ni marekebisho ya kuondoa wale wazamani wa secuko na kuingiza wapya kama alivyosema mdau ila vituo ni vilevile na hata kuripoti wanaweza wasibadili coz wengi washajua kuwa Kuna kuripoti au wanaweza ongeza pia Sio mbaya tuwe na subira#dah walimu wa mwaka huu watata sana.
 
Concern ya Chichimiz naiyona ipo vzr hta mm nlijiuliza hvo bt nkaona kama vle co kuna chezo la kupnduapndua linaweza kutokea kwmba mwanzon ulipangiwa Moro baada ya chezo unajkuta umepangiwa Roryaa. Ila najiuliza ktu kimoja tu kuripot kuko palepale tar.1/5 wadau???
 
Hawa walimu wetu hawa nina mashaka nao lile tangazo halijasema kuwa ajira zenu zimesitishwa bali limesema kuwa "kuondolewa kwa muda majina" na wala sio kusitoshwa kwa ajira mbona nyie walimu hamjiamini mnaboa sasa embu jiaminini.

Unanipa mashaka na uelewa wako mdogo but sio kosa lako may be hujasoma tangazo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom