Ajira za bara tunaomba wote, lakini za Zanzibar wanataka Mzanzibar pekee
Kumbuka lengo la muungano haikuwa ni kuimeza Zanzibar, japokuwa hapa ni kama Tanganyika ndio imemezwa. Watanganyika tumekuwa watanzania na wazanzibari wao wamebaki vile vile.
Suala hili la Muungano Lina kizungumkuti kikubwa sana, ni mtu mwendawazimu tu ndiye ambaye anaweza kulielewa vizuri.

Kuna mbunge mmoja kutoka Zanzibar alitoa Hoja bungeni anataka Watanganyika waingie Zanzibar kwa Viza, Sasa unajiuliza ;Je, Wazanzibari nao waingie Tanganyika kwa Visa? Kama jibu ni ndiyo, Kuna maswali mengine mengi sana yaliyo magumu yanaibuka. Mathalani, tukikubaliana kuweka utaratibu wa Viza kwa kuingia Zanzibar na Tanganyika, maswali yatayoibuka ni:- Je, endapo kama sisi Watanganyika tutaamua kuwanyima Viza Wazanzibari hali itakuwaje kwa wale Wazanzibari ambao wanafanya kazi katikà Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa huku Tanganyika?? Kwa Mfano, Watanganyika tukiamua kumnyima Viza huyu Rais aliyopo madarakani ambayo ni Mzanzibari ili asiingie Tanganyika, Je, atawezaje kuiongoza nchi hii ukizingatia kwamba atalazimika kubaki Zanzibar pekee bila kuingia Tanganyika kutokana na kukosa Viza ya kumruhusu kuingia ndani ya Ardhi ya Tanganyika?????

Yaani Muungano huu ni Vurugu mechi!
 
Kumbuka lengo la muungano haikuwa ni kuimeza Zanzibar, japokuwa hapa ni kama Tanganyika ndio imemezwa. Watanganyika tumekuwa watanzania na wazanzibari wao wamebaki vile vile.
Hahaha asante kwa kuongea kwa adabu.....lengo haikuwa kuimeza zanzibar lakini Tanganyika imemezwa.

Ugomvi wa Mamba na Chatu huu.
 
Haya majitu mabinafsi sana.., sasa huo Muungano tunaoambiwa ni upi? Na huku bara likitolewa tangazo waseme wabata tu ndio wanaruhusiwa then kuna Muungano gani hapo?!
 
Back
Top Bottom