Ikiwa Wazanzibari wanaruhusiwa kuapply kazi za Tanganyika, na wengi tu wameajiriwa huku Tanganyika, ni kwa nini ajira za Zanzibar ziwekewe kigezo cha "Awe Mzanzibari"?
Mbona ajira za Tangayika zikitoka kigezo kinakuwa "Awe Mtanzania" (Haijalishi anatoka Tanganyika au Zanzibar).
Hii kitu usoni watu wanaweza wakawa wanacheka lakini mioyoni mwao hawaifurahii kabisa.
HII NI RACISM YA WAZI KABISA.
Ili nchi iweze kuwa moja na kuondoa racism, inabidi kuwepo na mchanganyiko wa pande zote 2, wa huku awe huru kwenda kule, na wa kule aje huku bila kuwepo ubaguzi wa aina yoyote ile.
Mbali na hapo, huu Muungano ni suala la muda tu, hautafikisha hata miaka 100 utavunjikia mbali.
View attachment 3070521