Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Noma sanaTapeli huyu
Juzi nilimcheck nikamtumia cv yangu ya kazi ya uhasibu,akaniomba laki 1 ili tu eti anipe kazi..nikamwambia simpi hata mia mbovu.akaniblock.
Kuweni makini sana na huyu mtu.
Labda sio Abdul Ghafur uliyekumbana nae?Tapeli huyu
Juzi nilimcheck nikamtumia cv yangu ya kazi ya uhasibu,akaniomba laki 1 ili tu eti anipe kazi..nikamwambia simpi hata mia mbovu.akaniblock.
Kuweni makini sana na huyu mtu.
"Shaka" la nini? Kwanini uwe na shaka kama unaimudu kazi yako na unaufahamu uwezo wako?Shaka hilo
Ndivyo tufanyavyo hivyo. Tusome vizuri post zetu.Mkuu kwa kazi kama store keeper na personal assistant zinatrainika hata mtu akikosa uzoefu na ubobezi.
Wape nafasi vijana
Unaonesha hujapitia uzi vizuri, hili si jukwaa la siasa. Soma...Acha siasa,weka details za kampuni yako watu tuijue kiundani.
Shaka lipo sana hapo, company bila kuwa scale maalum ya ulipaji inatia shaka."Shaka" la nini? Kwanini uwe na shaka kama unaimudu kazi yako na unaufahamu uwezo wako?
Kama una shaka usije. Ukishaanza kuwa na mashaka basi utakuwa ni mtu wa mashaka mashaka, ukiwa na shaka na kitu usikifanye. Unachotakiwa uulize kwa usilolijua, usiwe na mashaka. Muono wako ni mwengine na hatuwezi kufanana miono yetu kama vile ambavyo DNA zetu haziwezi kufanana.Shaka lipo sana hapo, company bila kuwa scale maalum ya ulipaji inatia shaka.
Acha uongo, kama umeshindwa hizo nafasi waachie wengine watakaoweza. Mzee Abdul namfahamu hawezi kukutapeli hata senti yako hana shida hizo na pia hahitaji cv sasa imekauje wewe ukaombwa cv. Nakushauri kuwa hili jukwaa lina watu wa aina tofautitofauti sio kila unayemuona ni muhuni au tapeli, kuna watu wamepata kazi za mishahara mikubwa kupitia wanachama wa hilihili jukwaa. Jifunze heshima mkuu.Tapeli huyu
Juzi nilimcheck nikamtumia cv yangu ya kazi ya uhasibu,akaniomba laki 1 ili tu eti anipe kazi..nikamwambia simpi hata mia mbovu.akaniblock.
Kuweni makini sana na huyu mtu.
We jamaa unashangaza sana, unataka mzoefu wa kazi, mtu ameweka CV hutaki, sasa utajuaje kwamba ni mzoefu? au hujui maana ya CV?Labda sio Abdul Ghafur uliyekumbana nae?
Kwanza sisi hatuulizi CV ya mtu, sijui ni nani alikudanganya kuwa inayoajiriwa ni cv? Pili, nakumbuka kuna mtu katuma cv nikamuuliza nani kakuambia utume cv? akanambia "just ignore", nikamjibu "ignored" akaniita "tapeli" Nahisi ni wewe na hilo la kuambiwa utume l;aki moja ni uongo wa wazi kabisa, labda ulipigiwa na matapeli.
Kama huyo ni wewe, kweli kabisa nime ku block. You were just wasting precious time and you've asked yourself to be ignored. I did better to block you.
Niianike namba yangu JF kwa miaka sasa, picha yangu halisi, niandike humu mpaka anuani za nilipo halafu nikutapeli laki moja.
Kijana kama ndio hizo njia zako za kuomba kazi, basi nakutakia mema.
Wengi wa vijana hamna muelekeo wala hamja fundishwa namna ya kutafuta kazi, sio makosa yenu, faiza Foxy anasema tatizo ni shule za "kusomea ujinga".
Kama unamfahamu sio tapeli basi hawezi kabisa kujieleza, tangazo liko hovyo mno. Awaachie watu wanaoweza kujieleza vizuri.Acha uongo, kama umeshindwa hizo nafasi waachie wengine watakaoweza. Mzee Abdul namfahamu hawezi kukutapeli hata senti yako hana shida hizo na pia hahitaji cv sasa imekauje wewe ukaombwa cv. Nakushauri kuwa hili jukwaa lina watu wa aina tofautitofauti sio kila unayemuona ni muhuni au tapeli, kuna watu wamepata kazi za mishahara mikubwa kupitia wanachama wa hilihili jukwaa. Jifunze heshima mkuu.
Usemacho ni sahihi labda tuseme mzee huwa haelezi mambo yakanyooka na hii ni kutokana na kwamba huwa anaandika mara nyingi humu kuhusu hayo mambo. Ukienda utajionea mengi sana vijana wanajifunza ufundi mbalimbali kwa vitendo tena bure na wanafundishwa na vijana wenzao ambao ndio hao wanatafutwa kwa malipo yaani mshahara kabisa. Hiyo ni taasisi ya dini yenye lengo la kusaidia vijana kupata ujuzi nje ya mfumo rasmi.Kama unamfahamu sio tapeli basi hawezi kabisa kujieleza, tangazo liko hovyo mno. Awaachie watu wanaoweza kujieleza vizuri.
Nimekuelewa sana tu ila nataka kujua, je hao wahasibu unaohitaji kwa majukumu unaowahitajia mnawalipa Tsh ngapi endapo wataperform kama unavyotaraji?Kama una shaka usije. Ukishaanza kuwa na mashaka basi utakuwa ni mtu wa mashaka mashaka, ukiwa na shaka na kitu usikifanye. Unachotakiwa uulize kwa usilolijua, usiwe na mashaka. Muonowako ni mwengine na hatuwezi kufanana miono yetu kama vile ambavyo DNA zetu haziwezi kufanana.
Unaonesha unahitaji mafunzo zaidi za namna ya malipo yaliopo dunia ya leo. Hata marehemu Magufuli amelisema mara chungu nzima, "utalipwa kwa uwezo wako" sio kwa jina lako au jina la kazi.
Unaonesha haufahamu maana ya "performance-based payments". Tunacholipa ni kwa kazi aifanyayo mtu si kwa jina la kazi aifanyayo.
Unaweza kuwa mhasibu lakini wakati huo huo huo u8nafanya na kazi za utawala, procurement, operations, sasa tukuloipe kama mhasibu ambae anafanya data entry tu?
Hata wahasibu, wapo wa uwezo tofauti na ujuzi na uzoefu tofauti, unataka wote walipwe namna moja?
Nikuulize maswali? Umeshafanya kazi zipi na wapi na kwa miaka mingapi?
Lazima unishangae sana, kwa sababu mawazo yako na mawazo yangu ni tofauti, muono wako na muono wangu ni tofauti. Badala ya kunishangaa niulize kwanini sihitaji CV za watu. Kuhusu CV, kuna uwezekano mkubwa maana ya CV uijuavyo wewe na niijuavyo mimi tunatofautiana, kwa kuwa hata herufi CV ni kifupisho cha maneno ya lugha za kigeni. Nijuavyo mimi maana ya "CV" ni utambulisho wako binafsi, kama ulivyouandika au kuandikiwa. Utambulisho wetu tunaufanya kwa kutambuana ana kwa ana. Uzoefu wa kazi huonekana ufanyapo kiazi, kwetu kuna "orientation" ya wiki mbili itayotudhirishia uzoefu wako wa kazi. CV sio uzoefu wa kazi.We jamaa unashangaza sana, unataka mzoefu wa kazi, mtu ameweka CV hutaki, sasa utajuaje kwamba ni mzoefu? au hujui maana ya CV?
Umeulizwa mshahara unazugazuga tu, si useme tu kwamba ni commission watu waelewe?
Au kweli wewe ni Tapeli, hata kama ni wale watu wa kuuza vyombo mitaani, haiwezekani kusiwe na jina la kampuni! Anyway sikulaumu, maisha ni magumu. Wapige hela hao watakaokubali kupigika.
Hakuna kikomo cha malipo kwenye system yetu ya "performace based". Ukifika hapa kufanya orientation utayaelewa yote. Ni vigumu sana kukufahamisha kwa maandishi kwa upande wangu, Sisi hupendelea zaidi kufanya vitu kwa vitendo.Nimekuelewa sana tu ila nataka kujua, je hao wahasibu unaohitaji kwa majukumu unaowahitajia mnawalipa Tsh ngapi endapo wataperform kama unavyotaraji?
Amesema hataki utume maombi..amesema wewe mcheck tu watsap muulizane maswali then utaratibu mwingine utafuata.Hello nafasi bado zipo nataka kutuma maombi
Na mnachukua wakristo kweli, maana naona ni taasisi yenye jina la kiislamu?Hakuna kikomo cha malipo kwenye system yetu ya "performace based". Ukifika hapa kufanya orientation utayaelewa yote. Ni vigumu sana kukufahamisha kwa maandishi kwa upande wangu, Sisi hupendelea zaidi kufanya vitu kwa vitendo.
Poa asanteAmesema hataki utume maombi..amesema wewe mcheck tu watsap muulizane maswali then utaratibu mwingine utafuata.