Ajira za Uhasibu (Accountant), Store Keeper na Personal Assistant

Ajira za Uhasibu (Accountant), Store Keeper na Personal Assistant

ANGALIZO : Huyu mtu ni TAPELI yeye na genge lake wako pale jirani na shule ya msingi Misugusu! Najuta!

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
You are right. Lakini umekosea kidogo, tupo mbali na shule isipokua kufika kwetu njia mojawapo ni ya kuingilia shule ya msingi Misugusugu. Zipo na nyingine, unaweza kuingilia Kilimahewa, unaweza kungilia Check point, unaweza kuingilia kwa Sharrifu. Nikuongeze njia za kufika Madrassatul Abraar?

Tunaitwa Madrassatul Abraar.

Kipaumbele kwa sasa ni watu wa IT, wahasibu, wahasibu wasaidizi, watu wa logistics and supplies, site foreman wa ujenzi. Mafundi ujenzi wenye uzoefu na wasio na uzoefu lakini wenye Nia na wataopenda kujifundisha ujenzi Kwa vitendo. Wake kwa Waume.

Wasiliana nasi kwa WhatsApp 0625249605.

Tupo mtaa wa Vitendo, kata ya Misugusugu, wilaya ya Kibaha,mkoa wa pwani.

Stendi inaitwa Miyomboni Shule au Misugusugu Shule ya msingi.

Ukija unakuja na barua ya utambulisho wa Serikali ya mtaa.
 
Ana majivuno halafu hamna kitu
Angekua na ofis nzur uyu angetoa watu roho hayo mabanda lkn anvyoongea kwa nyodo [emoji3][emoji3]
You are right.

Kuna cha ajira hapo kweli mkuu au chenga tu?
Tunaitwa Madrassatul Abraar.

Kipaumbele kwa sasa ni watu wa IT, wahasibu, wahasibu wasaidizi, watu wa logistics and supplies, site foreman wa ujenzi. Mafundi ujenzi wenye uzoefu na wasio na uzoefu lakini wenye nia na wataopenda kujifundisha ujenzi Kwa vitendo. Wake kwa Waume.

Pia tunawapa fursa vijana waliomaliza vyuo na hawana uzoefu, wanachukuliwa kama "apprentices". Pia unawapa fursa wale wenye ujuzi wao lakini hawajafanikiwa kupata kazi wazitakazo na wapo "maweni", wamekwama, hawa tunachukua kama sehemu ya kuwapa faraja wawe wanajipatia japo vijisenti kidogo huku wanaendelea kutafuta ajira wazipendazo.

Wasiliana nasi kwa WhatsApp 0625249605.

Tupo mtaa wa Vitendo, kata ya Misugusugu, wilaya ya Kibaha,mkoa wa Pwani.

Stendi inaitwa Miyomboni Shule au Misugusugu Shule ya msingi.

Ukija unakuja na barua ya utambulisho wa Serikali ya mtaa.
 
Lazima unishangae sana, kwa sababu mawazo yako na mawazo yangu ni tofauti, muono wako na muono wangu ni tofauti. Badala ya kunishangaa niulize kwanini sihitaji CV za watu. Kuhusu CV, kuna uwezekano mkubwa maana ya CV uijuavyo wewe na niijuavyo mimi tunatofautiana, kwa kuwa hata herufi CV ni kifupisho cha maneno ya lugha za kigeni. Nijuavyo mimi maana ya "CV" ni utambulisho wako binafsi, kama ulivyouandika au kuandikiwa. Utambulisho wetu tunaufanya kwa kutambuana ana kwa ana. Uzoefu wa kazi huonekana ufanyapo kiazi, kwetu kuna "orientation" ya wiki mbili itayotudhirishia uzoefu wako wa kazi. CV sio uzoefu wa kazi.

Uzoefu wetu umetufundisha kuwa wengi wanaandikiwa CV na hawaandiki wenyewe na wengi hawaelewi hata kilichoandikwa humo ni nini.

Ngoja nikupe kisa kimoja cha CV kati ya vingi nilivyonavyo; Kuna kijana alikuja kwetu na kitu cha kwanza kanipa bahasha, nikamuuliza ina nini? akanambia CV na kopi za vyeti vyangu, nikamwambia baki na bahasha yako, nipe CV tu, akanitolea CV ina page 3. Nikaipitia haraka haraka, nikakutana na kipengele kinachosema kuwa yeye ni mwanamichezo na anapenda sana kucheza mpira wa kikapu (basket ball) na amekua kwenye mchezo huo kuanzia shule ya msingi. Nikaona safi sana, hapa tumepata kijana ataetufundishia vijana wengine kucheza mpira wa kikapu. Bahati, hapa kwetu tulikua na mpira wa kikapu kati ya vifaa vingi vya michezo tulivyo navyo kwa ajili ya watoto, wanafunzi wetu wa madarasa ya Qur'an. Tukampa mpira tukamwambia tuoneshe uwezo kidogo hapo uwanjani. Akabaki anatutazama kama mjusi anavizia nzi ukutani. Nikamuuliza, vipi, tuoneshe mambo. Akasema yeye aliikopi tu cv na kubadili jina na mambo mengine, hilo la mpira wa kikapu lilimpita.

Mambo kama hayo na mengine mengi yametufanya tusiulize cv ya mtu ya maandishi mpaka awe kamaliza orientation ya wiki mbili na sisi, na ndani ya hizo wiki mbili, kama itahitajika, huwa tunamuelekeza namna ya kuipangilia CV yake kwa namna ya sisi tuwekavyo kumbukumbu zake kwenye files zetu za kielektroniki.
Ok, hapa umefafanua.

Mwanzo ulisema tu kuwa ni nafasi za kazi, ulipaswa kusema kuwa ni taasisi ya dini, kuna wengine hataki kufanya kazi na taasisi za dini, hivyo ungewapotezea muda wao kutuma maombi.

Kila la kheri, lakini msije mkafundisha watoto imani kali, extremism sio kitu kizuri.
 
Nilishawahi ingia chaka nikafika bana kwa uyu mzee nilijuta kwanza mazingira ya kihuni sanaa
Anakufanyia interview uku anakula fegi balaa....
Kwel kazi tunatafuta lkn nilijikuta nataka kuaga mwenyewe[emoji3]
Ungefafanua kabisa shida ni nini, 1)hizo kazi anazosema hakuna? 2) hawalipi? au tatizo ni nini?
Au kilichokukera wewe ni mafegi tu?
 
Ana majivuno halafu hamna kitu
Angekua na ofis nzur uyu angetoa watu roho hayo mabanda lkn anvyoongea kwa nyodo [emoji3][emoji3]

Hahahaha. Imekuja umeshindwa hata kutambua kuwa umekuja construction site?

Inabidi nicheke Tu. Ulitegemea ukute office aina ipi kijana?
 
Ok, hapa umefafanua.

Mwanzo ulisema tu kuwa ni nafasi za kazi, ulipaswa kusema kuwa ni taasisi ya dini, kuna wengine hataki kufanya kazi na taasisi za dini, hivyo ungewapotezea muda wao kutuma maombi.

Kila la kheri, lakini msije mkafundisha watoto imani kali, extremism sio kitu kizuri.
Watoto wanafundishwa "Imani Kali" na media. Siyo Madrassa.

Vipi Yule aliyemuua mama'ke Kaskazini huko kwa kutaka pesa? Alifundishwa na nani? Au ile sio "Imani Kali"?
 
Ungefafanua kabisa shida ni nini, 1)hizo kazi anazosema hakuna? 2) hawalipi? au tatizo ni nini?
Au kilichokukera wewe ni mafegi tu?
Ni kwel mafegi yalinikwaza sanaa
Ila sio official office kama anavyotangaza hapa hata kama atakuajiri inawezekana ikawa kakuajiri kama housegirl ni sehemu ambayo hamna mfumo wowote ... Hapo anapokuambia mnafanya orietation week hapo ndo anapokufukuza kwani
1. Jamaa ni mjuaji balaa kila kitu anajua halafu halafu apo yy sio kila kitu kuna mfadhil msomali mwenziwe yupo njee yy ndo ana support
2. Mshikaj ana Gubu balaa kias kwamba mkipishana kidogo anakutoa
Halafu anavyoongea kama na fustrustion hiv
Sidhani kama ashajiri mfanyakaz akadum hata mwaka mmoja
 
Ni kwel mafeg yalinikwaza sanaa
Ila sio official office kama anavyotangaza apa ata kama atakuajir inawezekana ikawa kakuajir kama housegirl ni sehem ambayo hamna mfumo wowote ... Hapo anapokuambia mnafanya orietation week hapo ndo anapokufukuza kwan

Huyo anavyoonekana hawezi kudumu na mfanyakazi anaejielewa hata dakika moja.
 
Ni kwel mafeg yalinikwaza sanaa
Ila sio official office kama anavyotangaza apa ata kama atakuajir inawezekana ikawa kakuajir kama housegirl ni sehem ambayo hamna mfumo wowote ... Hapo anapokuambia mnafanya orietation week hapo ndo anapokufukuza kwan
1. Jamaa ni mjuaji balaa kila kitu anajua halafu halafu apo yy sio kila kitu kuna mfadhil msomali mwenziwe yupo njee yy ndo ana support
2. Mshikaj ana Gubu balaa kias kwamba mkipishana kidogo anakutoa
Halafu anavyoongea kama na fustrustion hiv
Sidhani kama ashajiri mfanyakaz akadum hata mwaka mmoja
You are right.
 
Tapeli huyu
Juzi nilimcheck nikamtumia cv yangu ya kazi ya uhasibu,akaniomba laki 1 ili tu eti anipe kazi..nikamwambia simpi hata mia mbovu.akaniblock.
Kuweni makini sana na huyu mtu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nafasi zipo.

Kwetu hakuna utaratibu wa kutuma maombi, tunaamini anaeombwa ni Mwenyezi mungu tu. Tuwasilianee whatsapp 0625249605.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu mimi alishaniingiza chaka nilienda siku moja nafikir mwaka jana nilijua kwel ni taasis lkn nilifika jamaa yupo ome pembeni ndo kuna magofu ya hiyo taasisi
Jamaa anatokea chumban na ma fegi anakuhoji kwa dharau sanaa utafikir amepak gar apo njee
An sikushaur ata kama hiyo taasis itakua inafanya kazi huyu msomali ni kanjanja tu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Watoto wanafundishwa "Imani Kali" na media. Siyo Madrassa.

Vipi Yule aliyemuua mama'ke Kaskazini huko kwa kutaka pesa? Alifundishwa na nani? Au ile sio "Imani Kali"?
Kuua kwa kutaka pesa sio imani kali, huo ni uhalifu tu.

Imani kali ni kuua kwa kudhani kuwa unatetea dini na kwamba utaenda peponi.
 
Back
Top Bottom