Akamatwa akiwa na milioni 29 Gest

Akamatwa akiwa na milioni 29 Gest

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Mkazi wa Jijini Dar es salaam amekamatwa na Polisi Mkoani Njombe akiwa na Tsh. 29,374,000 katika nyumba ya kulala Wageni (Gesti) Mjini Makambako ambapo fedha hiyo inadaiwa ameipata kwa njia ya wizi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga, amesema wamemkamata Mwakatundu wakiwa wanafanya upekuzi wa kawaida katika nyumba za kulala Wageni ambapo baada ya mahojiano amekiri kuipata fedha hiyo kwa njia ya uporaji.

“Tulipofika katika nyumba ya kulala Wageni ambayo inaitwa Lisbon ndio tulifanikiwa kumkamata akiwa na fedha hiyo lakini baada ya kumuhoji kwa kina alieleza kwamba fedha hizo amezipora katika kampuni aliyokuwa anafanyia kazi ya Interchick Dar es Salaam”

Amesema tayari Mtuhumiwa amekwishakabidhiwa kwa Jeshi la Polisi Mkoani Dar es salaam kwa ajili ya hatua nyingine za kimashtaka ili aweze kufikishwa Mahakamani.
 
Mkazi wa Jijini Dar es salaam amekamatwa na Polisi Mkoani Njombe akiwa na Tsh. 29,374,000 katika nyumba ya kulala Wageni (Gesti) Mjini Makambako ambapo fedha hiyo inadaiwa ameipata kwa njia ya wizi...
Upekuzi wa kawaida kwenye nyumba za wageni? Hawa polisi ni hovyo sana. Wangesema walikuwa na taarifa hilo ningeelewa!
 
Unakamatwaje kifala hivi...?? Yaan utoke nazo dar mpaka makambako na unaenda guest....kwan angechepuka tuu pale mafinga akaingia sao hill kule nan angemshtukia...
Huenda kuna watu walikuwa wanajua nyendo zake na habari zake zilikuwa zinajulikana na wengi. Navyowajua polisi wetu siyo rahisi kuachia fedha nyingi kama hizo. Ama wangemwambia agawane nao ili wamwachie au wangemuua na kusingizia ni jambazi na fedha wazichukuwe.
 
Ukute alikuwa na 169m hawa polisi wa Tz hawa!

Yaani hakuna kesi, hakuna mlalamikaji, hakuna mashtaka ila ukaguzi tu wa kawaida polizei wa bongo wakukute na 29 alafu wakukamate tu eti ndio waanze kukuhoji! Na watangaze ukweli kabisa kuwa una 29 na kweli uwe na 29!

Haya bana
 
Mkazi wa Jijini Dar es salaam amekamatwa na Polisi Mkoani Njombe akiwa na Tsh. 29,374,000 katika nyumba ya kulala Wageni (Gesti) Mjini Makambako ambapo fedha hiyo inadaiwa ameipata kwa njia ya wizi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga, amesema wamemkamata Mwakatundu wakiwa wanafanya upekuzi wa kawaida katika nyumba za kulala Wageni ambapo baada ya mahojiano amekiri kuipata fedha hiyo kwa njia ya uporaji.

“Tulipofika katika nyumba ya kulala Wageni ambayo inaitwa Lisbon ndio tulifanikiwa kumkamata akiwa na fedha hiyo lakini baada ya kumuhoji kwa kina alieleza kwamba fedha hizo amezipora katika kampuni aliyokuwa anafanyia kazi ya Interchick Dar es Salaam”

Amesema tayari Mtuhumiwa amekwishakabidhiwa kwa Jeshi la Polisi Mkoani Dar es salaam kwa ajili ya hatua nyingine za kimashtaka ili aweze kufikishwa Mahakamani.
Huyu jamaa watakuwa wamempora pesa nyingi halafu ubaoni ndio anapelekwa na hiyo.

Sasa kama kuna ndugu zake humu mwambieni akubali ni kweli lakini awaambie pesa zote zirudishwe kwanza ndio asaini hati ya mashtaka wakapane mahakamani.

Kuna huyu mwamba amfundishe mbinu.

Mtanzania, Denis Mfumbulwa (44) anayedaiwa kujipatia huduma ya kula katika Hoteli ya Serena bila kulipa, ameachiwa huru katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo jijini Dar es salaam kwa sababu hakuna ushahidi wa kuthibitisha kama kesi hiyo dhidi yake ni ya jinai.

Mfumbulwa ambaye ni Mkazi wa Goba ameachiwa leo na Hakimu Gladness Njau wakati kesi hiyo ilipoitwa mahakamani hapo kwa ajili ya kusikilizwa.

Mapema Meneja wa Hoteli hiyo, Desdery Doto alifika Mahakamani hapo kutoa ushahidi ambapo alipoulizwa alidai Mshtakiwa alifika hotelini hapo na kupata huduma ya chakula na malazi bila kulipa na kisha akatoweka.

Kufuatia maelezo hayo, Hakimu Gladness Njau alimuachia huru Mshtakiwa huyo akisema “inaonekana asili ya shauri hili ni la madai na siyo jinai hivyo kama Mlalamikaji ataona inafaa afungue kesi ya madai”

Katika kesi hiyo Mshtakiwa Mfulumbwa anayeishi Goba Kulangwa anadaiwa kuwa Machi 6,2022 hadi Machi 28,2024 kwa nyakati tofauti katika Hoteli ya Serena Wilaya ya Ilala, Dar es salaam alijipatia huduma ya malaz
IMG-20240515-WA0113.jpg
 
Back
Top Bottom