Kama nimemuelewa mtoa mada, hajasema kufungia kazi zao bali kudili na nidhamu na tabia zao wengi tabia zao mbaya,, na kinacho wapa jeuri ni ule wanaita umoja wao wa kishamba kwamba ukizinguana na mmoja wanakuja mia,,Sasa fikiria hizo akili zote zihamie kwenye ukabaji
Hujamuelewa tuKwenye ndoa yako bodaboda wanahusika vipi? Hizi lawama nyingine zimevuka mipaka
Si kwamba wapigwe marufuku hapana wathibitiwe kwa sheria kali tu mbona Rwanda🇷🇼 bodaboda wako vizuri kabisa njoo hapa sasa bodaboda imekuwa chaka la walevi vibaka majambazi wauza madawa ya kulevya wasafirisha magendo yasiyofuata sheria za usalama barabarani yaani ni kama watu waliokata tamaa na maisha wanejitoa muhanga kwa loloteUnajua bodaboda zikiwa 2milions zimeiokoa kwa kiasi gani serikali na upungufu wa ajira na je zikitolewa nini itakua mbadala wa ajira na usafiri wa haraka na nafuu adi vichochoroni?
Wapo bodaboda wanaojitambua na wanajali kazi yao ila hawa wenye walioachia nywele kama makinda ya ndege hapanaWadau mnamshambulia na kushupaza mishipa ya shingo, hebu msome mmalize na muelewe. Kasema angalau awabadilishe na kuwa wafuataji sheria na wenye maadili.
Sawa boda ni ajira na inaokoa vijana wengi mjini, kwa mantiki hii waachwe kupunguza msongamano wa wasiyo na ajira.
Ila hii isiwe sababu ya kuleta mazoea na wake za watu hadi kuwagonga, kutia mimba wanafunzi au kuwafanya wasifike shuleni kwa wakati.
Pia isiwe sababu ya kutotii sheria unakuta taa nyekundu simama na tii, unataka kuingia barabara kuu, subiri aliyepo huko akuruhusu hii ndiyo sheria, ya priority barabarani hutaka hivyo, si kuchomekea na kusababisha ajali zisizo na msingi halafu hodari wa kukimbia kuachia watu misala. Bado kosa likiwa la mmoja wao wanachoma hadi magari ya watu moto.
Tunawaheshimu ni fighter kama wengine mnaleta msosi mezani kwa wake na watoto wenu, mabachela mnakula hadi kuvaa hapohapo. Ila mkumbuke hizi barabara hamjaumbiwa nyinyi mpaka mfanye mnavyotaka.
Wacheni michezo ya kushindana na magari wakati wewe body ni mwili wako, mnaongeza idadi ya wajane, mayatima na wazazi wenye misongo ya mawazo.
Tiini sheria, ukipenda sketi ya shule mpe mkeo avae kiila ukirudi ndani, zipu yako ichunge wake za watu kisa kupanda bure.
Shenzi kabisa uzuri wao ndiyo wasifuate sheria za usalama barabaraniLakini Kuna wakaka wazuri huko
Bangi na pombe ndiyo shida hii kazi imeshakuwa kichaka cha vibaka majambazi wauza madawa kusafirisha magendoKuna uhusiano gani kua boda boda na kua mhuni ,mchafu, kua na tabia mbaya
Ni kwamba kuna athari ukianza kua boda boda unazipata hivi hili kundi shida ni nini?
Au bange na pombe ?