Wadau mnamshambulia na kushupaza mishipa ya shingo, hebu msome mmalize na muelewe. Kasema angalau awabadilishe na kuwa wafuataji sheria na wenye maadili.
Sawa boda ni ajira na inaokoa vijana wengi mjini, kwa mantiki hii waachwe kupunguza msongamano wa wasiyo na ajira.
Ila hii isiwe sababu ya kuleta mazoea na wake za watu hadi kuwagonga, kutia mimba wanafunzi au kuwafanya wasifike shuleni kwa wakati.
Pia isiwe sababu ya kutotii sheria unakuta taa nyekundu simama na tii, unataka kuingia barabara kuu, subiri aliyepo huko akuruhusu hii ndiyo sheria, ya priority barabarani hutaka hivyo, si kuchomekea na kusababisha ajali zisizo na msingi halafu hodari wa kukimbia kuachia watu misala. Bado kosa likiwa la mmoja wao wanachoma hadi magari ya watu moto.
Tunawaheshimu ni fighter kama wengine mnaleta msosi mezani kwa wake na watoto wenu, mabachela mnakula hadi kuvaa hapohapo. Ila mkumbuke hizi barabara hamjaumbiwa nyinyi mpaka mfanye mnavyotaka.
Wacheni michezo ya kushindana na magari wakati wewe body ni mwili wako, mnaongeza idadi ya wajane, mayatima na wazazi wenye misongo ya mawazo.
Tiini sheria, ukipenda sketi ya shule mpe mkeo avae kiila ukirudi ndani, zipu yako ichunge wake za watu kisa kupanda bure.